Pole January Makamba

Kama ulikuwa kwenye hicho kikao si ungemuuliza hayo maswali?kama sio unafiki ni nini..

Tena unafiki wenyewe ni wa ushuzi wa mavi hata uutoe polepole utanuka anaaacha kumuuliza mwenyewe analeta ushambenga humu
 
halafu wapiga kura tungejuaje kama kuna mtu anataka kununua kutuongoza?

Ununuliwe kwani wewe nyanya kama kununuliwa yeye ndo dalali kwa nini alipokea pesa ya kujikimu asingeikataa ni mshambenga
 
Makamba nae anataka tutuongoza watanzania? sasa nadhani taasisi ya raisi ni kama mchezo vile! .... makamba kwa mtazamo wangu, muda wako wa kufikilia uraisi bado sana, huna hata wizara uliyoongoza leo unataka nchi? nadhani bado ndani ya CCM wako watu wengi wenye sifa, ungana nao
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa

N kwel mkuu huyu jamaa n mnafk... posho kachuka af bado ana disi... af n kiongoz wa dhehebu.
 

Kumbe CHAMVIGA ni wa bumbuli ha ha ha naona povu lina kutoka kumtetea mghosi wa kaya......komaaa hivyo hivyo 2015 makamba akiwa rais utapata u DC......Ila nakubaliana na wewe kitu kimoja tu kwa jinsi januari anavyo ipigania bumbuli tofauti sana na shelukindo siku atleast ukiwa bumbuli utajihisi uko duniani maendeleo yana anza kuonekana kwa effort za makamba junior...hayo mengine ya kuhonga wachungaji mtajuana wenyewe...
 
Last edited by a moderator:
sina shaka kuwa alichokisema ndugu alinda ni uongo tena uongo mtupu! Kanda ya ziwa pekee haina maaskofu 152 vinginevyo kama anadhani kila kiongozi wa dini ya kikristo ni askofu!

Ujinga ni mzigo unaoelemea sana! amesema walikuwepo na wainjilisti.

wewe unajua kusoma lakini hujui kuelewa.
 
January makamba ni mtu anayeabudu sana rushwa.
ana umri mdogo kuliko pesa alizonazo. kwa umri wake akithibitisha kazi/biashara halali iliyompatia haya mapesa itakuwa ajabu la dunia.

Tuvunje utamaduni unaoanza kukomaa wa wananchi watoa rushwa kupitishwa kugombea nyadhifa za uongozi.

Rais Kikwete anawajibika kupeleleza, akibaini ukweli wa hili jambo ampoke unaibu waziri aliomzawadia huyu muumini wa rushwa. Ubakie upofu wa wana bumbuli kwenye ubunge wao.

NAMPIGA MUHURI JANUARY MAKAMBA KWENYE PAJI LA USO WAKE UKISOMEKA "HUYU NDIYE KIONGOZI MKUU WA RUSHWA KWA KUPOKEA NA KUTOA"
 
Rais wa kweli tutampata lakini;it will take us looong but we are heading there because we are going through this.
 
wanaomtete huyo kilaza makamba ni uvccm walihongwa simu kumtetea kwenye mitandao ya kijamii.....makamba hana sifa ya kuwa rais,what did he run to show up the society that he can????hapo alipo haja hasle kasaidiwa na baba yake mzee makamba kwa kutumia ukatibu mkuu kujinufaisha na familia yake,you cant compare him na vijana kama mnyika,lema,filikunjombe etc
 
Tena unafiki wenyewe ni wa ushuzi wa mavi hata uutoe polepole utanuka anaaacha kumuuliza mwenyewe analeta ushambenga humu

Hebu nikuulize wewe zuzu....Bila ya yeye kumwaga hapa ukweli wote mimi ningejuaje kama January Makamba anataka kununua viongozi wa dini?
 

Hizi ni nyakati za Mwisho na ww ni mtumishi wa mungu...umekula takrima na unafanya majungu
 
Mwanza. Katika kile kinachoonekana kama kujipigia debe katika kinyang'anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewaambia viongozi wa dini Kanda ya Ziwa kwamba vijana wanapofika kuomba ridhaa yao, muwaangalie, msiwabeze.

Huku akikataa kuweka bayana nia yake ya kuwania urais kwa maelezo kwamba muda wa kufanya hivyo haujawadia, Makamba aliwaambia viongozi hao wa dini kwamba wagombea hao wanapopita wawasomee sifa za uongozi katika Biblia na kusema kumekuwapo mjadala wa sifa za uongozi kuhusu kijana na kusema amekuwa akitoa mwito kwa vijana wasiokuwa na makandokando kushiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.

Akizungumza juzi usiku mjini hapa katika chakula cha pamoja na maaskofu na wachungaji kutoka Umoja wa Makanisa ya Kikristo wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema: "Huu ni wakati wa kila mmoja kutafakari hatima ya nchi yetu. Ndugu zangu… nadhani tuzungumze machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu sote ni Watanzania na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu."

Alisema vijana wengi wamekuwa waoga kwa madai kwamba hawana fedha, uzoefu lakini akasema maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo.

"Yeremia alipopewa unabii alilalamika mimi mdogo mimi siwezi, lakini Mungu alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) …. Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa," alisema na kuongeza:

"Bwana alimwambia usiseme, mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe."

Alisema Tanzania inapita katika kipindi kigumu, hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuongoza maombi yatakayoiwezesha kupata kiongozi mwenye sifa ya kuivusha katika kipindi hicho.

Makamba amesema nchi inakabiliwa na nyufa kama vile rushwa, udini, ukabila, Uzanzibari na Uzanzibara, huku akirejea hotuba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya Machi 1995, ambayo aliyataja mambo hayo kuwa nyufa zinazoweza kuliangamiza taifa.

Alisema Tanzania inahitaji uponyaji na ikibidi kuanza upya kwa maana ya aina ya uongozi unaohitajika hivi sasa na kwamba ili kutimiza lengo hilo, viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutafakari na kuielekeza nchi njia sahihi ya kufuata.

"Shughuli za siasa zimeingiliwa na matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingiliwa na matapeli. Sasa tunapotafuta uponywaji wa nchi yetu ninyi mna nafasi kubwa kwani uponyaji tunaouzungumzia ni wa maovu ya kiroho, uongo, ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mna nafasi kubwa sana," alisema.

Alisema viongozi wa kisiasa pia wanayo nafasi yao katika kuponya taifa lakini lazima wanapofanya kazi hiyo wawe wasafi.

Alisema askofu au mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi na hata katika uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ni vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
SOURCE: MWANANCHI

 
Naomba kuuliza hivi umri wa kugombea URAIS kwenye katiba mpya umependekezwa miaka mingapi?

Nijuavyo katiba ya sasa inasema mgombea URAIS wa JMT lazima awe na 42+ years. Huyu January Makamba hajafikisha huo umri.

Kama ameanza KUHONGA sasa hivi anajuaje kwenye katiba mpya UMRI utateremushwa? Au Katiba tayari CCM wanayo MFUKONI.

Mleta uzi tunakushukuru sana kwa kuleta habari hii, vinginevyo tusingeweza kufahamu madudu ya January Makamba.

Nafahamu amewapatia UVCCM laptop za kumtetea na kuitetea CCM mitandaoni, lakini always mafuta na maji havikai pamoja. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio na asikie
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa
Kuna tatizo??? Nadhan hakuna tatizo kuuliza maswali hayo humu ndani, Makamba na viongozi wengine wengi wamekuwa wakiulizwa humu na kutoa majibu humu humu. Sioni dhambi yoyote hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…