PM Pinda atavunja rekodi ya CHADEMA mkoani Kagera?

Mimi nadhani ni wajibu wake kama kiongozi wa kiserikali kutembelea wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kuwahamashisha wananchi katika kujiletea maendeleo. Naamini pia angefanya hivyo hata kama CHADEMA wasingekuwa wamezunguka huko.

Umewapa jibu sahihi. Anatekeleza wajibu wake.
 
CAHDEMA WALIENDA KIVYAO NA PINDA ANAKWENDA KIVYAKE, NAFIKIRI SIO BUSARA KUINGIZA USHABIKI USIO NA MAANA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU. KILA MMOJA WETU ANATAKIWA KUBUNI MIKAKATI YA KULIONDOA TAIFA HILI HAPA LILIPO. WAKATI NAWAPONGEZA SANA MAKAMANDA WA CDM WALIOKUWA KATIKA ZIARA YA KANDA YA ZIWA SI WENGINE TUNAFANYA NINI ILI KUHAKIKSHA TANZANIA INAPATA MABADILIKO YALIYO POSITIVE?

NDIO MAANA NAUONA MJADALA HUU KAMA KITU KISICHO NA TIJA KWA CDM, KWETU SISI NA TAIFA, KWA SABABU WOTE TUNAOLETA USHABIKI KUHUS SUALA HILI KILA MMOJA ANALO ENEO LAKE LA MAKAZI AMBALO AMA CDM ILIPATA USHINDI AU KUKOSA USHINDI. JAMBO LA MUHIMU AMBALO NINGESHAURI TUFANYE PALE TULIPOPATA USHINDI NI KWA VIPI TUTALETA MABADILIKO ILI HATIMAYE WANANCHI WASHAWISHIKE KUWA CDM NI BORA NA KUIPIGIA KURA TENA 2014 KATIKA UCHAGUZI WA SERKALI ZA MITAA NA 2015 UCHAGUZI MKUU.

PALE CDM ILIPOSHINDWA KUPATA MBUNGE AU DIWANI IFANYIKE TATHMINI NINI KILIPELEKEA HALI HIYO NA NINI KIFANYIKE KUWASHAWISHI WAPIGA KURA WA ENEO HILO KUICHAGUA CDM. TUKIJIKITA KATIKA SHUGHULI HIZI NINAAMINI KUWA HATUTAKUWA NA MUDA WA HOJA KAMA PM Pinda atavunja rekodi ya CHADEMA mkoani Kagera? KAMA AMBAVYO WENZETU WALIACHA CDM IFANYE MIKUTANO YAKE, NA SISI TUNATAKIWA KUONYESHA UUNGWANA HUO HUO WA KUWAACHA WAFANYE MIKUTANO YAO BILA YA KUANZA KUWALETEA MANENO MANENO YANAYOWEZA KUPELEKEA MALUMBANO NA MWISHO KUVUNNJIKA KWA AMANI.
 
maskini PM wetu aliyekuwa muadilifu..................... sasa anatumika kama mbuzi wa kafara. duuuuh,inauma sana!
 
hata wakiita bongo fleva yote hapo bk hawezi kupata umati wa cdm!

namshauri afanye ziara ya kimya kimya
 
Wanaouliza maandamano yatatusaidia nini nafikiri wamepata jibu. Viongozi wa serikali wanaanza kuondoka maofisini na kwenda kwa wananchi kujieleza.

Safari hii, wataogopa kuzungumza uongo.

Kitakachofuata, wataanza kufanya kazi inayotakiwa manake wasipofanya hivyo watazomewa kwa sababu wananchi wameshahamasishwa, na wanajua haki yao.

CHADEMA, fanya hima zunguka nchi zima ili watakapopita wao wakutane na moto uliowasha.
 
Masikini Pinda..yani wenzake wanavuruga halafu yeye wanamtuma akatulize mambo..Pinda utaendelea kutumika hadi lini?

c shock absorber ya serikali mwache atumike tu sema anakopita kuna mashimo mawe kokoto ashaanza kuchoka watu wanaelewa
 
Si ilitangazwa huyu jamaa alikuwa na ratiba ya kutembelea Bukoba leo?

Kuna mtu anajua kinachoendelea? Au mikutano yake inafanyikia vyumbani??
 
Cdm kusema sukari imepanda ni uhaini,wahitimu wa vyuo kukosa ajira ni uhaini? Kupinga Dowans ni uhaini? Mchele,unga,n.k wasiseme? Wananchi tumechoka,na sasa tunaanza kumwona Nduli,adui yetu hadharani. Siwezi nkaendelea kulia njaa nkaendelea kusikia Pinda ukiwakataza wanacdm watusaidie. Umeenda bukoba,ukawapa elfu5 tano ili wahudhurie,maskini wamefika na wanaambiwa aidha maneno ya dharau au maneno ya ujuha kwa wananchi. Tendwa unasema unataka kuifuta cdm,na umetuhakikishia kuwa una mawasiliano na mkurugenzi wa mashtaka na anaandaa mashtaka,kwa lipi? Serikali hii ni ya majuha wenye mchanganyiko wa madkteta! Kwa kauli zenu Tendwa na Pinda ,mmetudharau watanzania,tutapaswa tuwachukulie hatua!!!
 
wakiwakamata viongozi wa chadema nchi yote italipuka maandamano ambayo hawajawahi kukutana nayo. Subirini mtaona kama wanafikiri kubeep watanzania na wajaribu waone!
 
nasikia leo pinda alikuwa na watu kidogo sana na hawakutaka kusikiliza propaganda! C rahisi kufikia rekodi ya umati uliokuwepo juzi uwanja huo huo wa mashujaa
 
Issue siyo kuvunja record ya chadema ni je atajibu hoja? Chadema wanakusanya watu kwa kuwa wanahamasha kwa kuwaandaa watu kuwa wakaidi na kidharau serikali.wanakusanya watu kwa kutukana viongozi na kuahidi kuipindua serikali,pinda hawezi kufanya upuuzi huo zaidi ya kujibu tuhuma.
 
Back
Top Bottom