Leo tukiamua kusupport mavazi yanayozalishwa nchini tutafika mbali,tunachohitaji ni uzalendo wa kweli na siyo ulimbukeni wa mavazi toka nje.Lingine ni swala la ubora wa mavazi yetu ya ndani, inawezekana watu hawapendi kuvaa mavazi ya ndini kisa tu yanafubaa na kuchujuka upesi.Nia ya dhati ianze na viongozi wetu, ku-ssuport viwanda na kuvaa mavazi ya ndani.
Huyu Pinda asitake kuwapangia watu maisha yao. Haya matamshi yake yameanika utupu wa busara zake. Nashangaa hata huo uwaziri mkuu aliupataje.
Bluray,
..Wachina walikuwa wanavaa uniform kwa miaka mingi sana. baada ya mambo yao kuwa mazuri ndiyo wameanza kuvaa suti.
..nadhani anachokizungumzia Waziri Mkuu Pinda ni tabia ya watumishi wa umma na viongozi kupenda kujirusha wakati hali yetu ya kiuchumi siyo nzuri.
..inawezekana tatizo la Pinda ni mapungufu yake ktk kuwasilisha ujumbe huo. lakini ukweli unabaki palepale kwa serikali yetu ina matumizi makubwa yasiyo ya lazima and something needs to be done.
Bluray,
..Wachina walikuwa wanavaa uniform kwa miaka mingi sana. baada ya mambo yao kuwa mazuri ndiyo wameanza kuvaa suti.
Bluray,
..hata mimi nasubiri kuona kama Pinda ataachana na suti baada ya hili tangazo lake.
..kama hiyo picha imepigwa baada ya Pinda kudai atapunguza uvaaji suti na mambo mengine ya anasa-anasa na ufujaji basi atakuwa amejimaliza mwenyewe kisiasa.
..binafsi nadhani tunakosea kwa kuwa-fixated ktk suala la kuvaa suti. mjadala huu ni mkubwa na mpana na unahusisha UADILIFU na UMAKINI wetu ktk MATUMIZI YA SERIKALI na VIPAUMBELE VYA TAIFA LETU.
Bluray said:Hatukosei, PM ndiye kakosea badala ya kuongea vitu substantive kama nilivyosema hapo juu - viwanda, uzalishaji wa nguo nchini, suti zinazokuwa locally produced with high quality and affordable prices, some even for export since we have all the natural and economic advantages- yeye anaenda kwenye superficialities.
Hii inakuonyesha how weak his thought process is.
Bluray,
..kauli ya Pinda imetoa nafasi ya mjadala huu kuwa trivialized.
..ni kweli kwamba Pinda amekosea.
..lakini kosa kubwa ni kunaswa na mtego wa mapungufu ya kauli ya Waziri Mkuu Pinda. nadhani hilo ndilo tatizo la mjadala huu hapa jamii forums.
Mkuu wangu sema unatania!..Laa sivyo, nitashindwa kuelewa ikiwa kweli Mtanzania mwenye upeo mkubwa kama wako utapendelea kuongozwa na watu kama Mkapa na Lowassa kwa sababu ya hoja ndogo kama hii ya Suit!..ITatizo la Mkapa na Lowassa ni mafisadi arrogant (big issue1) otherwise I would rather have a Mkapa administration with Lowassa as PM than the incumbent jokers.
Mkuu it matters ikiwa PM kazungumzia na nadhani JF wanafanya kile kinachotakiwa kufanya.. Kusema wazi UBOVU wa viongozi wetu, ila tu tujaribu kujifunza na kuongezea vitu muhimu kama ulivyozujngumza hapo juu.Please naomba guys let us go back to issues otherwise we will be like Pinda .. PM asiyejua priorities ? Kuvaa ama kutokuvaa suti , does it really matter?
Mkuu it matters ikiwa PM kazungumzia na nadhani JF wanafanya kile kinachotakiwa kufanya.. Kusema wazi UBOVU wa viongozi wetu, ila tu tujaribu kujifunza na kuongezea vitu muhimu kama ulivyozujngumza hapo juu.
Kiutendaji hizi suti na magari ya fahari ndio sababu watoto wetu hawana nguo wanakaa chini madarsani na wagonjwa wanakufa bila kupatiwa dawa...Serikali yetu ni sawa na mzazi MLEVI hivyo ukizungumzia Pombe kuwa sababu sidhani kama kuna kosa ila jinsi PM Pinda alivyo wakilisha the all issue ndio kichekesho..
Somo bado linabakia palepale huwezi kunambia mlevi wa anasa (pombe) ukasahau familia yake ni swala ya individuals!
If it is a problem ni muhimu tulizungumzie...
Hivi jamani kuvaa ama kutokuvaa suti, do we really want to discuss that as a nation? Kuvaa ama kutokuva suti? I think this is individual issues? Does it deserve the attention we are giving it? Yani our neighbours say Watanzania wanajadili kuvaa ama kutokuva suti?
Kweli dunia itatuchukulia serious kwenye mambo mengine? Kwa nini tusiache pumba zingine ziende na upepo? Nasikia aibu kusoma headline inahusu suti? Wakati watoto wetu wanakaa chini, wagonjwa wanakufa kwa magonjwa yanayozuilika and here we are including JF discussing about suits.
Please naomba guys let us go back to issues otherwise we will be like Pinda .. PM asiyejua priorities ? Kuvaa ama kutokuvaa suti , does it really matter?
Ciao
Pinda yuko sahihi kuvaa suti ni gharama mno kwa uchumi wa nchi na ni kumaliza pesa za kigeni.Kwa nini na sisi tusivae nguo za batiki na vitenge zinazotengenezwa na viwanda vyetu na pamba yetu humu humu nchini.
Kuvaa nguo zetu wenyewe kungesaidia kupanua viwanda vya ndani,vya ushonaji n.k na mafundi cherehani wetu waliozagaa mitaani wangekuwa na soko la uhakika la kazi zao ambalo linachukuliwa na ready made suits za ulaya.Viwanda vyetu vikipanuka na wakulima watalima zaidi na hivyo kupata faida zaidi.Yako manufaa mengi tu ndio maana kiongozi wa Indonesia anapenda kuvaa bidhaa zake zizalishwazo nchini mwake hata kama si nzuri kama suti za ulaya.
Watu wa afrika magharibi na kati huvaa sana nguo za viwanda vyao si kuanzia akina baba,akina mama ndio usiseme hupenda zaidi hizo kuliko za ulaya hivi watanzania kuna nini kwenye vichwa? Afrika magharibi na kati watu wameamshwa sana kuvaa vyao Tanzania wasomi wazima hawaelewi wanamkalia kidedea prime minister wengine hadi kuthubutu kusema apimwe akili.Tanzania ruhusuni uraia wa nchi zaidi ya moja haraka kuna hawara yangu anataka kukimbia nchi kachoka ujinga wa Tanzania.
Kama kweli raisi a mawaziri ni wazalendo na wakareketwa wa nchi na bidhaa zake waanze kuvaa nguo za urafiki,karibu textile na kadhalika na viatu aina ya yeboyebo zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania. Nasubiri kwa hamu siku nitakayoona Kikwete katinga mashati na suruali za kitenge cha urafiki halafu chini akamalizia miguuni kwa kuvaa yeboyebo za sh.elfu moja akienda kukutana na Obama halafu tuone kama Obama atamtambua kuwa ni Raisi wa Tanzania au la kwa kuangalia kitenge na yeboyebo.
.