Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,943
- 25,284
Vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona imepata pigo kubwa nchini Kenya baada ya serikali kufunga kimya kimya vituo 20 vilivyokuwa vikihusika na ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya vipimo vya maambukizi ya virusi vya corona.
Serikali imeamua kuhamisha nguvu zaidi katika kutibu na kuhudumia wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Serikali hiyo imesema imeamua kuhamisha nguvu upande huo kutokana na kushindwa kustahimili upimaji wa watu wengi "mass testing".
Hata hivyo watafiti nchini Kenya wameishutumu serikali kwa kuwatelekeza wananchi wasiokuwa na uwezo katika saa wanayohitaji msaada zaidi. Hatua hiyo ya kufunga vituo hivyo imepelekea ufunguaji wa maabara sita (6) za taasisi binafsi zinazotoza gharama ya (shilingi za kikenya) Ksh 8000 mpaka Ksh 13,000 (sawa na dola za kimarekani 75 mpaka 121). Gharama hizo zimetajwa kuwa ni kubwa mno kwa raia wengi wa Kenya ambao tayari wamekwisha athirika kiuchumi kutokana na janga hili la virusi vya Corona.
Baadhi ya raia wamelalamika katika mitandao ya kijamii kutozwa kiasi cha shilingi za kikenya (Ksh) 5000 kwa wagonjwa waliolazwa ndani ya hospitali ya taifa ya Kenyatta ili kupata kipimo cha maambukizi ya virusi vya corona kama inavyoonekana katika risiti hapo chini.
====
Source:
Blow to Covid-19 fight as State abandons testing - People Daily