Picha za Mkapa na Vincent wakiwa kwenye msiba wa baba-Vincent yaani Kiboko Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha za Mkapa na Vincent wakiwa kwenye msiba wa baba-Vincent yaani Kiboko Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Mar 27, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Vincent Nyerere.jpg

  Kama hutaweza kuona vizuri picha hizi ni kwamba zimepigwa mara mbili. Moja ni Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Josephat Kiboko Nyerere, huku pembeni yake akiwepo Anne Mkapa, Maria Nyerere na Chief Japhet Wanzagi.

  Nyuma ya Mkapa ni Vincent Nyerere huyu mbunge wa CHADEMA lakini wakati huo yaani December 19, 2007 hajawa mbunge. Utaona picha ya Vincent imezungushiwa duara ili kumuonyesha vizuri.

  Hapo ni nyumbani kwa marehemu yaani kwao na Vincent Nyerere.


  Picha ya chini ni kwenye misa ya mazishi katika Kanisa Katoliki, parokia ya Butiama. Mnamuona Benjamin Mkapa amekaa kiti cha mbele kanisani akiwa ameshika kitabu akifuatilia misa. Hapa vilevile nyuma ya Mkapa ni Vincent Nyerere.

  Kazi kwenu wana JF, the place we dare talk, the place we dare expose the unexposed!

  Source:
  JAMHURI,
  ISSN-1821-8156, No. 17
  March 27, 2012
   
 2. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  duuh hapo sasa..
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ulimi ulimteleza mzee mzima. nadhani anajutia kauli yake kimoyomoyo.

   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Aibu yake mwenyewe Kipara sio Busara
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  hili gazeti linakuja vizuri.
   
 6. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,102
  Likes Received: 341
  Trophy Points: 180
  Mkuu umetoa kwenye gazeti la mfanyakazi nini??du nikupe password
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu hata mimi nimeanza kulizimia hili gazeti. Good replacement for Raia Mwema
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  BMW kaumbukaaaaaaa!
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Inatosha jamani tusiwafanye wakatokwa mapovu bure kwa kujitahidi kujibu/kutetea hili pia..
   
 10. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Jamani Ben alisema alikuwa anatania! Maajabu hayatakaa yaishe
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nina wasiwasi na kumbukumbu za kipipa mkapa!
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nilisema na nitarudia tena kusema Balile na Boss wake [Mmiliki wa gazeti la Jamhuri] wako kazini wakiwa na agenda ya 2012 ndani ya CCM na 2015 kwa ajili ya kuingia Magogoni. Hii habari haitaisha labda Mkapa aamue kwenda Mahakamani kuomba magazeti yasiendelee kuiandika, vinginevyo kuna mtu anataendelea kutumia habari hii kama mtaji.
   
 13. A2 P

  A2 P Senior Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuuu. Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu kali ili usichanganye mambo. Aibuuuuu...............................:violin:
   
 14. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ukiwa muongo hupaswi kuwa msahaulifu..mkapa kawa msahaulifu anakula matapish yake sasa
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  mtu mzima nguo zmemvuka
   
 16. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli Jf ni zaidi ya social netiweki...

  source
  ;
  Mwakalinga
   
 17. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huo msiba mwaka gani? Ungekuwa wewe ungemkumbuka mtu huyo uliyemuona miaka 15 iliyopita?
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama unajua hata kinachojadiliwa.
   
 19. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwa wote wanaoshabikia hili suala, wamekuwa hawana point muhimu zinazowafanya kumlaumu BWM. Mimi binafsi ktk ukoo wetu wengi wananijua lakini mimi siwafahamu hii inatokana na umaarufu wangu hivyo hakuna cha ajabu hapo.
   
 20. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Soma vizuri msiba ulikuwa 2007 mkuu!
   
Loading...