GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,895
- 6,667
Wakuu, sijaidharau, ila nimeshangazwa na bei yake. Nimeona mtandaoni pikipiki zinazouzwa Dar Es Salaam kwa bei ndogo sana. Zipo za kuanzia laki tano mpaka sh 1.8m. Zote ni used.
Sikuwahi kumiliki pikipiki. Lakini nilipoziona leo mtandaoni, kwa jinsi zilivyo bei "chee", nimepata wazo la kuinunua moja niipeleke shambani iwe inatumika kwa safari za "hapa" na "pale" zinazohusiana na shamba.
Shamba lipo mbali na zilipo huduma muhimu za kijamii. Linahudumiwa na "wafanyakazi" watatu. Usafiri wanaotumia kwa sasa huko shambani ni baiskeli.
Je! Hizo pikipiki za bei rahisi zinazouzwa Dar Es Salaam zinaweza zikafaa?
Japo zipo mpaka za laki tano, lakini ninafikiria niwachukulie ya kuanzia laki saba.
Haitapakizwa mizigo mizito, labda vitu vidogo vidogo kama unga kilo ishirini n.k.
Hizo zinazotangazwa mitandaoni zinafaa? Namaanisha hizo za bei rahisi ambapo zingine zinauzwa mpaka shilingi laki tano!
Zinafaa?