Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

Pinda, Bilali na Sitta jipimeni wenyewe

Mleta hoja nakubaliana na wewe 100 %!!

Kwa kweli hii ni aibu kwa nchi pia. Haiwezekani viongozi wakuu wa nchi, wachujwe na kamati ya maadili halafu tuendelee business as usual. Only in Tanzania. Ingeonekana ni kawaida kama wangeshindwa kwa kura ila hii ya kupigwa chini na kamati ya maadili is real questionable!! Jaji Mkuu mstaafu, Spika Mstaafu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wapigwa chini na kamati ya maadili!!? Ni AIBU kubwa. Hii imetupa picha halisi ya Viongozi wetu kuwa siyo waadilifu!! Ingekuwa kwa wenzetu, naamini Makamu na Waziri Mkuu wangeshaamua kuachia ngazi by now .... ila Bongo, hatoki mtu hapa mpaka utolewe!!

Kwa sasa Rais yuko nje ya nchi.... kwa nini kawaachia watu asiowaamini au wasio na maadili!!? Kwa sasa inabidi awachie watu kama akina Magufuli, January au Asha Rose ndiyo wa-act ikiwa nje ya nchi.

Kwa kweli hawa watu inabidi wajipime tena kama kweli bado wanastahili kurudi walau bungeni!!

Na hii ndiyo complaint ya Kingunge kuwa taratibu zilikiukwa. Huyu Magufuli wala hakuwa anatarajia kufikia hatua hiyo. Je, atakuwa sasa anasiadiwa rais mstaafu endapo atachaguliwa kuwa rais? Jamaa hakutegemea kabisa na wala hakujiandaa for sucj a big post.
 
Na wakatwe tu kwasabbau hatuna chakufanya
ningekua nauwezo ninge mwajibisha
 
sita alikua anajazijazia tu list lakini likua asitoboe hata top 30,
 
nani kakuambia kuwa hao waliishia kamati ya maadili? kama hujui ni vizuri ukauliza kuliko kukurupuka. ukiacha akina lowasa walioondolewa na kamati ya maadili wengine wote walifika kwenye central committee. huko ndo zilikopigwa kura na kupatikana tano bora iliyoenda kwenye NEC.
kavulata
 
Last edited by a moderator:
Ni aibu sana kwa mtendaji mkuu wa serikali kama waziri mkuu kuonekana sio muadilifu sasa sijui ushauri wake ulikuwa unachukuliwaje huko ikulu.
 
nani kakuambia kuwa hao waliishia kamati ya maadili? kama hujui ni vizuri ukauliza kuliko kukurupuka. ukiacha akina lowasa walioondolewa na kamati ya maadili wengine wote walifika kwenye central committee. huko ndo zilikopigwa kura na kupatikana tano bora iliyoenda kwenye NEC.
kavulata

Walishia wapi?
 
Last edited by a moderator:
Nilifikiri ungempongeza kwa kuwa mkweli kwamba alikuwa amejitwisha mizigo ndio maana hata shilingi wanaipeleka mbio shule zikiwa zinaishiwa chakula
 
nani kakuambia kuwa hao waliishia kamati ya maadili? kama hujui ni vizuri ukauliza kuliko kukurupuka. ukiacha akina lowasa walioondolewa na kamati ya maadili wengine wote walifika kwenye central committee. huko ndo zilikopigwa kura na kupatikana tano bora iliyoenda kwenye NEC.
kavulata
Kamati kuu ina wajumbe wangapi na ni akina nani hao ili tupime uadilifu wao, dhamira zao na shughuli zao za kila siku nje na ndani ya chama katika taifa hili. Maana tunavyojua sisi kulikuwa na CCM Mkapa/Mangula/Chiligati na CCM Kikwete/Yusuf Makamba/Kinana/Nape. Je wajumbe wa CC hii wengi wao ni ma pro CCM ipi? Hapo ndo tutakapojua ni kwanini Membe, January, Asha, Magufuli na Amina walipenya kwa ulaini.
 
kavulata

Ni kweli kabisa ,hatumkatai magufuli,lakini kitendo cha Kamati kuu kumueka Makamba 5 bora na kumuacha Bilal,Pinda na Mwakyembe ni udhalilishaji wa kupitiliza.
 
Last edited by a moderator:
mimi sitilii shaka huo uteuzi wa Mgufuli Buludoza ilaa kwa haraka haraka nasikia tume ya maadili ilitoa majina matano ambayo Membe na January hawakuwemo so ni dhahiri kabisa huyu anaekalia kiti alileta watu wake hao na kutoa wengine mwenye nyepesi hii atujuze najua kimbisa mama sofia simba na nchimbi hiyo orodha watakua nayo hebu tupeni tupepese tu pamoja na kwamba haitatusaidia NA HII NDIO DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA, KIDUMU CHAMA
 
zile za kuchukua form wengi zilikua mbinu tu za kumkata bwana EL,Isingekua hivyo angewasumbua.kwahiyo ataonekana kua mbona wenzake hawalalamiki ila yeye tu!! wazee wote waliokaa kimya wanaju kinachoendelea.
 
wajipime nini. wakati pesa za kutosha wameshavuna
 
Kusema kweli mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia ccm mwaka huu ulikuwa batili na ulikiuka kanuni na katiba ya ccm. Mchakato ulitawaliwa na mizengwe na ubabe usiokuwa na mantiki yoyote.
 
wajipime nini. wakati pesa za kutosha wameshavuna

pesa nini bana! imeandikwa kuwa "binadamu hataishi kwa mkate tu" bali atahitaji mambo mengine kama vile amani, upendo, kuheshimiwa, kuthaminiwa, n.k. Pesa haiwezi kununua kila kitu maishani, wako wenye hela nyingi lakini hawana amani nazo kabisa, lakini wako wenye hela za kawaida na furaha teleeeee...., Pinda na Bilali walikuwa na pesa zao za kuwatosha hata kabla hawajashika nafasi walizokuwa nazo, wanachotafuta pale walipo sio hela ya kula bali heshima na kuwatumikia watu katika ngazi za juu, hivyo kuwadhalilisha ni kuwafanya wakose raha kwa maisha yao yote yaliyobaki.
 
General wa jeshi; mwanasheria imara jeshini; jaji mkuu na Padre Agustino John Ramadhani kweli hana maadili hata ashindwe kupenyeza kwenye kamati ya maadili. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
 
jamani lazima tutambue ili kuwa rais ni zaidi ya uadilifu tu.
Ni kweli uadiiifu wa pinda, bilali na hao wengine hauna shaka. Lakini je kama ccm ikiwasimamisha hao nini nafasi yao ya ushindi?

Kwa mtazamo wangu ccm ina nafasi kubwa kupitia magufuli kuliko kupitia pinda au bilali.

Pia ukiangaia utendaji wao katika nafasi zao leo, are they presidential materials? To me no

rais must be a tough and aggressive guy like magufuli and not too soft character.
kwahiyo chama ni mtu??
 
Ni kweli utawala wa JK umekuwa wa kiujanja ujanja,fitina, udugu, chuki na makundi. Hili jambo siyo siri ndivyo alivyoingia pia kwenye madaraka ya urais. Watendaji wake wamekuwa hawamwamini kwa jambo lolote, hata wanapotaka kfanya maamuzi yoyote hata kwenye nafasi walizo na dhamananazo huhofia bosi wao atawaonaje. Hili pia limejidhihirisha pale waziri anaposema lingekuwa langu ningeamua hivi, lakini kwa sababu kuna mkubwa wangu siwezi kuamua. Tafsiri rahisi ni kuwa maamuzi hayapo kiserikali yako more Personal kuliko kuwa oficialised.
Lakini wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa mwaka 2015 wamemthibitishia JK kuwa CCM si chama cha wajanjajanja kwa kumchagua Magufuli kwa kuangalia umahiri utendaji kazi wake.
Ni kama uchaguzi wa mwaka 1985 wakati Nyerere alimwandaa Salim Ahamed Salim kuwa mgombea wa rais kwa kuangalia uchapakazi wake akisindikizwa na mtu aliyedhani dhaifu Ali Hassan Mwinyi, lakini wajumbe wakamchagua Ali Hassan Mwinyi kwa kuangalia Upemba na Uunguja. Wakakataa kuwa rubber stamp wa Mwalimu. JK alimtaka Bernad Membe au Rose Migiro lakini akitaka asindikizwe na John Pombe Magufuli, wajumbe wa Kamati kuu na Mkutano Mkuu wamekataa kuburuzwa na JK wakamchagua John Pombe Magufuli.
Kingunge nimemzungumzia sana katika uzi mwingine nisingependa kurudia lakini itoshe kuwa maoni yake hayako huru kwa sababu yupo kundi la Lowasa hivyo anakosa uhalali wa kuwa hakimu katika shauri alilo na maslahi nalo.
 
Rais tuliyenae kwa sasa hakusoma alama za nyakati kwa wakati stahili. Safari zilimzidia na alikuwa anasubiri funika kombe mwanaharamu apite lakini wazee wakataka kumng'oa kwenye uchair ndipo mkuu benny na wazee wenzake wakaona bora wabadili upepo
 
nguvu ya lowasa. nguvu ya lowasa. mijadala yoote hii ni kwa sababu ya nguvu ya lowasa. twiter, facebook, instagram habari zote ni nguvu ya lowasa. ifike mahali tukubali lowasa ananguvu.
 
Back
Top Bottom