Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,900
- 12,347
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika hapo chini.
Nchini kwetu kuna vyama vingi vya siasa. Na kila chama kina lengo na nia ya kushika madaraka na kutuongoza kupitia sera za chama husika.
Ingawa kila chama kina sera zake na maono yake, lakini ukiangalia kwa makini utakuta vyama vyote vina sera zenye lengo la kuijenga Tanzania yenye umoja, upendo, mshikamano, elimu bora, maendeleo ya watu na vitu nk, na hilo ndio huwa lengo kuu la uanzishwaji wa vyama au chama husika.
Sasa inashangaza leo hii kuna chama kinakuja na sera za kuigawa Tanzania na watanzania kwa ujumla. Chama hicho kimekuwa kikienda tofauti mno na misingi ya uanzishwaji wake kwa kuja na sera za kupinga Muungano wetu ambao ulikuwa ni maono ya viongozi wawili wa nchi zetu mbili baba wa taifa mwl J. K. Nyerere na mzee Abeid . A . Karume.
Wazee hao kabla ya kuungana bila shaka walikaa chini wakajadiliana kuhusu faida na hasara za muungano huo, ambapo bila shaka baadae walikaa wakagundua kuwa muungano wao utakuwa na faida nyingi kuliko hasara.
Sasa inashangaza leo hii kuna kundi lililokuwa linafaidika na utawala wa sultani, linatengeneza magenge ya kupinga muungano ili utakapovunjika waweze kuiteka tena Zanzibar na kuangukia katika mikono yao kama zamani.
Walianza kwa kulalamika kuwa tunawaonea, baada ya kuwapa kila walichokitaka, sasa leo hii wanakuja na visingizio vya kutaka mamlaka kamili.
Sipingi wao kupewa kisiwa chao ambacho kwa namna kubwa sisi wabara ndio tunaopata hasara kwa kuwabeba na kuwasaidia mengi ikiwemo kuwapa ardhi bure huku kwetu, sema sasa ni kwanini watumie njia hiyo ya kudai nchi yao kupitia chama kilichoanzishwa na mtu anaejiita msomi kutoka bara. Je lengo kuu la kuanzishwa ACT Wazalendo ilikuwa ni kuja kutumiwa na hawa wazanzibar uchwara? au imetokea tu baada ya kuhamia chama hicho na kukuta uongozi wa chama hicho chini ya Zito ni dhaifu, hivyo wakaona hapo ndio pazuri wao kupenyezea ajenda zao huku ndugu Zito ambae ndio kiongozi mkuu wa chama akiangalia tu bila kuonya swala hilo?