Pole Frank, mchumba hasomeshwi

Pole Frank, mchumba hasomeshwi

Inno laka

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,616
Reaction score
585
Habari wana Jf,

Mwaka 2009 nilisafiri na Rafiki yangu ambaye sasa hivi yupo Mara sec ni mwalimu kwa sasa tulikuwa tukielekea Nansio Ukerewe katika mihangaiko ya kimaisha, nikiwa kwenye meli nilikutana na kijana mmoja ambaye anaitwa Frank, katika kupiga piga story sehemu ambayo mimi nilikuwa naenda na yeye alikua anakwenda pale pale Chuo cha ualimu Murutunguru. Shida yetu kubwa ilikuwa ni kuonana na mkuu wa chuo ili tupate nafasi pale chuoni lakini tulipofika pale tuliambiwa mfumo wa kuingia vyuo vya ualimu kwa sasa umebadilishwa.

Tulirudi makwetu lakini niliendelea kuwasiliana na Frank. Baadae yeye alipata nafasi ya JKT na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi (JWTZ) na kupostiwa Songea, mwaka 2013 Frank alinipigia simu wakati huo mimi nikiwa Bukoba, kuwa amepata mchumba ambaye elimu yake ni form 4 anaona bora amtafutie chuo cha ualimu."Akaniambia sina mtu Wizarani atufanyie mishe, nikamwambia sina ila kuna chuo cha ualimu kipo Biharamuro ni kizuri tu ni cha Dini na wanachuo hufanya vizuri.

Kwa sababu yeye yupo mbali Songea mimi nilikuwa Bukoba kipindi kile nikaenda kuchukua form pale Nyamahanga ada yao ni kama mlionimoja au mbili hivi kwa mwaka. Frank akasema ataimudu kijana kajikunja kusomesha mwaka wa kwanza, mwaka wa pili huku akimuhudumia kila kitu, Frank akafunga safari kuwa aende kuhudhulia graduation ya mchumba wake ambayo ilikuwa tarehe 27 May mwaka huu.

Alipofika pale alikuta hali tofauti lakini yule mchumba wake alimwambia ukweli kuwa ana mmba ya miezi miwili ambayo kwa namna yoyote ile isingewezekana kumsakizia Frank. Mimba yenyewe kapewa na mwanachuo mwenzie nimemhurumia sana Frank anatia huruma, jamani hawa wasichana tunaowasomesha tuwe nao makini najua wanawake wapo wengi kama wa huyu mchumba wa Frank.

NDO MAANA WATU UCHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Nawasilisha
 
Kama anampenda wanaweza wakaendelea ,na wakamlea huyo mtoto
 
Safi sana alitakiwa kusomesha ndugu zake sio mtu aliye kutana nae ukubwani!

Mtu anasomesha akitegemea alipwe fadhila ya kupendwa huko ni kujidanganya...!
Ukiamua kumsomesha mtu ni kama kutoa sadaka tuu..!
 
Wanaume kizazi hiki sijui nani katuroga, sijui tumekula maharage ya wapi.

Huyo binti anastahili pongezi za hali ya juu sana. Nadhani ni wakati muafaka wa kumpa pongezi huyo binti.

Safi sana.
 
Kusomesha mtoto wa mwanaume mwenzio ni upuuzi tyu.....ila kila kitu kina tokea ili tujifunze kupitia tatizo....sku jua ata na hawa JWTZ huwa nao wana oshewa...!!
 
Dah pole Frank. Hapo kachepuka halafu kanogewa hata zana kasahau. Ni changamoto jikaze tu boss wangu, japo inauma. Kama unampenda na ye bado anakupenda pima weka ndani. But hakuna mwanamke utamkuta bikira katika ulimwengu huu. Ni nadra sana. Take it easy mani!
 
Back
Top Bottom