Pinda amvaa Lowassa: "Kuvunja Baraza" yataka moyo!

Wakati hayo yakitokea nurse anakatwa mshahara wake ili kulipia uniform yake ya kazini!!nchi hii!
 
Hapo kwenye red: wabunge wengi wa ccm walitumia muda wao wakati wa kujadili bajeti ya office ya waziri mkuu kwa kuishambulia CHADEMA na mipasho! Wakati wa hitimisho ndio wanashtuka na kuanza kutoa hoja za wananchi! huku ni kupoteza muda.
Mkuu ile kipande ya senkyu siioni ningekugongea. Umenikuna si haba! Senkyu bai ze wei.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Suala hilo lipo kwenye kitabu cha serikali cha matumizi volume II. VOTE 25 ofisi ya waziri mkuu ,chini ya kifungu kinachoitwa programme 10 adminstration and General kifungu kidogo cha 230100 ambacho kimeandikwa "routine maintanance and repair of roads and bridges" na zimetengwa shilingi milioni mbili za kitanzania .
Duh! Mkuu nimekukubali jinsi ulivyoiweka.Uko bungeni nini? Coz niko na hicho kitabu hapa yani umeweka maelezo kama ilivyo.Hongera Mkuu kwa jitahada za kuwa na data na kuzirusha fasta!
 
Pinda naona kamtolea uvivu...
Hapo ndipo umuhimu wa Lowassa kugoma kutoka peke yake wakati ule unaonekana. Makosa yalifanywa na Baraza la Mawaziri, akajifanya shujaa kumlinda swahiba wake! Angegoma si Serikali ingeanguka na tungekuwa na watu kibao "behind bars"?Mkuu, mi naona usanii plus plus tu hapo!
 
..uamuzi mgumu ni kama Raisi kwenda kuwapigia kampeni mafisadi.

..ni uamuzi mgumu lakini usiokuwa na maslahi kwa nchi.
 
Uamuzi mguma mwingine ni wa raisi kufanya ziara nyingi za nje ya nchi kuliko za ndani hadi kufikia ziara 312 mpaka sasa.
 
ofcourse hilo lilikuwa dongo kwa lowassa lakini nionavyo mimi aliyefanya uamuzi mgumu pale ni lowassa ambaye aliamua kujihudhuru. Baada ya lowassa kujiudhuru hakukuwa na namna nyingine zaidi ya baraza zima la mawaziri kuvunjwa kwa kuwa ndivyo taratibu zilivyo.
 
watanzania tumekuwa wajinga sana kupita maelezo hivi kweli diwani na Bsc. student wanakuwa na miashyahara ianayofunana? kama ni hivyo hakuna haja ya kusoma nikwenda kwenye siasa tu maana madiwani wetu wengi ni form fail na darasa la saba lakini cha ajabu wasomi wengi tena wachuo kikuu tunaliupwa laki tatu mpaki tano sijajua hao wabunge wanaakili timamu au la?
 
Maamuzi magumu yalenge kwenye Kuboresha Maisha ya Mtanzania!
Mfano wa maamuzi magumu ni Kuuza Magari yote ya Kifahari ya Yanayomilikiwa na Serikali na Pesa zake kuzielekeza kwenye Miradi na Uhuduma za Kijamii Vijijini ambako zimedorora,Kufuta Mikataba yote ya Madini katika migodi inayozalisha lakini fedha zinapaa.Kuwa na Baraza Dogo la Mawaziri n.k
Ile ishu ya Lowassa 2008 mbona ilikuwa ni kutekeleza Utaratibu!Aliyefanya maamuzi magumu ni Lowasa kuachia UTAMU,labda iwe alilazimishwa kusema anajiuzulu ndio hapo wote waonekane walifanya maamuzi magumu!
 
Lowasa amewashtua nao wameshtuka. Sasa kwa sababu Pinda amemtaja EL ngoja tusikie mashambulizi ya EL. atakuja na stanturi ya Richmonduli jinsi walivyogawana tender na maslahi kuwaangamiza wananchi. Ataeleza EPA walivyoitumia kumwingiza mkuu mjengoni 2005. Ataeleza mtandao walivyofaidika na fedha za minara mapacha bot. Na ataeleza usanii wa miradi ya umeme unavyinufaisha CCM.
 
Pinda ni waziri mkuu ambaye hana maamuzi yyt yale magumu,huwezi linganisha Lowassa na Pinda
 
milion 2 kwa ajili ya kutengeneza madaraja mabovu ndani ya makazi ya waziri mkuu!
 
Jana nimemsikiliza PM Pinda akiorodhesha Idadi ya Maamuzi aliyoita ni "magumu" wakati akihitimisha majumuisho ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu! Akizungumzia Hoja ya Maamuzi Magumu iliyotolewa na Waziri Mkuu "Mjiuzulu" (sio mstaafu kama ilivyozoeleka) Bw Edward Lowassa Pinda alidai kwamba mojawapo ya "maamuzi magumu" Serikali ya Awamu ya Nne iliyowahi kufanya ni pamoja na:1. Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata,2. Kuendelea na ujenzi wa UDOM ulioanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu,3. Kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya,4.... nk.Mimi sioni "ugumu" wowote katika maamuzi ya mambo hayo hapo juu kwa sababu ni sehemu ya mipango ya kawaida Serikalini! Mimi nionavyo kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne ni Serikali dhaifu mno, kila maamuzi, hata kama ni ya kawaida inaonekana ni magumu.Tujadili!
 
Nami nimemshangaa sana Pinda ameorodhesha wajibu na kazi ya serikali sio maamuzi magumu kama ya awamu ya kwanza .....ulanguzi na hata azimio la arusha!!yeye anasema kujenga barabara ni maamuzi magumu??kazi ipo nini wajibu wao kutekeleza ilani yao wenyewe???? Pinda kazi ipo!!
 
Back
Top Bottom