Usilipigie jibu mstari. Jua ni hivyo, ila, kwanini mnawasumbua wacha Mungu?? Mnapata faida gani?? Mtu kwenda Kuswali imekuwa ni ugaidini?? Haya lakini muelewe kuwa Mola anawaona wala hatokaa kimya
Watuhumiwa hao ni wa muda mrefu Sana, usihusishe mavazi na matendo ya mtu, kwa sasa baadhi ya waharifu wamegeuza mavazi kufanya uharifu wao huku wakigeuza na kuzichafua dini,
Hebu soma hiyo japo upate mwanza.
Kamanda Sabas alisema mtuhumiwa huyo alikiri kushiriki tukio la Mei 5 mwaka 2013 saa 10:30 eneo la Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Olasiti jijini Arusha ambapo aliratibu kurushwa kwa bomu na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 56.
Tukio la tatu lilitokea Juni 15 mwaka 2013 saa 11:50 jioni katika Viwanja vya Soweto Kata ya Kaloleni Jijini Arusha, ambapo marehemu na wenzake walirusha bomu na kujeruhi watu 60 na wanne kufariki dunia waliokuwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kamanda Sabas Alitaja matukio mengine aliyokiri kuhusika nayo ni lile la Julai 11 mwaka 2013 eneo la kwa Mrombo jijini hapa, ambapo alishirikiana na wenzake kumwagia tindikali usoni Sheikh Said Juma Makamba.
Tukio jingine ni lile la Februari 12 mwaka 2014 saa eneo la Tindigani Unga limited jijini hapa kwenye msikiti wa Sawiyatu Qadiria, walipommwagia tindikali usoni Sheikh Hassan Bashir.
Tukio la sita la Februari 28 mwaka 2014 saa 5:15 alfajiri huko msikiti wa Bondeni Jijini Arusha, marehemu na wenzake walimwagia tindikali Mistapha Mohamed Kiago na kumjeruhi usoni na shingoni.
Tukio la saba Aprili 13 mwaka 2014 saa 1:30 usiku, eneo la Mianzini, huko nyumba ya kulala wageni na Baa ya Night Park, walirusha bomu na kujeruhi watu kumi na mtu mmoja kusababisha kifo chake.
Kamanda alitaja tukio lingine aliloshiriki ni la Aprili 13 mwaka 2014 la saa 5 eneo la Majengo jijini Arusha, alirusha bomu kwa kushirikina na wenzake na kujeruhi watu wawili Sudi Ali Sudi (37) ambaye ni Mkurugenzi wa Answar Muslim kanda ya Kaskazini na mwenzake Muhaji Hussein Kifea (38) mkazi wa Dare s Salaam.
Tukio la tisa mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa Julai 7 mwaka 2014 saa 4:15 usiku eneo la uzunguni, mgahawa wa vama Traditional Indian uliopo jirani na Viwanja vya Gymkhana alirusha bomu na kujeruhi watu nane.