Pinda amethibitisha ndani ya bongo wote hatuko sawa mbele ya sheria. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amethibitisha ndani ya bongo wote hatuko sawa mbele ya sheria.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jul 3, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kulingana na katiba yetu mamlaka ya juu kabisa ya kuamua iwapo mtuhumiwa wa kosa lajinai afikishwe mahakamani hao la, ni Mkurugenzi wa mashitaka; lakini hivi majuzi wakati Pinda anahitimisha mjadala wa makisio ya ofisi yake alisema JK alifanya maamuzi magumu kwa kuridhia baadhi ya mawaziri wa awamu ya tatu kufikishwa mahakamani. Usemi huo ulinikumbusha sakata la fedha za EPA ambapo JK alisema kama watuhumiwa hao watarejesha fedha walizokwapua katika muda aliowapa hawatashitakiwa. Wakati huo wengi wetu tulijihuliza hayo madaraka JK ameyapata wapi! Kwani kwa mujibu wa katiba rais anayo madaraka ya kumsamehe mtu ambaye tayari amewekwa hatiani lakini siyo kabla. Katika mambo mengi yanayokwenda hovyo nchini mwetu ni pamoja na hii tabia ya watawala ya kujichukulia sheria mikononi mwao. Ifike mahali watanzania wote bila kujali vyama au itikadi zetu, tuseme kwa nguvu na kauli moja ya kuwa IMETOSHA.
   
Loading...