Raelish
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 489
- 162
Ajira hamna,tukio lililofanyika taifa limenisikitisha sana. Mimi ni mmoja kati ya vijana ambao hawana ajira, nimeshaomba mpaka ajira ya kuuza biashara za mtu nikakosa. Nilichoamua ni kurudi kijijin ambako ndio kwetu,mfukoni nilikuwa na tsh.130,000, of coz nilishindana na vingi,aibu + kujisikia vibaya lakin nikakaza moyo.. nilipofika kijijin nikaomba eneo nikapata bure,nikajenga banda la kuku,nikanunua kuku 20 tetea 17 jogoo 3,nikapata chanjo ya magonjwa ya kuku nikawapa, nikawaacha chini ya uangalizi wa anko wangu kule.. kuku wakaanza kutaga na nikapata vifaranga kama 169 hivi, bado ajira sikufanikisha nikarudi kijijn kuwahudumia kuku wangu hatimaye kuku wakawa wakubwa, kwa mara moja nikauza kuku 100 nikapata kama tsh.1.3 milion hivi, na mtaji wa kuku kama 70 hv baada ya wengine kufa.. Mpaka sasa kuku wanataga tena na nategemea kupata vifaranga zaid ya 200,. nimefungua duka la nafaka, na nataka nifungue salun ya kiume huku kuku wanaendelea.. JARIBU NAWEWE, 'fikra za kuajiriwa tufute,tutapata presha bure'