Pingamizi la CHADEMA Arumeru latupwa nje na NEC

buckreef

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
309
40
NEC yamsafisha Sioi (Tanzania Daima)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemsafisha mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, kutokana na tuhuma za utata wa uraia wake zilizokuwa zimewasilishwa katika rufaa na mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari.

Uamuzi huo wa NEC uliotangazwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa tume, Julius Mallaba, akisema kuwa kutokana na sababu kadhaa zilizoonyeshwa na jopo la ‘wataalamu' wa tume waliokaa kupitia vifungu vya sheria za uhamiaji za Kenya na Tanzania, rufaa hiyo imeonekana haina msingi.

"Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo vilivyowasilishwa pamoja na rufaa ya mrufani na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Katiba ya zamani ya Kenya, Sheria ya Uraia ya Tanzania, Na. 6 ya mwaka 1995, Tume inakubaliana na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa kukataa pingamizi la mrufani kwa sababu zifuatazo.

"Katika maelezo ya mrufani na vielelezo alivyowasilisha tume, hakuna popote ilipothibitishwa kuwa Sioi alipata uraia wa Kenya. Kwa kuwa mrufani ndiye aliyetoa madai kuwa mgombea alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa kwake Kenya, basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni," alisema.
 
Bora hivyo maana ushindi wa kirahisi rahisi hauwagi mtamu. Angetolewa huyo Naoa ushindi wa CDM usingekuwa na raha kabisa...
 
Nec ni mpaka wao wawe na maslahi na jambo hilo.otherwise,ndo maana sishangai hata Makamba katibu wa chama wakati huo alipoibuka na kusemea yale ya kiuhamiaji
 
unajua bwana sheria sio mambo ya propaganda lazima uwe na ushahidi wa juu ya unalolizungumza.nadhani sasa ni wakati wa kujikita ktk kampeni na kunadi sera ili mwisho wa siku wana arumeru waamue mchele ni upi na pumba ni zipi.
 
Tume hiyo hiyo ilimtema BASHE na kumwiita msomali wakati ni mnyamwezi mwenye aslili ya Somalia. Aibu tupu.
 
NEC yamsafisha Sioi (Tanzania Daima)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemsafisha mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, kutokana na tuhuma za utata wa uraia wake zilizokuwa zimewasilishwa katika rufaa na mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari.

Uamuzi huo wa NEC uliotangazwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa tume, Julius Mallaba, akisema kuwa kutokana na sababu kadhaa zilizoonyeshwa na jopo la ‘wataalamu’ wa tume waliokaa kupitia vifungu vya sheria za uhamiaji za Kenya na Tanzania, rufaa hiyo imeonekana haina msingi.

“Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo vilivyowasilishwa pamoja na rufaa ya mrufani na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Katiba ya zamani ya Kenya, Sheria ya Uraia ya Tanzania, Na. 6 ya mwaka 1995, Tume inakubaliana na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa kukataa pingamizi la mrufani kwa sababu zifuatazo.

“Katika maelezo ya mrufani na vielelezo alivyowasilisha tume, hakuna popote ilipothibitishwa kuwa Sioi alipata uraia wa Kenya. Kwa kuwa mrufani ndiye aliyetoa madai kuwa mgombea alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa kwake Kenya, basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni,” alisema.

tujikumbushe mkuu wa nec anachaguriwa na mwenyekiti wa ccm na uchaguzi ni kati ya ccm na cdm musimamizi akiwa mteule wa mwenyekiti wa ccm matokeo yake sitaki hata kujua
 
Tume hiyo hiyo ilimtema BASHE na kumwiita msomali wakati ni mnyamwezi mwenye aslili ya Somalia. Aibu tupu.

This is what we call double standard. Leo unaamua hili kesho unahalalisha hili. Upumbavu huu, halafu inakuwaje unakula desa kwa wa-Kenya. Shame on you!
 
Kumbe sheria zetu zinaathiriwa na sheria za nchi nyingine? mi sikulijua hilo.
 
Haya ndio yaliyotegemewa kwani NEC nayo imekaa kisiasa zaidi, but this is not over yet. I bet kama ikitokea SIOI akichaguliwa, basi atawekewa pingamizi mahakamani kuwa hakuwahi kuukana uraia wa Kenya hivyo kisheria si raia wa Tanzania.

Suala kubwa hapa si kwamba SIOI ni raia wa Kenya, bali kwa kuzaliwa kwake katika ARDHI ya Kenya anakuwa na HAKI YA UTAIFA wa nchi hiyo (Once such recognition has been conferred, then it follows that rights of citizenship and all other rights accrue to him) . This right (of nationality ) echoes international obligation under Article 7 of the United Nations onvention on the Rights of the Child, which is aimed at preventing the phenomenon of stateless children. This right to be registered as a national commences at birth.

Kifungu hicho kinasomeka
Article 7
1. The child shall be registered immediately after birth and shall have the right from birth to a name, the right to acquire a nationality and. as far as possible, the right to know and be cared for by his or her parents.

2. States Parties shall ensure the implementation of these rights in accordance with their national law and their obligations under the relevant international instruments in this field, in particular where the child would otherwise be stateless.
Je Kenya na Tanzania hawafungwi na Mkataba huu, japo wameuridhia? Na je ni kwa nini hilo jopo la wataalamu halikutumia sheria kama hizi?

Sasa kwa kuwa NCHI hii (Tanzania) haina sheria inayokubaliana na DUAL CITIZENSHIP, ndio maana anatakiwa aukane Uraia wa nchi moja baada ya kutimiza miaka 18, na SIOI hakuwahi kufanya hivyo kwa kuukana URAIA wa Kenya
 
Back
Top Bottom