Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

hiki kitu kimenishangaza,yaani kamati ya maadili ilikosa imani kwa jaji mkuu ambaye ni kiongozi wa mfumo wa utoaji haki,waliona nini kwa huyu bwana ramadhani,kamati ya maadili ilikosa imani na msaidizi wa karibu wa rais,makamu wa rais gharib bilal,na pia waziri mkuu,hawa ni watu wa karibu sana na rais,membe naye kapigwa chini na kuvunja mila ya waziri wa mambo ya nje kuwa rais kama ilivyotokea kwa mkapa na kikwete,hakika awamu ya nne ilikosa muelekeo

Mkuu bora Membe alifikishwa kwenye vikao husika na akabwagwa kwa njia ya kura! Ila Kamati haikuwa na imani na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ila ikawa na imani na Naibu Waziri! Kwa siku zilizobakia Rais anapokuwa nje ya nchi atalazimika amwachie nchi huyo Naibu Waziri au itakuwaje? Hao hata wakiachiwa watakuwa na moral authority ya ki-uongozi kweli? Au ndo bora liende mpaka siku ziishe?
 
Maadili ni madili ya kufuga wala rushwa. Wote walioachwa wasingeweza lea wala rushwa PERIOD!

Sahihisho dogo tu,hapo kwenye wote ingekuwa vyema kama ungeweka wengi.Maana kuna MAJANGILI walichukua form pia na hawakuingia ile tano bora.
 
Mkuu bora Membe alifikishwa kwenye vikao husika na akabwagwa kwa njia ya kura! Ila Kamati haikuwa na imani na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ila ikawa na imani na Naibu Waziri! Kwa siku zilizobakia Rais anapokuwa nje ya nchi atalazimika amwachie nchi huyo Naibu Waziri au itakuwaje? Hao hata wakiachiwa watakuwa na moral authority ya ki-uongozi kweli? Au ndo bora liende mpaka siku ziishe?
lazima kulikuwa na tatizo la unafiki kati ya viongozi wa juu,hasa bosi mwenyewe
 
Jamani lazima tutambue ili kuwa Rais ni zaidi ya uadilifu tu.
Ni kweli uadiiifu wa Pinda, Bilali na hao wengine hauna shaka. Lakini Je kama CCM ikiwasimamisha hao nini nafasi yao ya ushindi?

kwa mtazamo wangu CCM ina nafasi kubwa kupitia Magufuli kuliko kupitia Pinda au Bilali.

Pia ukiangaia utendaji wao katika nafasi zao leo, are they Presidential materials? To me NO

Rais must be a tough and aggressive guy like Magufuli and not too soft character.

Lakini kumbuka chaguo la Jk alikuwa Membe na siyo Magufuli.
 
Kwa Fisadi alitakao lolote lawezekana hata wakitaka kuwazika viongozi huku wakiwa hai hawashindwi.Ukiridhika na huo mfumo wao endelea kuwasappoti na kama unapenda mabadiliko na maendeleo ya kweli basi waruhusu wapinzani nao waongoze

Tuwapime Ukawa kwa miaka mitano tu
 
Hata mie nimepata taabu sana na hii ccm kiasi kwamba sasa naamini hakuna msafi au anayeaminika ndani ya chama hicho.
Sijaelewa kwa nini Lowasa na Sumaye wote wametupwa bila maelezo! Na sijaelewa na sintaelewa kwa nini Pinda na Bilali wasiwe kati ya 5 bora. Wanatakiwa wawe wameshajiuzuru kabisa sasa hivi.
Naamini ccm wanakwenda na upepo wa yeyote aliyechaguliwa. Nimejiuliza mara zote Magufuli kama ni mzuri kiasi hicho mbona hata wasimpe u PM kabla? Tunauziwa mbuzi guniani.
Siri sirini lakini nina wasiwasi hata Rais, Kinana na Nape hawako happy na ujio wa Magufuli, imetokea tu kama ajali isiyo na kinga. Nina uhakika watu wenye furaha na matokeo haya ni lile kundi la CCM Mkapa/Mangula/Chiligati/Msuya. Hata Nape mwenyewe anaugulia kwa maumivu ya mgongo hapo alipo ni kwamba tu hana la kufanya maana Magufuli hajaandaliwa vema kuendeleza siri za utawala unaotoka madarakani. Ndiyo maana kuna wakati Magufuli alitupwa wizara ya mifugo na uvuvi ili akafe njaa na kuchanganyikiwa, ni kwasababu tu ya rekodi yake ya kazi wizara ya ujenzi, kelele za watu na kuvurunda kwa Dr. Shukuru kwenye wizara ile ndiko kulikosababisha alejeshwe wizara ya ujenzi tena, hata hivyo aliwekewa Mwakyembe chini yake na hatimaye kupunguziwa ulaji kwa kunyang'anywa uchukuzi na usafirishaji na kupewa mtu mwingine. Hivyo ndugu wananchi mambo yalienda ndivyo sivyo si kwa lowassa tu bali hata kwa mwenyekiti mwenyewe, aliyeramba dume hapo ni akina Mkapa. Jambo baya tu hapo ni kuwaengua hata makamu wa rais na waziri mkuu katika hatua za awali kwa sababu ya kukosa maadili, ni maadili gani hayo wasiyokuwanayo, wizi, kutoa siri, uzee, uvivu, rushwa au nini?
 
Mada hii ni muhimu sana maana itarejewa hata vizazi vijavyo. Kati ya wote walioonekana mbele ya kamati ya maadili kuwa hawana maadili, watakao zungumziwa sana sasa na vizazi vijavyo ni Bilal, Pinda na Ramadani. Kweli hawa wasaidizi wakuu wa rais hawana maadili kwa vigezo vya chama?

Mwalimu alipoachia ngazi alikuwa na chaguo lake, lakini alikubali Mwinyi amrithi ili kutokutoa taswira mbaya kwa umma kuwa hakuwa anamwamini msaidizi wake mkuu. Sasa JK kaonyesha kuwa hakuwaamini wasaidizi wake wakuu. Vile vile hakuwa wazi kwao kwa vile angeweza kuwaeleza mapema kuwa wasichukue form, jambo ambalo lingewaondolea aibu ya kuonekana hawafai mbele ya umma.
 
Sikuwahi kufikiria wala kudhani kuwa kamati ya maadili akiwemo rais Kikwete ingewaona Membe, January, Asha Migiro, Magufuli na Amina walioingia 5 bora ya CCM katika kinyang'anyilo cha kumsaka mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM ni wasafi, wachapakazi, waadilifu na waaminifu kwa taifa letu kuwazidi hata Pinda, Bilali, Sitta, Wasira, Mwakyembe, Jaji Ramadhani na Mwingulu wasaidizi na washauri wakubwa wa rais.

Binafsi niliogopa sana kuona nchi inaongozwa na watu wasioaminika kiasi hiki, lakini niliogopa zaidi kuona rais anasaidiwa na watu asiowaamini kwa kiasi hiki. Kisiki cha watendaji wake wakuu hawa kingekuwa CC, NEC na mkutano mkuu na sio kwenye ngazi ya awali ya kamati ya maadili ambayo na rais ni mjumbe wake na mdau muhimu.

Kama wasaidizi wake hao walikuwa wana mafaili machafu kwanini hakuwaambia mapema kinagaubaga ili waache kutangaza nia ili kuwaepushia kupata aibu kama waliyoipata mbele ya wananchi ya kushindwa hata na mtoto mdogo kama January Makamba kwa uadilifu? Lakini ni kweli Asha Migiro ni mchapakazi na mwaminifu kuliko Pinda, Bilali, Mwakyembe, Sitta na Wasira? kwani kafanya nini kikubwa mno kwenye taifa hili kuwazidi Bilali, Pinda, Mwakyembe, Sitta na Wasira?

Huu ni udhalilishaji wa wazee wetu hawa wakuu ambao nao Kama mzee Kingunge hawana budi kutoa neno japo moja kwa wananchi ili kusafisha makoo yao. Kitaaluma kutoa dukuduku hadharani (mental ventilation) kunaongeza afya ya mtu kuliko kunyamaza na dukuduku moyoni. Wakikaa kimya namna hii ni dalili tosha za wazi kuwa kweli ni wachafu na wasioaminika kupewa urais kama kamati yao ya maadili ilivyoona, hivyo waondoke wapishe wengine waliosafi kwa taifa.

wewe kama si team kushindwa utakuwa ni chadema na mtu asiye na mapenzi mema kwa ccm. viongozi ulio wataja ni watu wenye akili sana kuliko unavowaza na haweza kamwe kusikiliza au kuishi katika msitari wa kipotevu kama ilivyo katika fikira zako
 
wewe kama si team kushindwa utakuwa ni chadema na mtu asiye na mapenzi mema kwa ccm. viongozi ulio wataja ni watu wenye akili sana kuliko unavowaza na haweza kamwe kusikiliza au kuishi katika msitari wa kipotevu kama ilivyo katika fikira zako

Nina kati ya umoja wa vijana wa ccm tangu mwaka 1984 na kadi hai ya ccm tangu 1988 ingawa siishi kutokana na kadi hiyo ingawa nimesoma bure hadi ngazi fulani kutokana na sera za ccm, sina kundi sina mtu ila nasema ukweli mambo yalivyopaswa kuwa, maana nchi hii ni yetu sote kazi ya kufikiria na kusema tunamuachia nani?
 
Jamani lazima tutambue ili kuwa Rais ni zaidi ya uadilifu tu.
Ni kweli uadiiifu wa Pinda, Bilali na hao wengine hauna shaka. Lakini Je kama CCM ikiwasimamisha hao nini nafasi yao ya ushindi?

kwa mtazamo wangu CCM ina nafasi kubwa kupitia Magufuli kuliko kupitia Pinda au Bilali.

Pia ukiangaia utendaji wao katika nafasi zao leo, are they Presidential materials? To me NO

Rais must be a tough and aggressive guy like Magufuli and not too soft character.

Kama kwenye Chama chao wanachaguana kwa mizengwe unategemea nini kwenye uchaguzi wa vya vingine dhidi ya Chama chao.Wakati wameshikilia vyombo vyote vya dola hapo lazima mchezo mchafu ni dhahiri,kwa hiyo hoja ya kuwa fulani hasingeuzika na CCM kupata ushindi halipo.
Kama ulikuwa unafuatilia chaguzi za rais wa Zanzibar tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi bila shaka unajua ninachokimaanisha hapo juu.
Juzi juzi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa kijana wangu alikuwa mmojawapo wa wasimamizi kwenye kituo cha kupigia kura,kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza waliitwa pembeni na viongozi wa CCM wakapewa maelekezo kuwa endapo mgombea wa chama cha upinzani atashinda wasitangaze matokeo bali wawapigie simu hili waje wawape maelekezo na walikuwa wamekaa karibu na kituo hicho,lakini matokeo yalikuja in favour of CCM.
Hapo nikawa najiuliza kama hata kwenye chaguzi za serikali za mitaa jamaa wanataka kuchakachua matokeo je tukienda kwenye uchaguzi mkuu itakuwaje?.
 
......kuhusiana na watendaji hawa kuishia kwenye kamati ya maadili inatupeleka marekani, ambako kama vile nakumbuka iliwahi tokea ziku za karibuni kiongozi mmoja aliondoka kwa office baada ya muda wake wa miaka nadhani 6. Alipoambiwa ampendekeze mtu wa kuchukua office, akampendeleza mtu wa nje ya ofice a akamuacha yule makamu wake wa miaka 6. Media ilipojaribu kumfuatilia akajibu "hakuwahi kumpinga"....seeeee
 
......kuhusiana na watendaji hawa kuishia kwenye kamati ya maadili inatupeleka marekani, ambako kama vile nakumbuka iliwahi tokea ziku za karibuni kiongozi mmoja aliondoka kwa office baada ya muda wake wa miaka nadhani 6. Alipoambiwa ampendekeze mtu wa kuchukua office, akampendeleza mtu wa nje ya ofice a akamuacha yule makamu wake wa miaka 6. Media ilipojaribu kumfuatilia akajibu "hakuwahi kumpinga"....seeeee
Inawezekana upole, utii, hewala kwa kila kitu kwa boss wao na kushindwa kumhoji boss wao kulitafsiliwa kama udhaifu wa wasaidizi hawa wakuu. Maana wasaidizi hawa wakuu ndo waliopaswa kuhoji kuyumba kwa shilingi na uchumi, safari nyingi mno za rais, kuongezeka kwa rushwa, kupitishwa kwa miswada mibovu, kuchakachuliwa kwa rasimu ya katiba, n.k. hawa walipaswa kumshauri boss wao kikamilifu lakini hawakufanya hivyo kumbe ikatafsiriwa kama ni wadhaifu wakubwa wasiofaa kuwa kuliongoza taifa.
 
Rais Kikwete yupo ziarani tena, safari hii amekwenda Australia.

Anayekaimu urais ni Makamu wa rais wa JMT, Dk Mohamed Bilal.

Bilal huyu huyu ambaye Kamati ya Maadili ya CCM ilimkata hata asiingie tano bora ya kugombea urais, na Kamati Kuu ikabariki.

Kweli hakuwa na sifa?

Au ndio ilikuwa kumsafishia mtu njia?

Tafakari.
 
Back
Top Bottom