PINDA aingia rasmi mbio za urais CCM?

PINDA aingia rasmi mbio za urais CCM?

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
Japokuwa ni wazi kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa ni Edward Lowassa kutokana na nguvu za kisiasa alizonazo ndani ya CCM kwa sasa, kitisho kipya kimeingia kwa kasi dhidi ya kambi hiyo baada ya mikakati ya Mizengo Pinda kutaka kugombea urais 2015 kuanza kuwekwa hadharani na baadhi ya watu hususani mawaziri wa serikali ya Kikwete.

Jambo hili limekuja baada ya Pinda kuwa na ziara za mara kwa mara za kichama mikoa mbalimbali na kufanya vikao vya ndani vya CCM na kiserikali visivyo na Agenda za wazi na huku pia akiendesha harambee kadhaa kwenye taasisi mbalimbali za kijamii na kikanisa kama vile ambavyo wanasiasa wengine wa CCM wanaowania urais wamekuwa wakifanya kila mara.

Na taarifa za karibuni kabisa zinasema kambi ya Pinda inayoongozwa na mawaziri kadhaa imepanga kuzivuta kambi ya Membe na Sitta ili kuungana na Pinda ili kupambana na Lowassa.

Mkakati huu unapangwa chini ya agenda ya kuhakikisha rais ajaye ni lazima atoke kwenye baraza la mawaziri la sasa kwa lengo la kulinda mfumo na maslahi ya Kikwete mara atakapo achia madaraka ya urais.
Huu ni utamaduni umekuwepo kuanzia kwa Nyerere, Mwinyi na Mkapa, na unasisitizwa kuendelezwa pia kwa Kikwete.

Kuna tetesi pia, hata kelele za kutaka Pinda ashtakiwe mahakamani kwa kauli yake ya ''Watapigwa tu, tena nasema wapigwe'' huenda pia zikazidi kuchochewa chini kwa chini na wafuasi wa kambi ya Lowassa ili kuvunja nguvu za kisiasa za Pinda kuelekea 2015.
Mpaka sasa limeanza kupelekea na litazidi kupelekea 'Wateule' wa Pinda wazidi kujitokeza hadharani kuanza kumtetea kwa hali na mali ili asishtakiwe mahakamani.

Swali, Pinda ameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha urais CCM 2015?
 
Kama u PM tu analia bungeni na kukurupuka kwenye maamuzi yanayoikiuka katiba aliyoapa atailinda, je akiwa rais itakuwa je? Ajifikirie mara mbilimbili kwani urais si kamasi kila mtu anazo
 
Na hizo ARV itakuwaje sasa maana miaka 10 ni mingi sana kuishi magogoni kwa kutegemea booster...

Akiingia Ikulu atasema Wauliwe kabisa na sio Wapigwe ya sasa
 
Pinda hata ukuu wa wilaya hataweza sembuse uraisi?CCM wakimsimamisha chadema tutaanza kupanga baraza la mawaziri na safu nzima ya uongozi wala hakuna haja ya kampeni!
 
TanganyikaTANU, tunataka Rais anaeyajua matatizo ya watu wetu na yuko tayari kupambana nayo hata kama angekuwa ni Mheshimiwa Pinda. Hizo sababu ulizotoa hapo juu ni mtazamo wako hafifu ndo umekufanya uulize swali jepesi kama hilo.
 
Last edited by a moderator:
Na hizo ARV itakuwaje sasa maana miaka 10 ni mingi sana kuishi magogoni kwa kutegemea booster...

Akiingia Ikulu atasema Wauliwe kabisa na sio Wapigwe ya sasa
Atapokea za mtangulizi wake!funny! kata mti panda mti!!
 
Pinda huyu anaekiuka utawala bora aje kuwa rais wa nchi? Ama kweli Ccm iko ICU kila kukucha mna jipya la chakubanga
 
Yaani magamba bora waweke jiwe kuliko mjinga kama huyu!
 
...udhaifu wa huyu m.k.w.e.r.e ndo amesababisha kila mtu ajione anaweza kuwa raisi,si ajabu kesho tukasikia Lusinde na Selukamba nao wanautaka uraisi...
 
haha haha haha pinda hyuhyu ambaye kila siku anatoa kauli zisizo na tija kwa taifa
 
Kwanza huyu mzee anasifa ya uo.ngo!sana!kufuga nyuki ok,ila uraisi?hapana
 
Hahaaaaa nimecheka sana..wakimuweka pinda cdm itapita bila hata kampeni....hahaaaaa ccm ni janga la dunia na sio taifa kama tunavyowaza.
 
Hizi kweli tetesi,pinda si nasikia kaapa akimaliza muda wake. hataki cheo chochote hata udiwani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ha ha ha we ulitaka kutuchangamsha asubuhi hii , ha ha ha....!!!!?
 
Japokuwa ni wazi kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa ni Edward Lowassa kutokana na nguvu za kisiasa alizonazo ndani ya CCM kwa sasa, kitisho kipya kimeingia kwa kasi dhidi ya kambi hiyo baada ya mikakati ya Mizengo Pinda kutaka kugombea urais 2015 kuanza kuwekwa hadharani na baadhi ya watu hususani mawaziri wa serikali ya Kikwete.

Jambo hili limekuja baada ya Pinda kuwa na ziara za mara kwa mara za kichama mikoa mbalimbali na kufanya vikao vya ndani vya CCM na kiserikali visivyo na Agenda za wazi na huku pia akiendesha harambee kadhaa kwenye taasisi mbalimbali za kijamii na kikanisa kama vile ambavyo wanasiasa wengine wa CCM wanaowania urais wamekuwa wakifanya kila mara.

Na taarifa za karibuni kabisa zinasema kambi ya Pinda inayoongozwa na mawaziri kadhaa imepanga kuzivuta kambi ya Membe na Sitta ili kuungana na Pinda ili kupambana na Lowassa.

Mkakati huu unapangwa chini ya agenda ya kuhakikisha rais ajaye ni lazima atoke kwenye baraza la mawaziri la sasa kwa lengo la kulinda mfumo na maslahi ya Kikwete mara atakapo achia madaraka ya urais.
Huu ni utamaduni umekuwepo kuanzia kwa Nyerere, Mwinyi na Mkapa, na unasisitizwa kuendelezwa pia kwa Kikwete.

Kuna tetesi pia, hata kelele za kutaka Pinda ashtakiwe mahakamani kwa kauli yake ya ''Watapigwa tu, tena nasema wapigwe'' huenda pia zikazidi kuchochewa chini kwa chini na wafuasi wa kambi ya Lowassa ili kuvunja nguvu za kisiasa za Pinda kuelekea 2015.
Mpaka sasa limeanza kupelekea na litazidi kupelekea 'Wateule' wa Pinda wazidi kujitokeza hadharani kuanza kumtetea kwa hali na mali ili asishtakiwe mahakamani.

Swali, Pinda ameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha urais CCM 2015?

Huyu Mh PM ni miaka saba sasa atakuwa anamaliza muda wake,ni nini hasa ambacho Watanzania watamkumbuka kwacho kwamba alikisimamia kikatekelezeka kwa ufanisi? Jibu ni hamna,

mtangulizi wake atakumbukwa kwa miaka miwili amejenga shule za Kata Tanzania nzima

Pinda hafai kwa Urais akafuge nyuki tu huko kwao
 
TanganyikaTANU, tunataka Rais anaeyajua matatizo ya watu wetu na yuko tayari kupambana nayo hata kama angekuwa ni Mheshimiwa Pinda. Hizo sababu ulizotoa hapo juu ni mtazamo wako hafifu ndo umekufanya uulize swali jepesi kama hilo.

Chizi Fureshi nadhani hujanielewa kabisa. Mimi nimeandika na kuripoti kile ambacho ninakiona na kinasemwa pasipo kuweka maoni yangu binafsi.
Mwisho nimeuliza swali ili kupata kujua zaidi, kwani mimi ni 'mwanaCCM' na nitahitajika kumpigia kampeni mgombea wa CCM 2015 hivyo ni bora nikahoji sasa.
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya ikatokea rais anakuwa huyu aliyePINDA kupindukia, basi tutakuwa tumechagua majanga.

Mzee wa LIWALO NA LIWE - watang'olewa kucha, meno na kutobolewa macho watu wengi sana watakokuwa wanayafichua mambo yake ambayo atakuwa ametudanganya maana Pinda anasifa pia ya kuwa MUONGO.

Pinda asiyeweza kuvumilia changamoto, atachoka na watu watauawa wengi watakaothubutu kudai haki zao kwa njia zozote iwe migomo au maandamano.

Nadhani hata bajeti kubwa ya serikali ataielekeza kwa jeshi la polisi ili watu wapigwe sana tu ktk kuwanyamazisha wasidai haki zao.
Atarudisha mfumo wa chama kimoja, maana vyama vya upinzani vitamnyima usingizi.
 
TanganyikaTANU, tunataka Rais anaeyajua matatizo ya watu wetu na yuko tayari kupambana nayo hata kama angekuwa ni Mheshimiwa Pinda. Hizo sababu ulizotoa hapo juu ni mtazamo wako hafifu ndo umekufanya uulize swali jepesi kama hilo.

Chizi Fureshi nadhani hujanielewa kabisa. Mimi nimeandika na kuripoti kile ambacho ninakiona na kinasemwa pasipo kuweka maoni yangu binafsi.
Mwisho nimeuliza swali ili kupata kujua zaidi, kwani mimi ni 'mwanaCCM' na nitahitajika kumpigia kampeni mgombea wa CCM 2015 hivyo ni bora nikahoji sasa.
 
Last edited by a moderator:
kama pinda ameweza kuwa pm basi hata nkamia anaweza kuchaguliwa na maccm kugombea urais..chezea mafisadi wa ccm wewe
 
Back
Top Bottom