Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

wazanzibari pumbavu kabisa ndiyo maana hamjaenda shule..na wanaotaka sana kuvunjika kwa muungano ni viongozi wenye uchu..
lkn mi pia ntashukuru tu uvunjike ili waarabu waingie rasmi zenji..na tuone kitakachoendelea

Wacha Upumbavu wako . Hiyo elimu yako ina maana gani kama unashindwa kuandika hata mstari mmoja wa hoja?
 
Msemo wa "umoja ni nguvu utengano ni udhaifu" ni msemo wa Kiswahili na Wazanzibari hilo wanalijuwa. Wazanzibari ukiachia wachache wenye jazba wanaupenda Muungano hivyo jawabu Muungano uwepo.
Hapa kuna tatizo la lugha ya kiswahili na utamaduni wan kutumia lugha hiyo. Wazanzibari wanapotoa macho wakisema -hatutaki basi ala- upumbavu huu!!. Siyo kama hawataki kweli, lakini wanataka wasikilizwe, ni namna gani wanavyotaka wao huo Muungano uwe ili uweze kukidhi haja na matarajio yao kwa jinsi ambavyo wanaona wanaweza kufaidika na Muungano huo kama vile wenzaio wa Tanganyika wanavyofaidika. Wa-Tanganyika inaoneklana wanashindwa kuelewa lugha ya Wazanzibari na utamaduni,uzoefu na mbinu zao za kujieleza. Nafikiri wawasome wenzao katika hilo kwanza.
 
Wapi Bwana huo ni mtizamo wako lakini wakubwa wako hawana mtizamo huo. Angalia yaondolewe mafuta tu kipovu kinawatoka hawana haya wala soni wakizani Muungano ni Mafuta tu leo Wazanzibari waseme wanajitowa si mauwaji na mafunzo ya kuuwa . Angalia wakati wa uchaguzi tu leo useme kujitangazia kujitowa Muungano. Muungwana ni vitendo kama mmechoka kuambiwa ukweli tangazeni nyie ili Wazanzibari wasage meno kama mnavyodhania.

,,,,,,Mafunzo ya mauajii???,yakitokea wapi tenaa NGEKEWA???,unajua hii kitu sio rahisi kama unavyoizungumza sheikh,hapo zenji kuna WAZANZIBARI na WAZANZIBARA,na hayo mafunzo na pengine MAUAJI basi yataandaliwa na WAZANZIBARA ambao hawawezi kukubali kwa urahisi kabisa kupoteza ndugu zao kibao waliopo huko BARA,ishu ya MAFUTA inaweza kuwa ni ishara moja wapo ya kuonesha ni kiasi gani wa ZENJI ni wachoyo tu na kutaka kufaidi peke yao rasilimali hii,lakini hawajiulizi,au pengine hawajui kwamba huu UMEME ambao wanaupata tena kwa bei rahisi kuliko watumiaji wa BARA unatokana na hio GESI kutoka MNAZI BAY,sasa kama ugomvi ni mapato,sijui hapo inakuaje,lakini sijawahi kusikia watu wa Kilimanjaro wakisema wagaiwe MAPATO yatokanayo na GESI hio.
 
Pinda alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ziwani Ali Said Salim (CUF), aliyetaka kujua mambo ambayo si ya Muungano yanaongozwa kupitia serikali gani, wakati kwa Zanzibar yanasimamiwa na Serikali ya Mapinduzi (SMZ).

Akijibu swali hilo, Pinda alisema serikali ya Tanganyika haipo na kwamba mambo yote yanayohusu shughuli zisizo za Muungano yanaongozwa na serikali ya Muungano.

Alisema mambo ambayo si ya Muungano kwa upande wa Zanzibar huongozwa na serikali ya Zanzibar, isipokuwa kwa upande wa Tanganyika mambo hayo huongozwa na serikali ya Muungano kwa kuwa Tanganyika haipo na hakuna serikali.

“Kusema kweli mimi ningekuwa kama nabii na mtume Issa ningesema kuwa naam,hapo umenena kuwa serikali ya Tanganyika ilimezwa na serikali ya Muungano na ndivyo ilivyo kweli,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu alisema kuwa ndoto yake kubwa ni kuona kuwa siku moja kunakuwa na mfumo wa serikali moja na nchi moja kuliko ilivyo sasa ambapo kuna serikali mbili ndani ya nchi moja.
"Suluhu ya Muungano ni nchi moja na serikali moja, ndipo kelele zote zitakwisha,"alisema Pinda.
 
1. Hata England ingependa UK siku moja iwe moja! Je Skotilandi, Wales watakubali??

2. Sema Visiwani ni ndogo sana kwa watu, uchumi na eneo: wana faida zaidi kuwa na 'good father' Bara kuliko kuwa wenyewe!
 
Get your facts right:

1.England washawchoka Scotland na vice versa...na Scotland possibly in the next 5 to 10 years wanaweza kuaondoka kwenye Muungano na England..Alex Salmond na SNP ndiko wanakoelekea afterall The party's main policy is full independence from the United Kingdom.

2.That is based on what? It certainly isnt based on economic analysis. As economic integration continues, economics views political disintegration as increasingly more beneficial for Zanzibar..na hizi comments za kutaka kuwa godfather to this and that ndizo zitakazo waponza nyie waTanganyika

alway arrogant as if mna birth right to Unguja na Pemba

3. Pinda anaongea kama vile anafikiri bado yuko Usalama wa taifa ya 1970's
 
Last edited by a moderator:
Daima ndivyo ninavyoamini siku zote, vingenevyo kila mtu apewe kipande chake aishie! Ni ukweli usiopingika kuwa kwa vyovyote kwa muundo huu ni lazima upande mmoja uwe unalemea upande wa pili. Na katika hili Tanganyika ambayo haipo inaumia zaidi kwa sababu kwetu ni kwao ila kwao ni kwao!
 
Tatizoni hizocolonialmindset walizonazowaTanganyika...mentality na sentiments zao hazina tofauti sana na wakina Edward Twinning
 
Kwa nini suluhisho lisiwe kuwa na serikali tatu na kwa nini iwe ni serikali moja ndo suluhisho peke yake?
 
Get your facts right:

1.England washawchoka Scotland na vice versa...na Scotland possibly in the next 5 to 10 years wanaweza kuaondoka kwenye Muungano na England..Alex Salmond na SNP ndiko wanakoelekea afterall The party's main policy is full independence from the United Kingdom.

2.That is based on what? It certainly isnt based on economic analysis. As economic integration continues, economics views political disintegration as increasingly more beneficial for Zanzibar..na hizi comments za kutaka kuwa godfather to this and that ndizo zitakazo waponza nyie waTanganyika

alway arrogant as if mna birth right to Unguja na Pemba

3.Pinda anaongea kama vile anafikiri bado yuko Usalama wa taifa ya 1970's

Tatizoni hizocolonialmindset walizonazowaTanganyika...mentality na sentiments zao hazina tofauti sana na wakina Edward Twinning

Mkuu GT imekuwaje siku hizi mbona?.......
 
Kwa nini suluhisho lisiwe kuwa na serikali tatu na kwa nini iwe ni serikali moja ndo suluhisho peke yake?

kwasababu hakuna mtanganyika anyelilia kuwa na serikali ya Tanganyika zaidi ya Mchungaji C. Mtikila. Kwa Ujumla wetu hatuna shida ya serikali ya Tanganyika na tungependa kuwa na Tanzania Moja yenye Rais mmoja, wimbo wa Taifa mmoja, na Zanzibar ni Mkoa na Mh. A. Karume ni mkuu wa mkoa wa Zanzibar. Hii ndio Ndoto yangu Pia,
 
Mzee unasema Zenji iwe kama Arusha au Rukwa kwa Mzee Pinda, bana na Karume awe kama Njoolay tuu bana?? Maalim Seif na CUF watagombea nini baada ya hapo hawawezi kukubali. Think narrow
 
1. Hata England ingependa UK siku moja iwe moja! Je Skotilandi, Wales watakubali??

2. Sema Visiwani ni ndogo sana kwa watu, uchumi na eneo: wana faida zaidi kuwa na 'good father' Bara kuliko kuwa wenyewe!

Kuwa Visiwa wala udogo hakuifanyi Zanzibar kuihitaji Bara kiasi cha kuleta ukoloni katika zama hizi. Hali inaonyesha kuwa Mataifa yanaamuwa kujitawala zaidi kuliko kutafuta kutawaliwa . La msingi kuwa mwenye tumbo ndiye anaejuwa kiasi cha njaa aliyonayo na kwa maana hiyo iwachiwe Zanzibar iamuwe mambo yake.
 
kwasababu hakuna mtanganyika anyelilia kuwa na serikali ya Tanganyika zaidi ya Mchungaji C. Mtikila. Kwa Ujumla wetu hatuna shida ya serikali ya Tanganyika na tungependa kuwa na Tanzania Moja yenye Rais mmoja, wimbo wa Taifa mmoja, na Zanzibar ni Mkoa na Mh. A. Karume ni mkuu wa mkoa wa Zanzibar. Hii ndio Ndoto yangu Pia,

Huo ndio colonialmindset aliozungumza GT. Hivyo WHO ARE YOU wa kutaka matakwa yenu ndiyo yawe ya jumla. Iwapo kama wenzetu mna fikira kama hizo hamuwezi kuwa na kitu cha ujumla na hivyo bora mrizike na Mafia.
 
kwasababu hakuna mtanganyika anyelilia kuwa na serikali ya Tanganyika zaidi ya Mchungaji C. Mtikila. Kwa Ujumla wetu hatuna shida ya serikali ya Tanganyika na tungependa kuwa na Tanzania Moja yenye Rais mmoja, wimbo wa Taifa mmoja, na Zanzibar ni Mkoa na Mh. A. Karume ni mkuu wa mkoa wa Zanzibar. Hii ndio Ndoto yangu Pia,

Nafikiri kuwa hii ni ndoto nzuri ya kuwa na Serikali moja Tanzania na sio serikali mbili ndani ya nchi moja hata mantiki haipatikani.Lakini mchakato wa kuwa na Serikali moja utakuwa mgumu na wa muda mrefu na unahitaji uongozi dhabiti kusimamia hilo.

Swali langu ni kuwa je huu ndio wakati muafaka wa kuanza mchakato huo na kama jibu ni ndio je tuna uongozi dhabiti wa kusimamia mchakato huo pamoja na changamoto zake?mimi sijui najaribu kufikiria kama inawezekana sasa.
 
Hiki tuliwahi kukiongea hapa kwani migogoro haitaisha mpaka watakaombiwa kuwa wao ni mkoa mmojawapo wa tanzania na raisi wao kuwa mkuu wa mkoa ndio watajua kuwa tanzania bara ndio yenye maamuzi juu ya zanzibar.

Nasema tanzania bara ndio yenye maamuzi juu ya zanzibar kwani viongozi mlionao wanaogopa kuondolewa madarakani na CUF kwahiyo wakiambiwa kuwa inabidi muwe mkoa wa tanzania watakubali tu, kwani kujitenga maana yake CUF wanachukua nchi na hakuna ambacho serikali yenu haitafanya kwakuwa haina jeshi wala polisi wa kuwazuia CUF kuchua nchi badala yake polisi na wanajeshi wa zanzibar watawasaidia CUF kuingia madarakani.

Huu ni wakati kuhafaka zanzibar kuwa mkoa wa tanzania kama hawataki wajitenge tuone kama CCM zanzibar watakubali kujitenga.
 
Sasa hivi viongozi wa CCM zanzibar wanapiga kelele kama kutingisha kiberiti lakini hawawezi kukubali kujitenga wakati wanajua watatolewa madarakani na CUF.

Kama wananweza waombe kujitenga kwanini wanaongea pembeni wakati tanzania bara wansema kabisa, nafikiri sasa umefika wakati wa kufuta serikali yao watulie kimya.
 
Get your facts right:

.......na hizi comments za kutaka kuwa godfather to this and that ndizo zitakazo waponza nyie waTanganyika

alway arrogant as if mna birth right to Unguja na Pemba

3.Pinda anaongea kama vile anafikiri bado yuko Usalama wa taifa ya 1970's

Yamekupata yepi tena GT.

Jenga hoja kwa umakini tu, tutaelewa.
Hakuna sababu ya kumshambulia mtu binafsi kwa kiwango hicho.
Endapo hukubaliani na hoja yake basi elezea kwa hoja zilizo na nguvu zaidi kudhihirisha ubora wa hoja zako na siyo kutumia lugha zisizokubalika ktk JF na pengine popote penye jukwaa la wastaarabu.

Suala la muungano si la kujadiliwa kwa jazba wala ubinafsi, linahitaji sana kuzingatia maslahi ya kila mmoja anayehusika ktk muungano wenyewe na ukomavu wa kisiasa.

Hoja ya kuifanya Tanzania iwe na serikali moja, "HAIKUBALIKI".
Nadhani ni budi hata mheshimiwa sana Pinda alijue hilo.
Itafutwe mbinu nyingine yoyote lakini siyo serikali moja. Lazima Zanzibar iendelee kuwa na serikali yake. Si vizuri kupoteza utaifa wa Zanzibar. Hoja hii haiuziki kwa wazanzibari, hata kidogo.

Pia suala la kuuvunja muungano, HALITAKIWI.
Tuudumishe muungano wetu kwa hali yoyote ile.
 
Pinda azidi kupindisha ,hebu atupe yote hayo na ayaweke kando ,hebu muulizeni hesabu zake za kura za kuwataja wauaji wa Maalbino zimefikia wapi mbona kimya ? Ya Zanzibar ndugu Pinda huyawezi yamemshinda Baba yako au Yenu Nyerere mtayaweza nyie mnaoendeshwa mbio na wahindi watatu ?
 
Back
Top Bottom