Pofesa Mussa Assad, adui wa wahalifu na wajinga

Oct 5, 2015
88
476
PROF MUSSA ASSAD, "WHISTLEBLOWER", ADUI WA WAJINGA NA WAHALIFU.

“…Inafahamika namna kampuni ya BAE system inavyofuatilia mahasimu wake, hasa katika biashara za silaha. Na hofu aliyokuwa nayo Norman Lamb inafanana na hofu aliyokuwa nayo Edward Hosea, aliyekuwa mkuirugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wa Tanzania. Mwaka 2007 Hosea aliwaambia wapelelezi kutoka Marekani kwamba; ‘maisha yangu yapo hatarini na kuongeza kuwa wanasiasa wa Tanzania hawagusiki katika sakata la mradi mchafu wa rada’. Hosea alikata tamaa ya kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika wa mradi wa rada lakini alikuwa na uhakika kwamba, wakuu wa vyombo vya ulinzi nawo walihusika katika kashfa hiyo. Hosea aliongeza kuwa amepokea vitisho kupitia ujumbe wa simu na barua, akitaarifiwa karibu kila siku, kuwa anapambana na watu matajiri na wenye nguvu. Hosea alieleza kuhusu mikutano nyeti ya serikali inavyosheheni ubabe na vitisho; “Unapoingia katika mikutano yao, wanataka ujione kuwa mdogo na wao uwaone kama miungu. Wanataka ufahamu kuwa wao ndio wamekuweka hapo. Usipokubaliana nawo, kuna hatari”.
Hosea alitanabaisha kuwa kama vitisho vitaendela juu yake, atahama nchi…(Kitabu: Istilahi za Uhalifu na Usalama – Dr. Christopher Cyrilo)

Ya CAG-Profesa Assad na bunge.

Baada ya Bunge kupitisha azimio la kukataa kufanya kazi naye, CAG Mussa Assad anasema, ‘wasiwasi wangu ni kwamba huenda likawa tatizo kubwa zaidi kuliko linavyoonekana sasa hivi… kwa sababu ‘technically’ (kiufundi) kunaweza kuwa na ‘constitutional crisis’ (mgogoro wa kikatiba)…kwamba ripoti zimeshawsilishwa kwa Rais, na mimi siwasilishi ripoti bungeni…Rais atawasilisha ripoti bungeni ndani ya siku sita zijazo na kama bunge litakataa kuzipokea…hilo ni tatizo kubwa zaidi…ni ‘Contempt’ (dharau) hiyo… kwa hiyo huo ndio wasiwasi wangu…na zikishawasilishwa bungeni zinakuwa ‘public documents’ (nyaraka za umma/watu wote), mimi ninapata fursa ya kuzungumza…na hilo pia linaweza kuwa tatizo. Kwa hiyo tafsiri ya kwamba hatutafanya kazi na CAG ni tafsiri panasana inatakiwa tuijue vizuri. Sasa kama nilivyokwambia mwanzo mimi sijapata hizi habari kwa uhakika, nitazitafuta leo nitaongea na watu wangu tutajua halafu tutafanya tathmini kitu gani tunaweza kufanaya labda. Alipoulizwa endapo anaweza kuchukua maamuzi yoyote magumu..alijibu; ‘Mimi sina maamuzi yoyote ya kuchukua bhana, mimi nnachokifanya mara nyingi hapa ni kufanya ‘dua’ tu basi. Kwamba watu waongoze vizuri wafanye maamuzi ambayo yana faida kwa nchi hii basi..’

Ukisoma haya ya kwanza hapo juu utajua kwa nini Yericko Nyerere anadhani kuwa Profesa Mussa Assad anahitaji ulinzi pengine kuliko wakati wowote sasa. Tanzania si sehemu salama kwa wazalendo wa vitendo, wasioogopa kusema ukweli hata kama ukweli huo hauwapendezi wakuu wa nchi na wapambe wao.

Kauli za Prof Assad katika haya ya pili, pamoja na matendo yake ya nyuma yanamfanya ajianike zaidi katika taswira kuu mbili, taswira moja ni ‘Whistle blower’ au mfichua maovu – na taswira nyingine ni ya ucha mungu. Mchanganyiko huu wa kufichua maovu na ucha mungu unamfanya Professa Assad kuwa mtu anayeogopwa na wahalifu, na ikiwa wahalifu hao wana nguvu ya kuamuru majeshi na watunga sera basi Professa Assad anakuwa kwenye mtego, sawa na mtego aliokumbana nao mkurugenzi wa zamani wa TAKUKURU, Edward Hossea wakati wa sakata la manunuzi ya kifisadi ya rada.

Taswira ya ‘whistleblower’ inamfanya Prof Assad kuwa zaidi ya CAG, na kuvuka mipaka ya uraia wa kawaida hadi kuwa shujaa wa nchi. Zaidi ya ma-CAG waliomtangulia, Profess Assad hamalizi kazi kwa kukagua mahesabu na kuandika ripoti, bali anakwenda mbali zaidi kwa kuwasema hadharani watu wadhaifu wasiotekeleza majukumu yao ipasavyo, kazi ya Whistleblowers. Wajinga huwaita watu wenye haiba ya Professa Assad kwa jina la ‘wanoko’..lakini mbele za Mungu, watu hawa ndio hasa wenye faida kubwa kwa wengine, watu hawa ndio wapambanaji haswa katika vita dhidi ya ufisadi, tupilia mbali wapiga kelele kwenye majukwaa ya kisiasa.

Maamuzi ya Bunge na azimio la kukataa kufanya kazi na CAG.

Inajulikana kuwa Bunge letu ni dhaifu, na inajulikana kuwa spika wa bunge ni mtumishi wa CCM zaidi kuliko alivyo mtumishi wa umma. Na kwa hiyo u-spika,ubunge na hata maisha yake yapo mikononi ya wamiliki wa CCM, tutarajie nini?. Hali hiyo ya spika ndiyo hali ya wabunge wengi wa bunge letu, ndio maana mambo ya CCM hukubaliwa na wanaCCM wote na ya wapinzani hukubaliwa na wapinzani wote, hakuna uhuru wa kufikiri..fikra zote zipo chini ya wakuu wa vyanma vyao na wengine hufuata. Haitatokea siku moja, wabunge wa CCM waamue kinyume na matakwa ya Mwenyekiti wao, ikiwa bado wanahitaji kuwa wabunge, na spika akiwemo. Hata maamuzi ya kupitisha azimio la kukataa kufanya kazi na CAG yametolewa kwa kufuata mfumo huo wa kimahusiano kati ya wabunge wa CCM na viongozi wao ambao ni wakuu wa nchi.

Bunge linapokataa kufanya kazi na CAG, maana yake litakataa kupokea taarifa zake ambazo Rais ataziwasilisha ndani ya siku sita zijazo. Au? Pengine maamuzi ya kukataa kufanya kazi na CAG yamekuwa ya kukurupuka, au labda ripoti ya mwaka huu ina ‘madudu’ mengi kuliko ya mwaka jana kwa hiyo mwenyekiti wa chama akaagiza ‘bunge lake’ lifanye hiki wanachokifanya sasa. Na kama kweli bunge litakataa kupokea hiyo ripoti ya CAG, Rais atafanya nini? Bila shaka atafurahi kwasababu mijadala kama ya Trilioni 1.5 haitakuwepo, matumizi ya fedha za umma bila kupitishwa na Bunge hayatahojiwa, manunuzi yasiofuata sheria hayatajadiliwa, serikali itakuwa na bahati kubwa. Huu ni usaliti mkubwa kwa watanzania.

Mwisho kabisa, watanzania wanapaswa kuomba dua pamoja na Prof. Assad ili asinaswe na mtego uliotaka kumnasa Edward Hossea.
Nawasilisha.
FB_IMG_1554275005922.jpg
 
View attachment 1062871
Mwalimu wangu Prof.Mussa Juma Assad nimeamini kuwa kweli wewe ni "Guru" katika fani yako!
Nakumbuka zama zile ukitufundisha AC 100 pale theater UDSM huku ukitumia Projector yako!
Sikuwahi kusoma Accounting kabla ya kujiunga UDSM ,wewe ndo ulianza kunifundisha maana ya Debit na Credit!
Pia nakumbuka kauli yako kama sikosei,ulipenda kutuambia kuwa ktk maisha yako huitaji mali nyingi! Ulisema mwisho wa yote utahitaji "Ubao wa mita 3" na " Shuka jeupe LA mita 3"! Vingine vyote havina umuhimu sana kwako kwani vitabaki na hutakwenda navyo!
Nilipoona kipindi kile Bunge la JMT linakudhalilisha kwa ukaguzi mithili ya kibaka niliumia sana lakini nilimshukuru Mungu kwani akina Ndugai hawakujua na mpaka sasa hawajui wana deal na mtu wa aina gani!
Wanafunzi wako tunajivunia wewe kuwa Mwalimu wetu na umetupa mtihani mgumu sana katika maisha yetu.Mungu akutangulie ktk shughuli zako!
 
Hongera kwa uandishi mzuri na bandiko zuri. Ulichokiongea ni dhahiri pasipo shaka kwamba kuna kitu kinasukwa kuanzia ikulu au makao makuu ya ccm, huko aliko mwenyekiti wa ccm taifa. Tangu Mwenyekiti huyo wa ccm taifa alipoingia ikulu kama rais kume kuwa na mambo meeengi ambayo watu wanayasahau sasa. Alianza na TUMBUA TUMBUA akaitwa Doctor wa Majipu, alipiga koote akianzia kw aOmbeni sefue aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, akamuweka mtu wake, na alichokuwa akikifanya ni kuondoa kila aliyewekwa na watangulizi wake ili AWEKE watu wake. Alipita kila aalikotaka kupita akifanya mabadiriko hayo, BOT,PPF,NSSF,TRA na akwingineko list ni ndefu sana. Sasa Alipofika kwa CAG mtihani ulianzia hapo, Maana anamteua rais lakini huyu kasha tafutwa sanaa afukuzwe, wamemtafuta kwa ubadhilifu wakamkosa, wamemtafuta kwenye report zake wakamkosa, hata lile swala la Trilioni 1.5 alipoulizwa swali la papo kwa papo ulikuwa mtego walimkosa.
Wakaanza na mahojiano yake ya huko New York, timbwili likawa ataitwa na kamati ya maadili ya bunge au la? Akaitwa na Bila hiyana CAG akaitikia wito, na akamalizana nalo, walitegemea hatokwenda wamfukuze lakini jamaa alikwenda na akarudi salama. sasa hili, la Bunge kutokufanya kazi na CAG walilipika ili kupeleleka message kwa rais kwamba huyo jamaa sisi hatumtaki anatudhalilisha sisi na CCM, kinachosubiliwa ni maamuzi ya kichama ya mwenyekiti wa CCM taifa ,Je atakubali wana ccm wenzake WAUMBUKE au atawalinda, na kuwalinda ni KUMFUKUZA huyu CAG kwa kisingizio kwamba BUNGE limekataa report yake na hawezi kuwa na CAG asiyekubalika na BUNGE.
Tusubiri kamati kuu ya CCM itamshauri nini mwenyekiti wao na mwenyekiti wao atafanya nini kuwalinda wenzake kule Dodoma.
 
Back
Top Bottom