PISHI: Dagaa Nyasa na mnafu unaweza kula na ugali

PISHI: Dagaa Nyasa na mnafu unaweza kula na ugali

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Hellow

Leo nikapata dagaa nyasa wangoni nipo tayari kunikosoa kama nimepika sivyo

Kwanza mimi nikawatoa vichwa dagaa
1742914735973.jpeg

Kisha nika waweka jikoni kuwachemsha kwanza lazima uwachemshe vinginevyo huwezi kula
1742914791249.jpeg

Baada ya kuchemsha kwa mda nikawaipua na kuwa weka kwenye chombo
1742914837474.jpeg

Baada ya hapo nikaweka sufuria jikon nikaweka mafuta baada ya kupata moto nika weka dagaa kuwakaanga
1742914995817.jpeg
Baada ya kuona wapo vizuri nikaweka kitunguu sasa
1742915031649.jpeg
Baada ya hapo nikaweka karoti na hoho
1742915069759.jpeg
Nika mix bay yas 😂 ili viende sambamba nikaweka nyanya nilio isaga
1742915135807.jpeg

Nika mix tena ika iva uzuri nikaongeza maji kidogo ili nipate mchuzi
1742915180583.jpeg

Vikatokota nikaweka nazi sasa baada ya kuona mchuzi umekuwa vizuri
1742915227092.jpeg

Baada ya kutia nazi ikachemka vizuri nikaipua
1742915407611.jpeg




Tuje kwenye mnafu uku
Kwanza niliuchambua vizuri tu na nikaukatakata vizuri
1742915463401.jpeg

Baada ya hapo nikauosha nikaweka maji kwaajili ya kuuchemsha kwanza nika weka jikoni
1742915515881.jpeg

Baada ya kuchemka nikachuja maji kisha nikauweka tena jikoni ni kwasababu mchungu usipo fanya hivi hii mboga ukuli 😂
1742915577737.jpeg

Baada ya hapo nikaweka sufuri jikoni na mafuta kisha nikaweka karoti na kitunguu maji
1742915637271.jpeg

Nika mix by yas kisha nikaweka nyanya
1742915678892.jpeg

Baada ya nyanya kuiva nikaweka mnafu
1742915707458.jpeg

Nika mix vizuri kisha nikaweka nazi si lazima
1742915751038.jpeg

Nikaichanganya nazi vizuri nikahakikisha imekolea haswaa 😂
1742915838210.jpeg

Baada ya hapo nikawa nimemaliza. Imebaki kazi moja tu kusonga ugali na nitasonga saa moja na nusu njaa ikikolea

Song la wangoni
🎶 eti nyumba ya baba usilete hawala nyumba ya baba usilete hawala kujibanabana aheeeee ……………..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom