Kibukuasili
JF-Expert Member
- May 15, 2010
- 1,050
- 605
Du! speechless
ndugu yangu huyo mungu aliyewanyima hawa ndo kakupa wewe. Tena usisema kabisa, maana laiti ungejua namna ambavyo mungu alivyo na sera kama za marekani wala usingekaa chini ujivune hivyo kwa kuwa mungu kakupa wewe mvua. Mungu hana rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Leo amekupa wewe mvua, lakini kesho atakunyima, hela utakuwa nayo lakini haitakuwa na uwezo wa kununua chakula kwa kuwa hakitakuwepo. Tuwaombee rehema hawa wenzetu. Hawakupenda yawakute hayo. Laiti mvua ingenyesha halafu wakashindwa kulima, tungewalaumu lakini hawana mvua, wafanyaje kuikabili hiyo changamoto. Au watengeneze mvua zao?