Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

wakatwe na waaibishwe tu mana tumechoka.
Nafikiri sasa wameelewa maana halisi ya msemo "siasa ni mchezo mchafu". na wanajuta kwanini walichukua fomu za kugombea urais.
mtu kama Ramadhani, mchungaji mzima, amestaafu utumishi wa umma lakini bado anatamani vyeo vya kisiasa. wamefuata nyuki ili wale asali lakini wameambulia manundu baada ya kung'atwa.
 
Ni kweli utawala wa JK umekuwa wa kiujanja ujanja,fitina, udugu, chuki na makundi. Hili jambo siyo siri ndivyo alivyoingia pia kwenye madaraka ya urais. Watendaji wake wamekuwa hawamwamini kwa jambo lolote, hata wanapotaka kfanya maamuzi yoyote hata kwenye nafasi walizo na dhamananazo huhofia bosi wao atawaonaje. Hili pia limejidhihirisha pale waziri anaposema lingekuwa langu ningeamua hivi, lakini kwa sababu kuna mkubwa wangu siwezi kuamua. Tafsiri rahisi ni kuwa maamuzi hayapo kiserikali yako more Personal kuliko kuwa oficialised.




Lakini wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa mwaka 2015 wamemthibitishia JK kuwa CCM si chama cha wajanjajanja kwa kumchagua Magufuli kwa kuangalia umahiri utendaji kazi wake.
Ni kama uchaguzi wa mwaka 1985 wakati Nyerere alimwandaa Salim Ahamed Salim kuwa mgombea wa rais kwa kuangalia uchapakazi wake akisindikizwa na mtu aliyedhani dhaifu Ali Hassan Mwinyi, lakini wajumbe wakamchagua Ali Hassan Mwinyi kwa kuangalia Upemba na Uunguja. Wakakataa kuwa rubber stamp wa Mwalimu. JK alimtaka Bernad Membe au Rose Migiro lakini akitaka asindikizwe na John Pombe Magufuli, wajumbe wa Kamati kuu na Mkutano Mkuu wamekataa kuburuzwa na JK wakamchagua John Pombe Magufuli.
Kingunge nimemzungumzia sana katika uzi mwingine nisingependa kurudia lakini itoshe kuwa maoni yake hayako huru kwa sababu yupo kundi la Lowasa hivyo anakosa uhalali wa kuwa hakimu katika shauri alilo na maslahi nalo.

Tatizo ukizungumzia tu utaratibu haukufuata wanaanza we TimuLowasa! No kwa kweli utaratibu huu ulikuwa na Risk kubwa sana Risk kubwamnooooo! Ni Mungu tu aliepusha majanga. Kwani angechaguliwa mwingine zaidi yaaliyechaguliwa. Amini nakuambia tungesikia mengine. Kwa sasa hata vyama vya upinzanivimepwaya.
 
Kwa kitendo cha kutolewa na kamati ya maadili logic ya CCM ni km ya punda..Pinda nae hana maadili ila utayakuta maccm yakimwita mtiifu.
 
Hata mie nimepata taabu sana na hii ccm kiasi kwamba sasa naamini hakuna msafi au anayeaminika ndani ya chama hicho.
Sijaelewa kwa nini Lowasa na Sumaye wote wametupwa bila maelezo! Na sijaelewa na sintaelewa kwa nini Pinda na Bilali wasiwe kati ya 5 bora. Wanatakiwa wawe wameshajiuzuru kabisa sasa hivi.
Naamini ccm wanakwenda na upepo wa yeyote aliyechaguliwa. Nimejiuliza mara zote Magufuli kama ni mzuri kiasi hicho mbona hata wasimpe u PM kabla? Tunauziwa mbuzi guniani.
 
kwa nini wawe makam na wazir mkuu kama hayo uliyoyasema ndo uharisia wao mbona kikwete asingewatimua au asingewashaur waache kugombea

ccm walikuwa na vigezo 13 katika mchakato wao ,hivyo waliokidhi vigezo vyote bila mbwembwe wala kupenyeza rupia ,au kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini wao imekula kwao
pili katika kupata wagombea ccm wana balance makundi ,wazee ,vijana ,beijing,nk ndio maana unawaona wakina makamba
 
ccm walikuwa na vigezo 13 katika mchakato wao ,hivyo waliokidhi vigezo vyote bila mbwembwe wala kupenyeza rupia ,au kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini wao imekula kwao
pili katika kupata wagombea ccm wana balance makundi ,wazee ,vijana ,beijing,nk ndio maana unawaona wakina makamba

Kwa hiyo, hiyo ndio demokrasia?
 
Wapumzike kunusuru kajiheshima kao kaduchu kalikobakia mana hakafiki Hata mb8
 
General wa jeshi; mwanasheria imara jeshini; jaji mkuu na Padre Agustino John Ramadhani kweli hana maadili hata ashindwe kupenyeza kwenye kamati ya maadili. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Hakuwa mwenzao kwa maana ni msafi.Ni sawa na kumuonyesha extenal auditor madhambi yako.
 
Maadili ni madili ya kufuga wala rushwa. Wote walioachwa wasingeweza lea wala rushwa PERIOD!
 
ccm walikuwa na vigezo 13 katika mchakato wao ,hivyo waliokidhi vigezo vyote bila mbwembwe wala kupenyeza rupia ,au kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini wao imekula kwao
pili katika kupata wagombea ccm wana balance makundi ,wazee ,vijana ,beijing,nk ndio maana unawaona wakina makamba

hapo sasa umejichanganya zaidi makamba na membe wote walifungiwa kwa kosa lakuanza kampen mapema leo wewe unasema vigezo 13 sema hivi bwanamkubwa alikuwa na safu yake
 
Kama kaaachwa Makongoro kwanini eengine wasiachwe ama wangechaguliwa wote?
 
Nilikuwa nawaambia humu ni magufuli aliyekuwa anafaa zaidi ya wengine, na mwingine nilikuwa namtaja mwakyembe. Nchi hii inahitaji watu wa aina yao kuisogeza mbele. na hawa wanajulikana na watu na ni wachapa kazi wazuri. Na walikuwa wanang'aa katika mazingira magumu. Sipati picha mg'aro kwa magufuli akiwa yeye ndo rais wa nchi.

Tusubir tuone.

Hata ukawa watapata kazi kubwa kupambana nae kwenye urais. Labda hili si la muhimu kwako ila ni la muhimu sana kwa ccm.

Angepita mwingine zaidi ya hawa wawili njia ya ukawa magogoni ingekuwa kama kwenda sokoni. Au ingekuwa kama kumsukuma mlevi
 
Katika hao watatu uliowataja siamin kama kuna mmoja kati yao ambaye angeimudu ukawa. Na huenda cdm isingehitaji ukawa kupambana na mgombea wa ccm na kushinda. Ingekuwa na uhakika na Dr slaa kupita. Kuna wengine humu ndo walichokuwa wanakitaka

Lasivyo, kama nilivyokuwa nawaambia, ili ccm ishinde kama mgombea wake asingekuwa magufuli au mwakyembe basi ingetakiwa mabomu na silaha zingine nyingi na askari kibwena wawepo. Sasa hii ingekuwa nini? Kama si kuhatarisha tu usalama wa nchi na kujitafutia tu matatizo yasiyo ya lazima
 
hiki kitu kimenishangaza,yaani kamati ya maadili ilikosa imani kwa jaji mkuu ambaye ni kiongozi wa mfumo wa utoaji haki,waliona nini kwa huyu bwana ramadhani,kamati ya maadili ilikosa imani na msaidizi wa karibu wa rais,makamu wa rais gharib bilal,na pia waziri mkuu,hawa ni watu wa karibu sana na rais,membe naye kapigwa chini na kuvunja mila ya waziri wa mambo ya nje kuwa rais kama ilivyotokea kwa mkapa na kikwete,hakika awamu ya nne ilikosa muelekeo
 
Watangazi nia 33 kati ya 38 wa kugombea urais wa Tanzania kupitia CCM walienguliwa na kamati ya usalama na maadili kwa sababu ya kukosa maadili ikiwemo kununua uongozi na kutishia chama!!

Hii ni ajabu na kweli kwamba hata viongozi ambao bado wapo serikalini kama makamu wa rais Dr. Bilali, Waziri Mkuu Pinda, Mwandosya na mawaziri wengine nao wameunganishwa na wakosa maadili wengine!!

Jambo la kushangaza ni kwa CCM kuendelea kuwavumilia viongozi hawa kueneza virusi vya uvunjifu wa maadili serikalini na chamani!!

Kikubwa cha kujiuliza ni kwa nini CCM haichukui hatua ya kuwavua uongozi na kuwafukuzilia mbali chamani ili liwe funzo kwa wengine na kurejesha imani ya chama kwa wananchi?!
 
Ccm kila kitu kwao kinawezekana ndio maana hata wao hawalalamiki wanalalamika wanachama na wakereketwa wao tu
 
Kwa Fisadi alitakao lolote lawezekana hata wakitaka kuwazika viongozi huku wakiwa hai hawashindwi.Ukiridhika na huo mfumo wao endelea kuwasappoti na kama unapenda mabadiliko na maendeleo ya kweli basi waruhusu wapinzani nao waongoze
 
Back
Top Bottom