Picha za mlima Kilimanjaro toka angani

Hii itafanya watoto/wajukuu wetu baadae ,kujimbua makaburi ye2 ili wapeleke maabara kutafiti kama 2likuwa na akili sawa sawa kwanini 2shindwe ku2nza mazingira ye2??
Hali inaonesha hakuna kizuri kitakachosalia .......unafikiri hichom kizaz kitaish vp...
 
Safi sana mpiga picha. Ukipiga picha mlima huu mida ya asubuhi huwa zinatoka vema sana, I did the same in 2008 when flying over there, mlima unapendeza sana.
 
Hizi picha (mbili za juu) zimepigwa kutokea upande wa Kaskazini, upande wa Kenya ambako snow hakuna sana na kipindi cha kiangazi hutoweka kabisa. Hizo picha zingine ni kile kilele kidogo cha Mawenzi ambacho huwa hakina snow kabisaa labda kipindi cha masika tena kidogo sana
 
Ni kweli inategemea picha imepigwa msimu wa kiangazi au wakati wa baridi na mvua.,lakini ukibahatika kufika huko kileleni ndio umaweza kuappreciate kinachoonekana kwenye hiyo picha, mimi nimewahi kubahatika kupanda huo mlima, ukiwa uhuru peak unaweza kuona vizuri mazingira ya huko juu, hali ni mbaya kwa kweli, ile permanent snow cap inatoweka kwa kasi ya ajabu kutokana na global warming, ni kweli kama wanavyosema wataalamu baada ya miaka labda 15 au 20 ijayo hicho kilele kitakuwa hakina tofauti na kichuguu.

Naomba kuhabarishwa; Hivi watalii wanapanda mlima Kilimanjaro kwa sababu ya kuwepo barafu au kwa sababu ni mlima mrefu Afrika?
Nauliza hivi kwa sababu hata barafu ikiisha ambao ndio ukweli bado Kilimanjaro utabakia mlima mrefu kuliko yote Afrika?.
 
Back
Top Bottom