Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,150
Pikipiki kuwakaanga viongozi CCM Arusha
Mussa Juma, Arusha
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha, imependekeza zichukuliwe hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi waandamizi wa chama hicho wilaya ya Arusha kwa kumwalika Mwenyekiti Taifa, Rais Jakaya Kikwete, katika hafla ya kugawa pikipiki zilizo kuwa na utata.
Mapendekezo ya kamati hiyo, ambayo yalijadiliwa juzi usiku na Kamati ya Maadili ya CCM mkoa yalipelekwa jana kwa njia ya Fax kwenye sekretarieti ya chama Taifa.
Wajumbe kamati ya maadili waliokutana katika ofisi za CCM mkoa kujadili mapendekezo ya kamati ya siasa ya mkoa ni Katibu wa CCM mkoa , Mohamed Mbonde, mwenyekiti wake, Onesmo Nangole, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya, Katibu Uenezi na Itikadi mkoa, Loota Sanare na Mkuu wa Mkoa, Isdori Shirima pamoja na Samweli Urassa.
Habari za uhakika toka ndani ya kikao cha awali cha kamati ya siasa ya mkoa zimeeleza kwamba, licha ya viongozi wote wa kamati ya siasa ya chama wilayani Arusha, kuomba radhi kwa maandishi kwa kitendo hicho, kamati ya mkoa imependekeza kuwa wachukuliwe hatua.
Vikao vya kamati hiyo ya siasa na maadili vya CCM mkoa wa Arusha, vilikutana mfululizo kutokana na agizo la Rais Kikwete kwa viongozi wa chama wa mkoa kwamba, apewe taarifa juu ya tukio zima la kutakiwa kugawa pikipiki hizo ambazo
miongoni mwake zipo zilizotolewa na mfanyabiashara mmoja anayekabiliwa na kesi ya ufisadi wa mabilioni ya fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.
Habari toka ndani ya uongozi wa CCM mkoa, zimeeleza kuwa baada ya viongozi hao kuhojiwa, akiwemo Mbunge wa jimbo la Arusha, Felix Mrema, Mwenyekiti wa wilaya, Jubilate Kileo na wake Mohamed Nyawenga na viongozi wengine, ilibainika kulikuwa na kasoro katika mipango ya ugawaji wa pikipiki hizo.
Mjumbe mmoja wa kikao kilichowahoji viongozi hao, aliyeomba kutotajwa jina alifahamisha kuwa kitendo cha kumualika Rais Kikwete katika tukio hilo kilitafsiriwa kama kutaka kuhujumu jitihada zake za kupiga vita ufisadi.
Tuliwauliza kwamba, hata kama mfanyabiashara huyo alichangia pikipiki hizo mwaka 2007, ilikuwaje aalikwe ili apongezwe na rais wakati inajulikana kuwa ana kesi ya EPA mahakamani? alisema mjumbe huyo.
Katika kikao hicho, viongozi hao walibanwa sababu za kuzigawa pikipiki hizo wakati Rais Kikwete alisita na kuagiza
apewe taarifa, lakini walijitetea kuwa aliruhusu baada ya
kusema ameziona na wagawane wenyewe.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wa wilaya alisema awali ilipendekezwa kuwa mfanyabiashara huyo asiudhurie na badala yake atume mjumbe, lakini bila wao kutarajia siku ya tuko alifika yeye mwenyewe.
Hata sisi tulishangaa kumuona pale kwani tunajua anakesi. Lakini pia ikumbukwe kuwa alichangia pikipiki hizo mwaka 2007 na kama ulikuwepo siku ya tukio, nadhani hata wewe uliona hali ilivyokuwa, alisema kiongozi huyo.
Hata hivyo, wakati kamati ya Siasa ya CCM mkoa ikiwa imependekeza kuswachukuliwa hatua baadhi ya viongozi wa wilaya, tayari kumeibuka mgawanyiko mkubwa ndani ya chama mkoani.
Kundi moja la wana CCM wilayani Arusha linapinga kuchukuliwa hatua kwa viongozi wao kwa madai kuwa, pikipiki hizo zilitolewa kwa nia njema ya kukisaidia chama mwaka 2007 na kwamba, mtuhumiwa huyo wa EPA licha ya kuchangia pikipiki hizo kwa miaka mingi amekuwa akikisaida chama katika ngazi mbali mbali.