Ole
JF-Expert Member
- Dec 16, 2006
- 2,157
- 975
Mhe Pinda leo amelonga hapa Bukoba mida ya saa 12 na kusema
Pamoja na serkali kuleta maendeleo makubwa Kagera. Pamoja na shule, barabara na mkonga wa mawasiliano.
Bei ya sukari ataishughulikia katika ziara yake. Bukoba ni km 70 toka kiwandani. Hadi tar 8 itatelemka bei.
Kuh amani ya nchi anasema Kikwete amewavumilia sana watanzania. Anasema maandamano haya yanapima uvumilivu wa Kikwete. Ila anasema anavyojua yeye uvumilivu wake unakaribia mwisho. Watu wenyewe hata mabomu mnaogopa, likipigwa moja watu wanakimbia wala hakuna hata mmoja anayesimama. Karibu sasa atasema basi na hapo ndipo mtakapo ona cha moto.
My take baby face anatishia amani ya tz na kujenga hofu katika mioyo ya watu kuwa wakati wowote watashambuliwa na vyombo vya dola.
Anayemvumilia mwenzake ni nani? Wananchi ndio uvumilivu wao umekoma watakiona cha moto wataondoka Magogoni kwa viboko.