Mzee wa Rula asante sana kwa comments zako lakini kuna mambo unaweza kufafanua ama kujifunza.
Kwa mfano,Inawezekana kabisa Magufuri akawa mmoja wa machaguo ya Kikwete, lakini ni vipi Magufuri atapitishwa na CCM akawa mgombea urais wakati hana nguvu ndani ya CCM ya sasa?
Hivi unajua hata Nyerere Chaguo lake la kwanza lilikuwa Dr.Salim Ahamed Salim na sio Ally Hassan Mwinyi lakini bado Nyerere alishindwa kumpitisha Salim!!
Hata Mkapa mwaka 2005 chaguo lake la kwanza lilikuwa Dr.Abdallah Kigoda na chaguo la pili lilikuwa Sumaye, lakini bado hakufanikiwa.
Sijui kama unakumbuka kisa cha Dr.Salimin Amour 2000 kutaka waziri kiongozi wake Dr.Bilal kuwa mrithi wake Zanzibar na bado lilishindikana.
Kitu ninachokijua ni kuwa siku zote rais anayeondoka madarakani anakuwa na chaguo lake 'rasmi' (Mara nyingi chaguo zaidi ya moja) hivyo hata Kikwete ana chaguo zaidi ya moja, Membe akiwa ni mmoja wao.
Kwani mpaka sasa tena katika hali mbaya ya kisiasa ndani ya CCM kuna haja au uwezekano wa suala la mgombea wa CCM 2015 kubaki kama 'Top Secret' kwa rais Kikwete na watu wake wachache?
Kwa vyovyote ilivyo kwa CCM mgombea wa urais 2015 ni lazima atakuwa amejiandaa vya kutosha kufanikishwa hilo na sio kwa kubebwa tu na kwa sasa Lowassa yuko mbele sana na njia pekee labda ya kumshinda Lowassa ni makundi makuu yote kuungana dhidi yake na kutumia mfumo wa sasa wa serikali kufanikisha hilo na hapo ndipo Pinda amesimamia kwa sasa.
Keep my words, soon utakuja kuniambia.