Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,901
- 2,782
Kumbe sheria zetu zinaathiriwa na sheria za nchi nyingine? mi sikulijua hilo.
Kwa maelezo hayo. Je, sheria za Kenya ambazo NEC walizipitia ktk sakata hilo zinahusiana vipi kufikia uamuzi wao?
Hata mimi nisiye Mwanasheria naona wamebofoa, NEC iliwapasa waangalie sheria za Tanzania zinasemaje ktk hilo, kama walivyofanya Idara ya Uhamiaji.
Hili suala litaendelea hata baada ya uchaguzi ikiwa Siyoi atashinda, na NEC wataunganishwa kama walalamikiwa.
Nashauri hata CDM wakishinda, waangalie namna ya kuishitaki NEC Mahakamani, hili suala liko wazi kabisa, na Uhamiaji wawe mashahidi
unajua bwana sheria sio mambo ya propaganda lazima uwe na ushahidi wa juu ya unalolizungumza.nadhani sasa ni wakati wa kujikita ktk kampeni na kunadi sera ili mwisho wa siku wana arumeru waamue mchele ni upi na pumba ni zipi.
Ingekuwa vyema zaidi kama ungetuambia ni kigezo gani kilichotumika ktk kufikia maamuzi hayo, otherwise wewe ni great sinker.CDM pingamizi lenu ndiyo hivyo limetupwa sijui mtakuja na nini tena! Kote huko ni kutapatapa tu mambo ni magumu Arumeru.
NEC yamsafisha Sioi (Tanzania Daima)
Katika maelezo ya mrufani na vielelezo alivyowasilisha tume, hakuna popote ilipothibitishwa kuwa Sioi alipata uraia wa Kenya. Kwa kuwa mrufani ndiye aliyetoa madai kuwa mgombea alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa kwake Kenya, basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni, alisema.
Bashe alitemwa na CCM na sio tume jamani, tujaribu kuweka kumbukumbu vizuri
Mkuu unajaribu kusema nini hapa?Kuna uhusiano gani Kati ya mgombea wa arumeru na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi? What does the rule against bias say? Je alideclare interest zake Mara baada ya hii issue kuvuka mezani kwake?
Majibu ya masuali haya ndio Tutajua ni kwa nini tume ya uchaguzi imevaa madaraka ya mahakama na kuendelea hata kutengua uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Kulikuwa na concern kubwa wakati wa uteuzi wa mwenyekiti wa Tume watu tukapuuzia
Mkuu unajaribu kusema nini hapa?
Tume imetimiza wajibu wake kisheria, sasa kama haujafurahishwa na matokeo jenga hoja kwanini Sioi ni Mkenya na tume imeamua sio Mkenya
Sheria za urai zipo wazi kabisa, fafanua