Pole January Makamba

Kaka nimekulewa. Nadhani ni suala la "methodology" iliyotumika. Wewe unashauri alete maswali na majibu. Upo sahihi. Lakini nadhani mleta mada alikuwa anahofia usalama wake. Manake siku hizi watu wanamwagiana tindikali mchana kweupe.


Wabheja ngalooo
 
Chamviga et al,

Maendeleo ya Bumbuli kwetu siyo issue, suala kubwa hapa ni suala la ukoo wa panya. Tupo hapa tulipo kwa sababu za kipuuzi za kulindana kwa koo za watawala. Sidhani kama itakuwa 2015, and you should join this effort kuakikisha ilo halitokei.
 
mtunzi wa riwaya anapaswa kua makini sana ili wasomaji wake wasijue kua ni hadithi!
 
Kwi kwi kwi kwi kwi kimtu chenyewe kilivyo kama kimebemendwa kisiasa sijui kiburi cha uprsidaaa kamapa nani?
 
kwa kuwa alikua mwandishi wa hotuba za rais, sasa naye anajiona anaweza.
 
Mchungaji nakulize na wwe. ulikula? ulikunywa? ulilazwa? je hiyo 50 ulichukua? naomba nijibu na mimi
 

Mimi nimemjibu huyu ajitae mchungaji kuhusu hizi propaganda zake. Mimi nimuumini wa mabadiliko lakini si kupitia vyama vya kilaghai na ubabaishaji. Hivi ni vyama hatari zaidi ya chama tawala. Vyama vinavyoshindwa kujiendesha na kusimamia taratibu na kanuni bila bias vitawezaje kuhimili kuliongoza taifa?. Akhsanta.
 
Na wewe uliotoa post hii ni mdini!tena ni mtu hatari sana kwa taifa hili, kwanini usingemuuliza palepale na akupe majibu kisha utume humu? ulilizika kugonganae glssssssss!
 
Huyu sio mtumishi wa bwana,, labda bwana mwingine na si huyu wa majeshi aliye hai,,, umekula pilau,, ukanywa na koka "haramu" na fweza ukabeba,, na kitanda chako cha telemka tukaze ukakisahau,, na choo cha dumbukiza pia ukakipa kisogo japo kwa siku moja,, leo mtumishi baada ya kumnanga palepale kikaoni unatuletea huku kama sio unafiki ni nini kwakweli,, ndo maana nchi haiedelei maana wanafiki mpaka watumishi wa Mungu (sio wote) tumechoka na uzandiki,, kwanza kuwaita nyie watumishi sio kosa,, maana watumishi ni wawakilishi wa makundi ya kijamii kama walivyo wengine!!! msigeuze JF kuwa ukumbi wa taarabu


Kama ulikuwa kwenye hicho kikao si ungemuuliza hayo maswali?kama sio unafiki ni nini..
 

hayo yote ulimuuliza kwenye kikao hicho?
 
hongera mchungaji kwa kulamba kaposho ka sh 50,000/=!lakini hakuna sababu zozote za kuwashawishi viongozi wa dini kuhubiri siasa tena siasa za kumwagiana tindikali.waacheni viongozi wa dini wahubiri neno la mungu na amani
 
Kama ulikuwa kwenye hicho kikao si ungemuuliza hayo maswali?kama sio unafiki ni nini..

Unawashwa wewe...hujui hata protocol za vikao..tukisema watu waulizane hukohuko magazeti,Jf, Fb, pamoja na wanasiasa, vyombo vyote hivyo vitakuwa na kazi gani? Wachungaji na mashehe nao wamalizane na maandiko matakatifu bila kuonana na waumini wao?Japo sijui jinsi yako lakini nakiri kuchukizwa na mtazamo wako wa kipuuzi..Rudi darasani maana huenda elimu yako ni sawa na ya yule naibu waziri wako wa elimu...
 
Wagombea CCM
1. Edward Lowassa-Ana pesa na watu.
2. Stephen Wassira- Ana watu na ushawishi.
3. January Makamba - Bado mchanga ndo anajitangaza.
4. Bernard Membe-Bado hajaoteshwa anautamani.
5. Emmanuel Nchimbi- Yuko njia panda kwasasa.
6. Fredrick Sumaye-Anajikongoja anautamani
7. William Ngeleja-Msindikizaji.
 
Wakati watu siku ya jana wameitumia kukaa na ndugu na jamaa, wenzetu kumbe mmepanda mabasi kwenda kunywa pombe za bure za mwanasiasa na kupokea posho. Ama kweli njaa kitu kibaya, hivi halafu mtu anapokwita si lazima ujiulize anataka kukwambia nini au wenzetu mlichosikia ni posho tu.

Umeenda, umekunywa na umekula bure, umelipiwa hoteli na ndugu zako umewakimbia kisa umeahidiwa posho were are your morals mtu wamungu, sasa ndio unajiuliza. If you ask me ni umbea tu.
 
Nomaa Sana kateketeza 20m per day!! Kodi zinatumika vibaya!

Siasa inalipa sana Tanzania. Iwapo viongozi wetu wangekuwa na juhudi za kuliendeleza Taifa kama walivyo na juhudi za kutafuta madaraka, nchi hii ingekuwa kisima cha maraha kwani ingekuwa ndiyo "Singapore ya Afrika."
 
Safari hii Ikulu haingiliwi kwa pesa,Watanzani tuweni makini na hao wanaotumia fedha.
Mleta mada anashambuliwa na vibaraka wanaoponea fedha dhalimu za kuwaingiza wenyenazo ikulu.
Hakika hawatashinda na wataishia kutapanya fedha zao na hawata ambulia chochote.Watanzania wameelimika na hawadanganyiki.Mwenye sifa pekee ndie atakaye iingia Ikulu kwa ridhaa ya Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…