Picha ya Tabora jazz Band | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha ya Tabora jazz Band

Discussion in 'Entertainment' started by ngalikikinakiki, Aug 30, 2011.

 1. ngalikikinakiki

  ngalikikinakiki Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2013
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dahhh, hizi Band za zamani na miziki yake ilikuwa poa sana. I wish ningeliweza kuwaona LIVE wakihangaika kucheza maana siku hizo hata kucheza hawajui labda hadi walewe wanaanza kujirusharusha na kujipinduapindua kama funza...

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2013
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Asante sana ndugu yangu Sikonge.

  Huu wimbo wa Alhamdulillahi ni wimbo nilioupenda sana kuliko hata ule wa Dada Asha. Wimbo huu ulitolewa mwaka 1972 muda mfupi sana baada ya Morogoro Jazz kusambaratika na kuundwa kwa Super Volcano. Kipindi hicho bendi iliyokuwa na ubavu wa kubanana na Tabora Jazz ilikuwa ni Morogoro Jazz tu, ambapo kipindi hicho Tabora Jazz ndiyo iliyokuwa inashikiria taji na bendi bora ya muziki Tanzania kabla hawajanyang'anywa taji hilo na sunburst na baadaye Afro Sabini. Tabora Jazz walikuwa wamepokonya taji hilo kutoka kwa Morogoro Jazz ambayo nayo ilikuwa imebadilishana taji hilo na Jamhuri Jazz ya Tanga mwaka mmoja tu nyuma yake.

  Sasa wakati Morogoro Jazz inasambaratika na kuuundwa kwa Super Volcana, Jamhuri Jazz nayo ilikuwa aimeanza kusambaratika kwa vile wapigaji wake wakubwa akina George Kinyonga na Professor Omari walikuwa wamehamia kwenye bendi ya Kurugenzi ya Arusha ambako ndiko walikotokea na kwenda kuanzisha Simba wa Nyika.

  Mzee Shem Kalenga aliona kuwa taji la ubingwa wa bendi lilkikuwa linafuatiwa na balaa la kuvunjika kwa bendi ndipo akatoa dua kwa kutunga wimbo huo wa Alhamdulilahi.

  Sijui kama nimekusaidai kidogo
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2013
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kaka Kichuguu,

  Nashukuru sana kwa majibu ambayo nafikiri jamaa wengi wa Blog hasa Mzee John Kitime wangelichukua kabisa hiki kipande kizuri cha historia na kukiweka kwenye Blog zao. Nategemea siku moja mtu atakuja kuandika historia nzima ya hizi Band tatu maarufu za mziki za mkoa wetu wa Tabora.

  Ningelisoma zaidi na zaidi na hasa Band hizi nyingine mbili ambazo niseme ukweli sijawahi kabisa kufahamu historia yake yaani Nyanyembe Jazz na Kiko Kids ambazo nazo kwa aina moja au nyingine zilipata sifa kubwa mjini Tabora na hata nje ya Mkoa.   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280

  Nausaka sana ule WIVU UKIZID MAPENZI YAPUNGUA
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2013
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  KUTOKA KWA KITIME GLOG:

  [​IMG]

  Mkuu kitime kwenye picha hii ya Tabora Jazz,huyo aliyesimaa wa kwanza kulia(jacket ya track) ni mjomba wetu soloist wa kwanza kabisa kabla ya Shem Karenga Athmani Tembo(Baba Nyota)R.I.P,aliacha miziki akaingia kazi ya railway akafanya Shinyanga,Moshi,na kurudi Tabora alifariki muda mfupi tu baada ya kustaafu Railway,pia alipoacha miziki akawa mswalihina mtu wa swala tano,atakumbukwa sana kwa kuwa nae alikuwa guitarist mzuri sana.R.I.P uncle AthmaniTembo.
  Abbu Omar,prof.Jnr.(Mwanamuziki)Tokyo,Japan .

  Kijiwe cha KITIME: Chakula kwa jirani ya Tabora Jazz Band
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2013
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Asha wewe...kibao kitamu ajabu!
   
 9. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2013
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
Loading...