Pingamizi la CHADEMA Arumeru latupwa nje na NEC

Pingamizi la CHADEMA Arumeru latupwa nje na NEC

Okay,ikae hivi..Sioi sio raia wa Tanzania.Hapa hatutaki kujua kama ni raia wa Kenya,Uganda au kokote kule.Sijui walikuwa wanahangaika na katiba ya kenya ili iwe nini!?Yaani wanataka kuimply kuwa usipokuwa raia wa Tz basi unakuwa raia wa Kenya?shortly ni kuwa hana uraia wa Tz wala wa Kenya.Period.
 
Haya ndiyo majibu niliyotegemea NEC. CCM ninachowapendea ni kwamba wakiamua kumtosa mtu hata kama hana tatizo lolote watamtosa tu. Wakiamua kumpenda mtu hata kama ni Al-shabaab watatumia any means kumhalalisha, hata kama ni shoga watamsafisha by force na watu watamkubali kwa kupofushwa macho na akili. Kwa hili nawapongeza. NEC yao, Jeshi lao kazi inaendelea. Nikikumbuka Uraia wa Bashe, kwa hii ya Sumari napata mashaka sana kama nchi hii inaongozwa kwa misingi ya utawala bora, au kwa akili na uwezo wa mtu fulani. Tanzania nakupenda kwa moyo wote.
 
sasa hili tamu wakashindane tu kwenye sanduku la kura.

Nakubaliana na hii hoja ya KUSHINDANA KWENYE SANDUKU LA KURA. Lakin bado ninajiuliza ni kwa gharama gani? NI kwa gharama ya kuzikanyaga sheria zetu na wajibu wetu wa kimataifa? Ni kwa gharama ya kuweka PRECEDENCE mbovu kwa vizazi vijavyo kwa maslahi ya muda mfupi tena ya kisiasa?

Hivi MM, hujui kwamba mtoto kwa kuzaliwa kwake katika ARDHI ya nchi ya kigeni anakuwa na HAKI YA UTAIFA wa nchi hiyo (Once such recognition has been conferred, then it follows that rights of citizenship and all other rights accrue to him) . This right (of nationality) echoes international obligation under Article 7 of the United Nations Convention on the Rights of the Child, which is aimed at preventing the phenomenon of stateless children.

This right to be registered as a national commences at birth.
 
Ndio madhara ya kuwa na NEC inayotumiwa na CCM kama CONDOM.
 
...ama-kweli tunahitaji katiba mpya harika sana,yaani tumefika hatua ya kuazima katiba ya Kenya?!...
 
Kwa jinsi ninavyofahamu wameru wamechochea moto na hasira. Advantage kwa CDM
 
Tume hiyo hiyo ilimtema BASHE na kumwiita msomali wakati ni mnyamwezi mwenye aslili ya Somalia. Aibu tupu.
Bashe alitemwa na CCM na sio tume jamani, tujaribu kuweka kumbukumbu vizuri
 
NEC yamsafisha Sioi (Tanzania Daima)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemsafisha mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, kutokana na tuhuma za utata wa uraia wake zilizokuwa zimewasilishwa katika rufaa na mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari.

Uamuzi huo wa NEC uliotangazwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa tume, Julius Mallaba, akisema kuwa kutokana na sababu kadhaa zilizoonyeshwa na jopo la ‘wataalamu’ wa tume waliokaa kupitia vifungu vya sheria za uhamiaji za Kenya na Tanzania, rufaa hiyo imeonekana haina msingi.

“Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo vilivyowasilishwa pamoja na rufaa ya mrufani na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Katiba ya zamani ya Kenya, Sheria ya Uraia ya Tanzania, Na. 6 ya mwaka 1995, Tume inakubaliana na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa kukataa pingamizi la mrufani kwa sababu zifuatazo.

“Katika maelezo ya mrufani na vielelezo alivyowasilisha tume, hakuna popote ilipothibitishwa kuwa Sioi alipata uraia wa Kenya. Kwa kuwa mrufani ndiye aliyetoa madai kuwa mgombea alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa kwake Kenya, basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni,” alisema.

Safi sana NEC. Si pambano la mpira , eti timu itapewa ushindi wa mezani kisa imeogopa timu pinzania na kuanza kutafuta visingizio vya ajabu. Tuachiwe wana-Arumeru wenyewe tuamuae tunayemtaka.
 
Nadhani akina Tundu Lissu wanajipanga katika hili kama issue ipo wazi ila sheria imepindishwa makusudi.
 
Bashe alitemwa na CCM na sio tume jamani, tujaribu kuweka kumbukumbu vizuri
hapo ndipo wengi huwa tunapotea njia, kwa hali ya sasa ni kuwa CCM = NEC

Ndio maana wanaochukizwa na hili waliamua hata kujitoa muhanga kwenda hadi ikulu katika kupigania katiba mpya!

 
Mlitaka mpate ushindi wa mezani?
OTIS
 
Mi nawaambieni, na ndyo ukweli, nchii bila kuja kupigana haki hatakaa ije ipatikane!
 
sheria inasema kama wazazi wako au mmoja wa wazazi wako ni mtanzania na wewe unakuwa mtanzania autaomatically. na marehemu mzee Sumari alikuwa mtanzania. sasa suala ni kuthibitisha kama Sioi ni mkenya otherwise inakuwa ni kupoteza muda
 
Kwa maelezo hayo. Je, sheria za Kenya ambazo NEC walizipitia ktk sakata hilo zinahusiana vipi kufikia uamuzi wao?
Hata mimi nisiye Mwanasheria naona wamebofoa, NEC iliwapasa waangalie sheria za Tanzania zinasemaje ktk hilo, kama walivyofanya Idara ya Uhamiaji.
Hili suala litaendelea hata baada ya uchaguzi ikiwa Siyoi atashinda, na NEC wataunganishwa kama walalamikiwa.
Nashauri hata CDM wakishinda, waangalie namna ya kuishitaki NEC Mahakamani, hili suala liko wazi kabisa, na Uhamiaji wawe mashahidi
 
CDM pingamizi lenu ndiyo hivyo limetupwa sijui mtakuja na nini tena! Kote huko ni kutapatapa tu mambo ni magumu Arumeru.
 
Back
Top Bottom