Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Pratik Joshi alikuwa akiishi London kwa miaka sita. Akiwa mtaalamu wa programu, alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuijenga maisha ya Ulaya pamoja na mke wake na watoto wao watatu wadogo, waliokuwa wakikaa India.
Baada ya miaka mingi ya kusubiri kibali, hatimaye ndoto hiyo ilikuwa karibu kutimia. Siku mbili tu zilizopita, mke wake, Dk Komi Vyas, daktari maarufu kutoka Udaipur, aliacha kazi yake. Mifuko ilikuwa tayari imefungwa, waliaga wapendwa wao, na maisha mapya yalionekana kuwa karibu kufikiwa.
Siku ya safari Juni 12, familia hiyo ya watu watano, wakiwa na matumaini na furaha, walipanda ndege ya Air India kuelekea London. Walipiga picha ya pamoja (selfie) na kuituma kwa ndugu. Ilikuwa ni safari ya njia moja kuelekea maisha mapya. Lakini hawakuwahi kufika. Ndege ilianguka. Hakuna aliyenusurika.
Kwa muda wa sekunde chache, ndoto za maisha yote ziligeuka kuwa majivu. Ni ukumbusho wa kikatili kwamba maisha ni dhaifu mno.