Pilau la njegere

Huo wali mbona Una rangi rangi au ndo Biriani?
Hii ni biriani kavu mpwa.
Japo mie si mpenzi wa biriani, ila nilipata mgeni ikabidi nimpikie maana anapenda sana biriani.

Ndipo nikampikia biriani kavu la pishori, kuku wa kukaanga, yai la kuchemsha, kachumbari ya kiswahili na bila kusahau ndizi pembeni.

Kufahamu na kujua kupika ni raha sana.
Hapa kisamvu cha karanga, sangara wa chukuchuku na kaugali kalaini.
 
Sure kujua kupika inasaidia sana
 
Siku nyingine utukaribishe
Sawa, kesho nitakukaribisha
Ila leo nimepika hivi

Nyama ya ng'ombe nimechanganya na viazi,
Mchicha pori (bwasi) nimechanganya na mgagani, mnafu na nyanyachungu.
Wali wa nazi.

Karibu sana.
Nina vyungu vya kupikia kama 20 hv, napenda sana kupikia vyungu.
Si unajua nina unyamwezi upande wa mama.
Wanyamwezi na vyungu ni kama uji na mgonjwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…