japokuwa ni wazi kuwa mgombea urais wa ccm 2015 huenda akawa ni edward lowassa kutokana na nguvu za kisiasa alizonazo ndani ya ccm kwa sasa, kitisho kipya kimeingia kwa kasi dhidi ya kambi hiyo baada ya mikakati ya mizengo pinda kutaka kugombea urais 2015 kuanza kuwekwa hadharani na baadhi ya watu hususani mawaziri wa serikali ya kikwete.
Jambo hili limekuja baada ya pinda kuwa na ziara za mara kwa mara za kichama mikoa mbalimbali na kufanya vikao vya ndani vya ccm na kiserikali visivyo na agenda za wazi na huku pia akiendesha harambee kadhaa kwenye taasisi mbalimbali za kijamii na kikanisa kama vile ambavyo wanasiasa wengine wa ccm wanaowania urais wamekuwa wakifanya kila mara.
Na taarifa za karibuni kabisa zinasema kambi ya pinda inayoongozwa na mawaziri kadhaa imepanga kuzivuta kambi ya membe na sitta ili kuungana na pinda ili kupambana na lowassa.
Mkakati huu unapangwa chini ya agenda ya kuhakikisha rais ajaye ni lazima atoke kwenye baraza la mawaziri la sasa kwa lengo la kulinda mfumo na maslahi ya kikwete mara atakapo achia madaraka ya urais.
Huu ni utamaduni umekuwepo kuanzia kwa nyerere, mwinyi na mkapa, na unasisitizwa kuendelezwa pia kwa kikwete.
Kuna tetesi pia, hata kelele za kutaka pinda ashtakiwe mahakamani kwa kauli yake ya ''watapigwa tu, tena nasema wapigwe'' huenda pia zikazidi kuchochewa chini kwa chini na wafuasi wa kambi ya lowassa ili kuvunja nguvu za kisiasa za pinda kuelekea 2015.
Mpaka sasa limeanza kupelekea na litazidi kupelekea 'wateule' wa pinda wazidi kujitokeza hadharani kuanza kumtetea kwa hali na mali ili asishtakiwe mahakamani.
Swali, pinda ameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha urais ccm 2015?