Duu Waziri mkuu sikuzote amekuwa ni wakuficha madhaifu ya Maraisi wetu. Waziri mkuu wetu hana madaraka ya kisheria na kikatiba ya kuwawajibisha viongozi walioteuliwa na raisi. Hana uwezo hata wa kumsimamisha kazi mkuu wa wilaya. Lakini wakati unapofika inabidi awajibike hata kwa makosa ya watu asioweza kuwawajibisha. Kuna haja ya kufuta cheo hichi kwenye katiba pendekezwa au kumpa madaraka waziri mkuu ya kuwafukuza watendaji dhaifu. BILA hivyo lawama zitaendelea kuelekezwa kwa mawaziri wakuu ambao kwangu nawaona kama wanaficha uchafu na udhaifu wa mfumo raisi. Mwangalie kawawa enzi zile, mwangalie malecela enzi zile, mwangalie msuya enzi zile ,mwangalie Sumaye Enzi zile ,Mwangalie lowassa enzi zile, mwangalie Pinda sasa. Tatizo ni mfumo raisi tulionao. Kwaheri Pinda laikini tushirikiane kufuta cheo hiki au kuongeza madaraka ya nafasi ya waziri mkuu aweze kuwafukuza hata mawaziri wasiotekeleza maagizo yake.