Pigo la kwanza kwa Simbachawene

Pigo la kwanza kwa Simbachawene

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,991
Reaction score
831,561
Kapokewa ofisini na vifo mfululizo. Ukiachana na vifo vya majanga asilia ya mvua nk. Kuna haya yaliyotokana na mwenendo wa matendo ya kibinadamu

Kabla hata hatujamaliza wiki ya kwanza ya mwezi wa pili tayari tumeshapoteza Watanzania wenzetu wasiopungua 40 kwenye matukio mawili tu. La mkanyagano Moshi kwenye kongamano la kidini.. Na vijana wetu 10 wa JKT waliopoteza maisha kambini Msata..

Hili la JKT taarifa rasmi bado lakini la Moshi tayari matamko yenye kukanganya yameshatolewa na viongozi mbali mbali. Wa kwanza kutoa Tamko na ambaye ni mhusika mkuu ni Waziri wa mambo ya ndani. Na alitoa angalizo zuri kuhusu sasa kuvifuatilia hivi vibanda na mabanda ya imani na shughuli zake. Amepongezwa na wengi

Kwa mstuko wa wengi jana kwenye shughuli za kuaga marehemu waliopoteza maisha yao kwenye kongamano la kukanyaga mafuta mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alisema hakuna haja ya kuzuia shughuli kama hizo na waliosababisha mkanyagano ni vijana vibaka waliotoka nje wakitakaa kuingia ndani

Mkuu wa mkoa kajuaje kuwa walikuwa vibaka na si watu wengine wowote?
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia kuhusu hali ya ulinzi na usalama wa eneo husika
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia muda ulioongezeka nje ya muda wa kibali
Mkuu wa mkoa hakuzungumzia kuhusu uzembe na uwajibikaji wa pamoja kwenye swala zima.
Sana sana amemkata kalima Waziri mwenye dhamana na sasa hawezi tena kuendelea kuchukua hatua alizotaka kuchukua.
Kwa hali ilivyo hakuna atakayewajibika wala kuwajibishwa....

Je, Mwamposa ni mkubwa kuliko mamlaka? Badala ya viongozi kuungana kukemea haya yanayotendwa na hawa viongozi wa dini janja janja ndio kwanza wanahamasishwa...

Jr
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amesema paliwekwa mabeseni ya mafuta katika mageti yote ila cha ajabu katika geti moja palitokea kundi la vijana kutoka nje ya uwanja na kulazimisha kuingia ndani kwa nguvu ndipo watu wakaanza kukanyagana.

Akizungumza katika ibada ya kuwaaga marehemu mama Mghwira amesema vijana hao hawaeleweki walikuwa wanaingia uwanjani kufanya nini kwani ibada ilishamalizika, yawezekana walikuwa vibaka.

Mkuu wa mkoa amewataka vijana hao wasiofahamika hadi sasa kutubu mbele za Mungu kwani dhambi waliyoitenda ni mbaya sana.

Mama Mghwira amesema Huduma za kiimani zitaendelea kama kawaida na kwamba mikutano ya Injili kuanzia sasa itaratibiwa kwa makini na ameomba kukutana na viongozi wote wa dini mkoani humo.

Mama Mghwira amesema aliongea na Rais Magufuli leo asubuhi na kwamba Rais alimtaka kutositisha shughuli za kidini bali waweke utaratibu mzuri wa kuzimonitor.

Source: TBC

Jr
 
Kuna kitu kimemuingia huyu mama, siku ya kwanza alionekana ktk video akikemea aina ya mahubiri ya nabii. Tena alishangazwa atawezaje kutatua matatizo ya watu wengi vile kwa wakati mmoja!!, akaenda mbali zaidi kwa kusema Alichokiona pale ni biashara, kila kitu kinauzwa tena kwa bei ya juu. Maji ya 700, yanauzwa 1000. Mama ghafla kabadili msimamo wake.
 
Engine mbili zinapokutana yenye nguvu ndogo huzima ghafla

Kwa inavyoonekana kwa sasa huyo mwamposa hakamatiki, si unaona ameweza kumtuliza hata mwenye mkoa wake, (yule wa Pompeo) sasa anaenda kumpiku hadi gwajboy ktk system.
 
Watu na nyakati.. Nyakati na watu..!!!
Kwa inavyoonekana kwa sasa huyo mwamposa hakamatiki, si unaona ameweza kumtuliza hata mwenye mkoa wake, (yule wa Pompeo) sasa anaenda kumpiku hadi gwajboy ktk system.

Jr
 
Siasa imeingia hapo, kila mtu ana hofu hajui afanye nini na kauli zinabadilishwa.

Shetani anashangilia kwa ushindi

(nyuma ya pazia) japo ni dhahili alijua atashinda mara baada ya kufika Dar.

Vinginevyo watu wamejua ukweli huko mtaani so wale waliokula keki na mafuta tu ndiyo wataendelea ila hawa wapya
labda pepo liwapitie gizani.
 
Kuna kitu kimemuingia huyu mama, siku ya kwanza alionekana ktk video akikemea aina ya mahubiri ya nabii. Tena alishangazwa atawezaje kutatua matatizo ya watu wengi vile kwa wakati mmoja!!, akaenda mbali zaidi kwa kusema Alichokiona pale ni biashara, kila kitu kinauzwa tena kwa bei ya juu. Maji ya 700, yanauzwa 1000. Mama ghafla kabadili msimamo wake.
Tatizo papara viongozi wengi wa Serikali wanakuwa wepesi kutoa matamko haraka haraka bila kufanya uchunguzi wa kina kwanza

Nilimshangaa Simbachawene nikasema huyu naye vipi si atulie kwanza na mkuu wa mkoa naye nikamshangaa

Matukio yakitokea ukisema tunaendelea na uchunguzi tutatoa taarifa kamili tukishakamilisha Kuna shida gani?
Mambo makubwa yakitokea viongozi wajifunze kutulia kwanza sio unatoka Kama alivyotoka Simbachawene na huyo mkuu wa mkoa na kuanza kukebehi imani za watu

Imani ya mtu ni kitu nyeti kiongozi wa Serikali anatakiwa kuwa makini nacho
 
Tatizo papara viongozi wengi wa Serikali wanakuwa wepesi kutoa matamko haraka haraka bill kufanya uchunguzi wa kina kwanza

Nilimshangaa Simbachawene nikasema huyu naye vipi si atulie kwanza na mkuu wa mkoa naye nikamshangaa

Matukio yakitokea ukisema tunaendelea na uchunguzi tutatoa taarifa kamili tukishakamilisha Kuna shifa gani?
Mambo makubwa yakitokea viongozi wajifunze kutulia kwanza sio unatoka Kama alivyotoka Simbachawene na huyo mkuu wa mkoa na kuanza kukebehi imani za watu

Imani ya mtu ni kitu nyeti kiongozi wa Serikali anatakiwa kuwa makini nacho
Dah! Taifa lina kazi kubwa hili. Shida ipo kuanzia juu hadi chini kabisa, kama maoni yenyewe ndio haya...safari bado ni ndefu!!!
 
Back
Top Bottom