PM Pinda atavunja rekodi ya CHADEMA mkoani Kagera? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PM Pinda atavunja rekodi ya CHADEMA mkoani Kagera?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Manyanza, Mar 4, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  KATIKA kile kinachoonekana kama mpango wa Serikali kukabiliana na nguvu za maandamano na mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku nane katika Mkoa wa Kagera ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo.

  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Waziri Mkuu ataanzia ziara yake katika Manispaa ya Bukoba kisha atakwenda Muleba, Chato, Biharamulo, Ngara, Karagwe, Missenyi na kumalizia Bukoba Vijijini.

  Katika ziara yake ya Kanda ya Ziwa, Chadema kilitembelea na kufanya mikutano katika Wilaya za Biharamulo, Misenyi, Muleba na Chato ambako viongozi wake walifanya mikutano na maandamano huku wakitaka Kampuni ya kufua umeme ya Dowans isilipwe, bei ya umeme ishuke na kikitaka utawala wa CCM uwajibike.


  Baadhi ya shughuli kubwa ambazo Waziri Mkuu amepangiwa kufanya wakati wa ziara hiyo ni pamoja na kuzindua Barabara ya Zamzam na mkutano wa hadhara kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba katika Uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform).


  Akiwa wilayani Muleba, Waziri Mkuu Pinda atakagua shamba la mkulima bora wa kahawa katika Kijiji cha Ilogero kabla ya kwenda Buganguzi ambako atakagua mashamba ya migomba yaliyoshambuliwa na magonjwa ambayo mpaka sasa hayajajulikana kisayansi.


  Pia ataweka jiwe la msingi katika mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Buyaga na kuhutubia wananchi katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Kasharunga.


  Akiwa wilayani Chato, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua Saccos ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Shule ya Msingi Chato.


  Akiwa Biharamulo, Waziri Mkuu atakagua mnada wa ng'ombe wa Lusahunga, kukagua ujenzi wa wodi katika hospitali hiyo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya St Clara huko Rukaragata na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Michezo wa CCM.


  Akiwa Biharamulo, Jumanne ijayo Waziri Mkuu atakwenda Ngara kufungua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Ngara Farmers kabla ya kwenda kwenye Mgodi wa Nickel wa Kabanga. Pia atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara huko Muurusagamba.


  Akiwa Karagwe, Jumatano ijayo atakagua bwawa la samaki huko Kishoju na kusalimiana na wananchi kisha atakwenda Kayanga kuzindua jengo la masjala ya ardhi. Mchana ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ualimu Katera kabla ya kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Isingiro.


  Akiwa Missenyi, Alhamisi ijayo, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo. Baadaye ataelekea Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuona mitambo ya kisasa ya umwagiliaji mashamba ya miwa. Pia atakagua shughuli za kiwanda hicho na kisha kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi.


  Akiwa Bukoba Vijijini, Ijumaa, Waziri Mkuu atatembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku, maabara na baadhi ya vijishamba vya utafiti wa kilimo. Pia atakwenda Hospitali ya Izimbya kuzindua majengo ya OPD, watoto, maabara, chumba cha upasuaji na jengo la ushauri na upimaji VVU (CTC).


  Jumamosi ijayo, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo.


  Source: Mwananchi
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  labda afanye kuwakusanya tokea mikoa mingine kwa mabasi ya wao ccm kulipia kama ilivyokawaida yao.

  Au inawezekana watu wengi wakaenda kumshangaa huyu kiumbe PINDA.
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Na kuchezea picha kwa kutumia photoshop kama walivyokuwa wanaunganisha picha wakati wa kampeni.
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Masikini Pinda..yani wenzake wanavuruga halafu yeye wanamtuma akatulize mambo..Pinda utaendelea kutumika hadi lini?
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ngoja tuone ila wasiwasi wangu ni kuzomewa anaweza kuwakwepa wananchi akaishia kuongea na viongozi tu wa halmashauri
   
 6. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pinda anendelea kujishushia hadhi. Naamini hana jipya la kueleza zaidi ya kujiondolea heshima katika jamii. Ngoja tuone...
   
 7. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watakodisha malori kuwabeba watu na kuwapeleka kwenye mkutano ili wawe wengi.
   
 8. S

  SARAWAT Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muache akauze sura bk, hahahahahahaha!!!!!!!!!!!!
   
 9. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani ni wajibu wake kama kiongozi wa kiserikali kutembelea wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kuwahamashisha wananchi katika kujiletea maendeleo. Naamini pia angefanya hivyo hata kama CHADEMA wasingekuwa wamezunguka huko.
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  WM Pinda anafanya ziara ya kiserikali. Hizo ziara za kuijibu CHADEMA atazifanya Msekwa na Makamba
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  CCM wamempeleka Pinda kwani wanaamini bado anapendeka. Ila wamekosea. Pinda is on a downward spiral.

  Angekwenda JK mwenyewe, lakini nadhani anaogopa uma. Wanaweza kumzomea au hata kumtoa mkuku jukwaani. Si alishapigwa mawe kule Mbeya? Na wakati ule alikuwa hajashuka chati vibaya kama hivi. Masikini CCM! Hawana hili wala lile!
   
 12. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri kama yale mabango kwenye maandamano ya Chadema wamkaribishe nayo na kila anapoenda wampelekee ayasome.
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HAta hivyo haikuwasaidia!!
   
 14. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kama alivyofanya UDOM
   
 15. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu jamaaa wanamuua kisiasa wenzake lakini halijastulia tu,sio tena mtoto wa mkulima ila limekuwa beki tatu la mafisadi
  "Nakuchukia Pinda kwakuwa ni mnafiki na Muongo"
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi ni Ziara za kawaida kwa viongozi kutembelea mikoa mbalimbali.

  Suala langu hapa, safari hii ilipangwa mara baada ya Slaa kupita au ilikuwa katika ratiba zake za kazi?
   
 17. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eeeh watu watasombwa haoooo macho yetu!
   
 18. m

  mtimbwafs Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muacheni WM Pinda aende kufanya kazi zake na kipimo tutakiona tu wakati wa Ziara yenyewe ndugu zangu WATANZANIA TUNACHOTAKA NI UMEME, ELIMU BORA, MAISHA MAZURI na MAENDELEO basi na hiki ndicho ambacho CDM wanataka.
   
 19. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  its too late,,,,,too late,,,,very late,,,,,extremely late,,,,,WAY TOO LATE!!!
   
 20. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wote walewale tu!
   
Loading...