Pinda ashindwa kupelekea madaktari wanajeshi ktk hospitali za DSM

ndo walimu wajue kua they are fighting a loosing battle, nadhan watapata fundisho zuri jinsi ya kudai haki zao kwani madaktari watalipwa wanachokitaka very soon, madktari nawaunga mkono waendeleee na uzi uleule wacjali watu eti wanapoteza maisha, kwa kudai better pay and good working condition watu kufa is acceptable afterall human being inevitably die!
 
Wote mnamshambulia Mgaya na TUCTA hapa pasipo kujua matakwa ya sheria yapoje. Mgaya aliwashauri madaktari wafate matakwa ya sheria. Kosa lake lipo wapi? Ukiachilia mbali sheria aliyoisema Mgaya, pia wamevunja Employment and Labour Relations Act, No. 6, 2004 ambayo imetoa utaratibu endapo italazimika wafanyakazi wa sekta ya afya watalazimika kugoma. Tukimshambulia Mgaya tunaonesha umbumbumbu wetu katika sheria za kazi.
 
huu moto kabla ya kulipuka ulianza kutoa moshi. Je, huyu Nikola Hausi Mgwaya alikuwa hakuona moshi ulivyokuwa unatoka hadi asubiri aone msitu unateketea kwa moto ndipo ajue kuna sheria ya mwaka 2003???

Kwa nini hakufanya hayohiyo NEGOTATION kabla ya mambo kufika hapa?

MNAFIKI :spy: MKUBWA ANATAFUTA UMAARUFU TU!!!!

MADAKTARI INGAWA WANANJI TUNAUMIA LAKINI NI HERI, TUNAKUBALI YOTE KWANI LEO HII TANZANIA TUPO HURU BAADA YA KUMUONDOA RICHARD TURNBUL NA WENZAKE :hat:.

Ni kwamba mababu zetu walikufa ili haki na uhuru upatikane!!!!!

Kwa msimamo wa Viongozi wetu wa nji hii inaonyesha kuwa Haki haipatikani kwa kukaa mezani pale Diamond Jubilee kama mnakunywa Bia, bali ni kwa kutumia nguvu kama wao viongozi LEGELEGE wanavyotumia DOLA

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kama kweli Waziri Mkuu aliwaita, walipaswa kwenda kumsikiliza, kama wasingeridhika na maelezo yake, wangelea na mgomo kama kawaida. Lakini kama hawakwenda, inatia shaka.
 
kila mmoja auguliwe na ndg yake mmoja2 wa karibu ambaye yupo mahututi tuone kama mtashabikia madaktari kugoma. Mgogoro wa madaktari na serikali unazungumzika lakini utekerezaji wake unahatua zake, sasa tusubiri huo mchakato umalizike au madaktari tuwasihi warejee kutoa huduma kwanza kuokoa maisha ya watu?
 
Pinda anampango wa kumleta babu wa Loliondo na waganga wa jadi kutoka Sumbawanga baada ya kugundua madaktari wa jeshini hawatoshi
 
kila mmoja auguliwe na ndg yake mmoja2 wa karibu ambaye yupo mahututi tuone kama mtashabikia madaktari kugoma. Mgogoro wa madaktari na serikali unazungumzika lakini utekerezaji wake unahatua zake, sasa tusubiri huo mchakato umalizike au madaktari tuwasihi warejee kutoa huduma kwanza kuokoa maisha ya watu?

Sisi sote si kwamba tunafurahia na hii hatua tulipofikia. Lakini tatizo Viongozi wetu LEGELEGE wanalichukulia jambo hili KISIASA zaidi badala ya kuweka Ubinadamu.

Madai ya Madaktari ni sahihi kabisa ambayo pia ni kwa manufaa yetu, kwani huduma katika Hospitali zetu zikiboreshwa ni nani anayefaidika kama si mimi na wewe mlalahoi mwenzangu???

hawa viongozi legelege wao wakiumwa wanapanda ndege sisi tunapanda daladala, sasa tunataka watuboreshee huduma zetu watu wa kupanda daladala kwenda Muhimbili / mwananyamala!!!!!!

ndio maana wao hata malaria wanapanda ndege kutibiwa nje kwasababu wanajua huduma za hapa njini ni mbovu, je nani wa kuziboresha????

Kwani huko India au London hospitali zao zilishushwa toka mbinguni na kuwana vifaa pamoja na mazingira mazuri au waliziboresha????

TUSIWEKE SIASA KATIKA JAMBO HILI WENGINE HATUNA HATA USHABIKI WA SIASA TUNAONGELEA UTANZANIA

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
katika kuthibitisha ukosefu wa umakini ndani ya serikali, mchana huu mwandishi wa Clouds Redio ameripoti kuwa wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili hawakupata huduma yeyote ikiwemo kushuhudia zaidi ya ambulance 7 zikileta wagonjwa toka hospitali mbali mbali na kulazimika kuondoka na wagonjwa wao kutokana na kukosekana kwa huduma katika hospitali hiyo. Hii inashiria kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshinde kutekeleza ahadi yake kupelekea madajatari toka JWTZ na JKt akama alivyoahidi jana wakati akitoa kauli za dharau dhidi ya madakatari wanaogoma.

My take: Tukumbuke kiini cha mgogoro huu ni madakatari walioko mafunzoni yaani interns katika hospitali ya Muhimbili kunyanyaswa na uongozi wa Wizara ya Afya hivyo kutakiwa Waziri Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa kuondolewa mara moja kwa kuishawishi serikalim kuchukua hatua za kionevu dhidi ya madakatari hao waliokuw akatika mafunzo. Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe katika kuwalinda wazembe watatu?

Ni imani yangu watatu hao wakiondolea hata leo madakatari walioko katika mgomo watakuwa tayari kuzungumza na serikali kuhusu madaia yao.

Soma agizo lake between line kwa nia ya kuelewa na ondoa ushabiki utalielewa.

Alitoa siku moja kuwataka warejee maramoja maofisini kwao na kama watashindwa kufanya hivyo basi watakuwa wamejifukuza kazi wenyewe na wao sasa wataleta madaktari toka kwenye vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

Sasa utaona hakupaswa kuleta jana ma doctor kutoka jeshini ila leo ndio tunasikilizia.

Tuombe kheir itawale shari mambo yaende vizuri huko tanganyika

Wote mnamshambulia Mgaya na TUCTA hapa pasipo kujua matakwa ya sheria yapoje. Mgaya aliwashauri madaktari wafate matakwa ya sheria. Kosa lake lipo wapi? Ukiachilia mbali sheria aliyoisema Mgaya, pia wamevunja Employment and Labour Relations Act, No. 6, 2004 ambayo imetoa utaratibu endapo italazimika wafanyakazi wa sekta ya afya watalazimika kugoma. Tukimshambulia Mgaya tunaonesha umbumbumbu wetu katika sheria za kazi.

Dumb ass, hizo sheria za ajira unazotaka madaktari wazifuate serikali yenyewe inazifuata? Msijazwe upumbavu huo wa kuamini kuwa serikali peke yake ndiyo inayopaswa kusikilizwa na si raia.
Wewe, Mgaya na serikali yenu wote ******* nyie.
 
Imepatikana tarifa ya uhakika kutoka kwa rafiki angu ambaye baba yake ni daktari bingwa na ana miliki hosptali yake hapa mjini kwamba,wao madaktari bingwa ndio wanachochea mgomo huu kwani wengi wao wana hospitali zao binafsi ambapo wamekuwa wakiondoka kwa kificho/siri kwenda kwenye hospitali zao lakini kwa wakati huu wa mgomo wanakwenda wazi wazi.

Wengi tutakubaliana kwamba wenye hopitali binafsi wapo kwenye mavuno kwa sasa kutokana na wagonjwa kumiminika huko.

Intern Docters hawajui siri hii na watakapofahamu watakuwa wameumia wao pamoja na wagonjwa wanaokosa huduma.

Rafiki angu anasema kuwa baba yake kwa sasa yupo busy kwenye hospitali yake na anajivunia kuwa kwa sasa mavuno yapo juu.

Maduka ya dawa pia ni ya madaktari,nao wananufaika kwa kiasi kikubwa na mgomo huu kwani nao hutoa ushauri kutokana na maelezo ya mgonjwa na hali aliyponayo.

Nawasilisha.
 
Hivi madaktari wa jeshi wakienda kutoa huduma kwenye hospitali za serikali kule kwenye hospitali za jeshi nani atakuwa anatoa huduma?

Manesi wa Muhimbili wamewakataa wanasema experience waliyoipata mwaka 2006 ya kufanya kazi nao hawataki itokee tena.Wanawataka Madaktari wao vinginevyo hawatafanya kazi,sasa pengine hao manajeshi watakwenda Amana.
 
Dumb ass, hizo sheria za ajira unazotaka madaktari wazifuate serikali yenyewe inazifuata? Msijazwe upumbavu huo wa kuamini kuwa serikali peke yake ndiyo inayopaswa kusikilizwa na si raia.
Wewe, Mgaya na serikali yenu wote ******* nyie.

matusi yanaonesha kipimo chako cha fikra!
 
Madaktari bingwa wana hospitali zao binafsi na huko ndiko kuna maslahi yao zaidi kwa mgomo huu wameneemeka wanaendelea na kazi binafsi.
 
Madaktari bingwa ni moja ya eneo lenye matatizo makubwa hawa jamaa ubingwa wao utaukuta kwenye hospitali zao binafsi. Kila utakapofika hospitali utaambiwa wako busy.
 
Team ya maafande wa JWTZ yatua muhimbili kitengo cha dharura ilikuto huduma kwa wagonjwa wanaofikishwa katika kitengo hicho na inasemekana kua katika madakitari hao kumi na moja ni medical doctors na saba ni specialist doctors.
Hawa madakitari ni madakitari ambao walikua hawapractise medical kwa muda mrefu na dio maana wauguzi wanaona kua watapata shida kufanya nao kazi na kujikuta wanafanya kkazi mara mbili.

Hapa ndio tutakuja kusikia mchangayiko wa matibabu, Serikali lazima ikubari kumaliza hili tatizo la madakitari la sivyo tutazidi kwenda pabaya.
 
Wote mnamshambulia Mgaya na TUCTA hapa pasipo kujua matakwa ya sheria yapoje. Mgaya aliwashauri madaktari wafate matakwa ya sheria. Kosa lake lipo wapi? Ukiachilia mbali sheria aliyoisema Mgaya, pia wamevunja Employment and Labour Relations Act, No. 6, 2004 ambayo imetoa utaratibu endapo italazimika wafanyakazi wa sekta ya afya watalazimika kugoma. Tukimshambulia Mgaya tunaonesha umbumbumbu wetu katika sheria za kazi.

Hiyo sheria anayoisema mbona amekuwa anaitumia katika kudai maslahi ya watumishi lakini mpaka sasa haijaweza kutatua matatizo ya watumishi??kama yeye alifuata sheria serikali ilivunja sheria kwa kuvunja migomo iliyokuwa halali (kumbuka hukumu ya jumapili usiku kuhusu mgomo wa walimu),elewa kuwa nchi hii sheria zilishawekwa makabatini,sheria zinafuatwa tu kama zinawasaidia wao kama sheria zingekuwa zinafuatwa hata haya tunayopingana sasa yasingekuwepo,ukiona watu wanaamua kuvunja sheria jua kuna matatizo sehemu fulani.
 
Namkubali Pinda alichotuahidi watanzania ndio hicho nina ndugu yangu mgonjwa muhimbili pengine kufikakwa JWTZ atapona
 
Back
Top Bottom