PISHI: Wali mixer by tambi

PISHI: Wali mixer by tambi

Hellow mchana mwema

Leo tupike hiki chakula asili yake Madam B atasema

Kwanza chukua tambi zako ulizo kataka ndogo ndogo kisha weka kwenye sufuria ya mafuta yalio chemka kisha anza kuzikaanga mpaka zibadirike rangi na kuwa kahawia zisiungue
View attachment 3287755
Baada ya hapo chukua mchele wako ulio uosha kisha tia kwenye sufuria anza kuukaanga na tambi
View attachment 3287762
Baada ya hapo weka maji yako kama una tui la nazi tumia mimi nazi nakuja kuweka baadae baada ya maji kupungua kidogo
View attachment 3287764Kisha funika na upunguze moto moto weka mdogo kabisa na ukaee kwa muda mrefu
Baada ya hapo mm nikaweka nazi kisha nikageuza nikaacha nikaanza kupika mboga
View attachment 3287767
Mboga kwa mimi natumia kuku rosti na wewe unaweza tumia samaki au nyama mboga yoyote ulio nayo
Nilianza kukaanga kuku kwanza
View attachment 3287770
Kisha nikaweka vitunguu pamoja na hoho na karoti
View attachment 3287771
Kisha nikaweka nyanya nilio saga
View attachment 3287774
Baada ya nyanya kuiva nikaweka nazi
View attachment 3287776
Baada ya hapo nipo nakula karibuni sana wote
View attachment 3287778
Nipo tayari kwa kusimangwa 😂
mkuu wali unapika kwenye jiko la gesi...utakua mzoefu sana manake wadada wenyewe wanashindwa kupikia wali kwenye jiko la gesi wanapendelea jiko la mkaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom