Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma, imetupilia mbali pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, na hivyo kufungua rasmi mlango wa kusikilizwa kwa ushahidi katika shauri la uchaguzi la Jimbo la Kigoma Mjini.
Uamuzi huo umetolewa leo, Desemba 16, 2025, na Mheshimiwa Jaji Projestus Khayoza katika Shauri la Uchaguzi Namba 28949 la Mwaka 2025, ambapo mahakama imewapa ushindi walalamikaji Johary K. Kabourou, Loum H. Mwitu, Pendo D. Kombolela na Luma H. Akilimali, wanaosimamiwa na Wakili John Seka.
Kupitia uamuzi huo, Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za walalamikaji kuwa shauri hilo ni halali, lina msingi wa kisheria na limekidhi matakwa ya Sheria ya Uchaguzi pamoja na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi, hivyo kuondoa kikwazo kilichokuwa kikizuia kesi hiyo kusikilizwa kwa misingi yake.
Hapo awali, walalamikiwa kupitia mawakili wao waliwasilisha pingamizi la awali wakiiomba mahakama itupilie mbali shauri hilo kabla ya kusikiliza ushahidi, wakidai kuwa kulikuwa na mapungufu katika Aya ya Uthibitisho wa hati za shauri, pamoja na hoja kwamba walalamikaji walipaswa kuomba msamaha wa dhamana ya gharama za kesi hata kama walikuwa na hati ya msamaha kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Aidha, walalamikiwa walidai walalamikaji hawakuwa na mamlaka ya kisheria kuomba baadhi ya nafuu ikiwemo upekuzi na uhesabuji upya wa kura.
Source: Jambo