Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 1, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  • Asema Indonesia wanavaa batiki
  Habel Chidawali, Dodoma

  SIKU moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka viongozi waandamizi waache kununua magari ya kifahari, jana alikuja na lingine jipya kwa kuwataka Watanzania kuachana na vazi la suti akisema kuwa lina gharama kubwa na halifai kwa wananchi maskini.

  Pinda ambaye juzi alikaririwa akisema kuwa ni lazima nchi ibane matumizi kwa magari ya bei ndogo, jana alisema suti wanazovaa Watanzania ni za gharama kubwa ukilinganisha na kipato cha Mtanzania wa kawaida.

  Aliyasema hayo wakati akifunga mkutano wa siku tatu uliofanyika katika ukumbi wa St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, ambako alikuwa mwenyekiti kwa siku zote walipojadili masuala ya mifugo nchini.

  “Tazameni hata nchi ya Indonesia, juzi juzi nilikuwa huko ilinibidi hata mimi na msafara wangu tuache suti zetu na tuvae mashati ya batiki ya yaliyoshonwa kwa kutumia kitambaa cha nchi hiyo, ili tuweze kuonana na rais wao ambaye pia tulimkuta akiwa katika vazi la shati la kawaida kabisa hivi sisi Watanzania kwa nini tunapenda vitu vya kuiga?" aliuliza Pinda.

  Waziri Mkuu alisema kama Watanzania wataamka na kufikiria kuwa wapo Watanzania wenzao ambao wanaishi bila ya kupata hata dola moja, hawatakumbuka kuvaa hizo suti ambazo alisema sio vazi la lazima sana kwa watu maskini kama Tanzania.

  “Pamoja na magari ya kifahari, lakini pia kuna hili suala la kuvaa suti, hivi kwa nini tusiige hata mfano wa Hayati baba wa Taifa kuwa alikuwa akivaa mavazi ya kawaida kabisa, lakini hakuweza kupoteza heshima yake ya Urais,” alisema Pinda.

  Juzi baada ya kutamka kuwa magari ya kifahari hayafai na iko siku atatangaza kupigwa marufuku na kusisitiza kwamba magari ya serikali yatakuwa aina ya Land Cruiser (Hard Top), baadhi ya wadau walianza kutoa maoni yao wakisema kuwa kiongozi huyo alitakiwa kutamka rasmi ni lini serikali itaachana na mashangingi.

  Hata hivyo baada ya kusikia maoni hayo, Waziri Mkuu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Serikali jana alisema katika bunge la bajeti lijalo kutakuwa na kazi moja tu ya kupitisha bajeti ya kununua magari ya bei nafuu bila ya kutaja ni aina gani ya magari yatakayonunuliwa.

  Kama alivyofanya juzi kwa kutolea mfano wa nchi ya India ambayo alisema kuwa imebana matumizi ya magari ya kifahari, jana alitoa mfano wa nchi ya Indonesia ambako alisema hata vazi la Taifa ni nguo iliyoshonwa na batiki ya nchi hiyo.

  Wakati huo aliwatahadharisha wakurugenzi na viongozi wa wilaya ambao wanapenda kukaa maofisini muda wote bila ya kwenda vijijini kukagua shughuli za maendeleo ambapo alisema jicho lake litawamulika watu hao na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika na makosa.

  Alisema umezuka mtindo wa baadhi ya viongozi katika halmashauri ambao wanatumia muda mwingi kukaa ofisini na kupulizwa na viyoyozi ili hali maisha ya Watanzania huko vijijini yanakuwa ni ya hatari na wanategemea msaada wao.

  Katika mkutano huo kulikuwa na maazimio 11 ambayo aliagiza utekelezaji wake uanze kabla ya kumalizika kwa mwezi Oktoba na akamtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, John Magufuli kuendelea na kasi aliyonayo na kwamba yeye Pinda atakuwa nyuma yake akimuunga mkono.

  Huku akiyasema hayo, ziara iliyofanywa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa Septemba, 2007 katika mataifa hayo ya mashariki ya mbali ilizaa wazo lililoisukuma serikali kutaka kuleta wataalamu kutoka Thailand kwa ajili ya kutengeneza mvua, maarufu kama 'Mvua ya Lowassa'.

  Hata hivyo, mpango huo ulivurugika wiki chache baada ya Lowassa kurejea nchini, kufutia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Serikali ya Waziri Mkuu, Thaksin Shinawatra, yaliyotokea Septemba, mwaka jana.

  Kupinduliwa kwa Shinawatra na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Sonthi Boonyaratglin, kulivuruga mpango huo ambao uliombwa na Lowassa wakati Tanzania ikikabiliwa na ukame, uliosababisha kukauka kwa mabwawa ya kuzalisha umeme.
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  huyu bwana ana kazi mie naona mengine sio ya kusema angeachana nayo

  maana sasa watamuuliza mbona ww unavaa na hapo jibu sijui litakuwaje? abakie pale pale tena kwa vitendo kuhakikisha matumizi ya serikali kwa vitu visivyo vya lazima yanapungua akianza na ofisi yake tena aect aaccordingly sio kutuletea ngonjera
   
 3. w

  wasp JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je Waziri Mkuu Mhe. Pinda analionaje swala la kupunguza gharama ya masurufu na mishahara mikubwa ya wabunge na viongozi wenzake wakati wafanyakazi wa kawaida na walalahoi wengi wanataabika kupata mlo mmoja kwa siku?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nadiriki kusema huyu Pinda akapimwe akili..hatuwezi tukawa na PM anaropoka ropoka tu mambo yasiyo na mantiki,yaani yeye kipimo cha matumizi ya pesa na anasa ni kuvaa suti??hivi huyu ana nini?mi ananitia mapka kichefuchefu jamani
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu bwana anatafuta umaarufu kwa njia za mkato; kama kweli hayo ya mashangingi na suti za bei mbaya vinamkera angeonyesha yeye mwenyewe kwa vitendo!! Angeanza kwa kuliweka kando shangingi lake na akatumia Suzuki halafu akaanza kuvaa mashati ya batiki halafu tuone kama wachini yake watamuiga au vipi? Mkwere yeye amekwisha rogwa na waamerika hawezi tena kuacha suti na kupanda vigari vidogo yeye ni mtu wa mashangingi na BMW kama MSWATI. Pinda aangalie kwani wanamtandao ndio wanaovaa suti za bei mbaya ingawa nyumbani kwao baba zao na mama zao wanalala kwenye matembe!!
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  huyu bwana hajui atendalo nayaelekeaa hii nafasi inampwayaa sanaaaaa..

  ana mengi ya kufuatilia na kusimamiaa katika utendaji wa kila siku wa serikali.
  kama anataka kupromote local industry sio lazima kutoa ngonjera ka hizi zaidi ya kuonyesha kwa vitendoooooo

  pinda badilikaa, wakati ni ukuta.
   
 7. c

  chach JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 433
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Huyu ndiye pm wa bongo' hivi tutafika kwa mwendo huu.mwisho atasema tusile nyama ni expensive.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mamaweeee yaani nilitaka kusema hivo hivo atasema kula wali nyama ni expensive so watanzania tule ugali wa muhogo na mchicha kupromote kilimo kwanza
   
 9. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani Kigogo wewe ndiwe unapaswa kwenda kupimwa akili yako. Pinda wakati wote anazungumza mambo ambayo yakiangaliwa na kuzingatiwa kwa makini yanaweza yakailetea mabadiliko makubwa nchini mwetu.

  Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.

  Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

  Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  sometimez wanaongeza mshahara sh .4500 why ?:)
   
 11. I

  Inviolata Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhh! Kichekesho! Mhe Pinda mara ya mwisho aliwaasa watendaji wakuu serikalini kuacha kuagiza magari ya kifahari, hajui kwamba watanzania tumechoka kusikia porojo kila kukicha. If you want to take action you dont have to go to the media and say, chukua hatua tuone mashangingi serikalini yameisha barabarani, hapo hatahitaji hata kusema sie watanzania tutaona tu. Yaani huyo ni Waziri Mkuu eti anahasa, badala ya kuamuru. hivi kweli hapa tuna viongozi kweli, Inasikitisha.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asante kiongozi kwa kumbukumbu nzuri ,huyu huyu Pinda alisema hakuna kufanya semina mpaka yeye atoe kibali,watu wanang`ong`a wanadunda semina kila kukicha..mi sijaona kitu alicho initiate Pinda kikawa successful kwa kweli..kura za maoni ya albino mpaka leo kimya and they spend hela ya walipa kodi to do it,,wapi report ya CAG kuhusu UBUNGO BUS Terminal???
   
 13. M

  Muuza Maandazi Member

  #13
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  PM lazima afikirie umakini unaotakiwa kuzungumzia mambo muhimu katika nchi yetu...muda wa kusema bila ya kutenda umekwisha. ameshasema vitu vingi lakini hakuna utekelezaji maana labda alikuwa anafurahisha baraza tu. kwa mfano tunataka tumwone sasa anayatekeleza yeye mwenyewe kwana...nakumbuka sokoine alikuwa anavaa safari buti na kutembelea landrover 109...hakutowa kauli ila kesho ameamka na kuitekeleza. tatizo wakubwa wetu sasa wanasema mambo kama wanashauri vile kumbe wao ndo wanatakiwa kuyatekeleza kwanz...posho za vikao alizikataza pinda lakini mpaka leo watu wanalipana maboresho...juzi tanesco wamenunua mashangingi...wizara inasema inachunguza...huyu pm kweli anahitaji ushari nasaha.
   
 14. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aibu kubwa. kama waziri mkuu anaongea hivyo , mtu wa kawaida ataongea nini? hii inaonesha ni kiasi gani waTanzania tilivyo wapumbavu. nikiwemo na mimi . İnakuaje Tanzania inaongozwa na watu kama hawa? mimi nimechoka na hii nchi. sioni matumaini ya aina yeyote yale. ikili za waTanzania zimedumaa ,tuko kama wadudu , hatuna thamani popote pale duniani na hata ndani ya Tanzania. sio siri mimi naona iabu kuwa mTanzania.
   
 15. F

  FOE Member

  #15
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona mtu akienda nje ya nchi tu basi anafikiri kila akionacho huko ni lazima alete bongo hata bila kutumia akili akakaa na kutulia. Ndio matatizo ya watu tuliosoma hapa bongo. Tukitoka nje kidogo basi tunaona kama vile kila kitu tunachokiona ni lazima tukilete home. Hivi huyu jamaa anafikiri hizo nchi za Asia ndio kioo kikubwa kwetu kuliko nchi zingine zote duniani? Hivi kila aendae nje akileta anayoyaona kuimpliment hapa bongo tutakuaje jamani? Kila alikoenda lazima alete maneno ya ajabu tu...kenya,india,indonesia ...arghhhhh!!!!
   
 16. M

  Muuza Maandazi Member

  #16
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mi sioni aibu kuwa mtanzania...wala siamini samaki mmoja akioza ndo wote waoze...kama wao wajinga mimi sio...nakuombeni musione aibu kuwa waTZ tujitahidi kuwabidilisha wenye mawazo mgando.
   
 17. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hivi huyu bwana pamoja na mheshimiwa Rais si wana bajeti za mavazi katika ofisi zao? Wangeanza kwanza na kuziondoa hizo
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Oh My Dear Lord,

  Help thee

  PM Pinda anahitaji counselling ya haraka:

  Kila kukicha anashangazwa

  1. Semina za wafanyakazi wa serikali

  2. Magari ya kifahari ya viongozi

  3. Kuvaa suti wafanyakazi wa serikali

  4. ... who knows ... Mishaara minono ya wafanyakazi wa Umma

  this is very very very LOW for a Prime Minister!
   
 19. GP

  GP JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamaa ni mjamaa kwelikweli, tangu enzi za mwalimuuuuuuu!
   
 20. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Bludgeoning buffoonery.
   
Loading...