Mayor ni diwani = mwakilishi wa wananchi kwenye kata yake kwenye halimashauri ya wilaya/ mji wao) ambaye madiwani wengine wa wilaya/ mji huo wamemchagua kuwa mwenyekiti wa vikao vyao.
Kazi ya udiwani au umeya ni part time, yaani ya kuhudhuria vikao vya baraza (= bunge) la madiwani kusimamia na kuishauri halimashauri yao kwa niaba ya wananchi wa kata zao. Baada ya vikao hawana kazi nyingine kwenye kata zao. Na wala hawalipwi mshahara wa serikali, bali hulipwa tu sitting allowance ya siku za vikao ambazo ni siku moja au mbili tu kwa mwezi. Wana kazi zao za kuendeshea maisha.
Ni vyeo vya heshima tu kama wawakilishi wa wanamchi kwenye serikali zao za mitaa. Si vyeo vya kiutendaji.Kwa kiwango fulani vyeo hivi unaweza kuvilinganisha na wabunge wa majimbo ambao mwenyekiti wao anaitwa Spika. Tofauti ni kwamba baada ya enzi za mwalimu wabunge walianza kulipwa mshahara wa serikali pamoja in addition to their sitting allowances.
Wabunge au madiwani wako muhimili wa wakilishi wa wananchi. Rais akisaidiwa na maRC na maDC wako muhimili wa dola (executive) au kwa jina jingine serikali. Bendera ya dola/ serikali ya Tanzania ndiyo hiyo bendera ya taifa, hivyo mwenye stahili wa kuipeperusha ni huyo mkuu wa dola katika eneo lake (DC, RC, Waziri, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais). Meya hupeperusha bendera ya Halmashauri yake ya serikali za mtaa ambayo hutofautiana kila halmashauri ili kujitofautisha na mameya wa halmashauri zingine. Kwa kuwa spika wa bunge ni mmoja tu kitaifa basi yeye hupeperusha bendera ya taifa. Rais pia ana bendera yake ya urais in addition to the national flag. Nadhani tupo pamoja, mkuu.