Picha ya Etoo na Ligobert Song inaongea

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Picha inaongea:

Wawili pichani ni wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, kulia ni Samwel Eto'o na kulia ni Rigobert Song.

Wakati wakicheza Samwel Eto'o alikuwa ni mchezaji tegemezi katika safu ya ushambuliaji na upachikaji mabao. Song yeye alikuwa mlinzi na ndiye alikuwa Kilanja au Nahodha(Captain) wa timu Yao ambayo si haba, ilikuwa na mafanikio ya kutosha ikitwaa mataji ya Afcon na kushiriki michuano ile mikubwa kabisa ya Kombe la Dunia.

Kwa sasa baada ya kustaafu kucheza soka, Song yeye ni kocha(mwalimu wa Mpira wa miguu), na Eto'o yeye kwa sasa ndiye Bosi wa Soka nchini Cameroon akiwa ndiye Rais wa chama cha soka cha nchi hiyo ya Afrika ya magharibi.

Kwa Imani aliyokuwa nayo kwa Captain wake wa zamani, Eto'o aliamua na kubariki kumkabidhi Song jukumu la kufundisha timu ya taifa, tena wakati ikiwa na ratiba ngumu ya kucheza michezo ya hatua ya makundi kupata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia.

Pichani kama unavyoona, Eto'o akimuangalia kwa hasira Kocha wake mteule wa timu ya taifa baada ya Cameroon kupoteza Mchezo muhimu na mgumu katika uwanja wa nyumbani kwa bao moja kwa bila dhidi ya Timu ngumu ya Algeria.

Hakuna amani kati Yao, sura zao zinaongea, Eto'o akikunja sura kimamlaka na katika namna ya kulaumu, wakati Song yeye akiinamisha uso chini ishara ya kukiri au kujutia makosa.

Kuna kosa Eto'o amelifanya, ndio linalomgharimu, na kwa kiasi fulani anajutia kwa maamuzi yake ya kumwamini Kaka yake(kiumri) Song.

Majuto aliyo nayo Sasa hayawezi kubadili hali ya mambo, tayari wameshapoteza point Tatu, tena katika ardhi ya nyumbani, ni kosa kubwa sana kwa Mpira wa kileo ambao unalazimisha kila mtu kuhakikisha anashinda uwanja wa nyumbani.

Kosa alilofanya Eto'o ndiyo makosa ambayo wa Afrika wengi tumekuwa tukiyafanya na kutugharimu, kumwamini mtu kwa kuwa unamjua si kwa kuwa ana Vigezo.

Kwanini Eto'o alikubali kuifanya timu ya taifa kama field(darasa la mafunzo) kwa Song ambaye Nina uhakika hajawahi au hana rekodi yoyote ya kufundisha soka kwa mafanikio popote, iweje akaaminiwa kwa timu ya taifa?

Yaani ni sawa na hapa kwetu leo umpe majukumu ya Timu ya taifa Mecky Mexime au Mwanamtwa Kihwelu. Yes ni makocha wazuri na tutajivunia sana kama wako fanya vizuri, wakiharibu hatutokuelewa, na ni hapo wachambuzi wetu utawajua ni wachambuzi au wachang'ombe
Lakini Kwa upande wa pili inawezekana kwa Imani ya Eto'o kwa wachezaji wa kizazi cha Sasa cha Cameroon aliona hakuna wa kuwazuia, akaona ni heri sifa za kufanya vema ziende kwa mzawa kuliko kwenda kwa mzungu.

Inawezekana yeye Eto'o anaamini sana kwa uwezo wa wachezaji uwanjani kuliko uwezo wa kocha kuwaunganisha wachezaji kimfumo.

Lakini kama dhamira yake Eto'o ilikuwa ni kuondoka utegemezi kwa makocha wa kigeni basi nampongeza kwa ujasiri na uthubutu wake.

Na kama aliamini katika MAZOEA kwamba Cameroon kwa kushiriki World Cup haina mjadala, basi anapaswa kuwaomba radhi wana wa Cameroon na Afrika kwa ujumla.

Lakini yote kwa yote, hii ya udugu (nepotism) na kujuana tukaacha weledi (professionalism) ndivyo vinaharibu Mpira WETU Africa.

'the Bridge is too far' Safari bado ni ndefu sana.

IMG-20220328-WA0007.jpg
 
Mtu mmempa team wakati mbaya,team ina michezo miwili ambayo ndo anaanza nayo unategemea nini hapo mkuu, team haijengwi Kwa siku moja inahitaji mda kitu ambacho waafrika hatukiwezi.

Tunataka kocha akichukua team aanze kupata matokeo.

Jambo la msingi Etoo alipaswa amuache Yule kocha amalizie kipindi chake Hadi hatua hiyo ya kufuzu kisha baada ya hapo ndo angeanza upya na kocha mpya kujenga kikosi.....
 
Cameroon tuliwaona majuzi wakicheza mashindano ya Africa, pamoja na kuwa yalichezwa kwao lakini hawakuwa na kiwango cha kueleweka.

Walibebwa bebwa ili wasitoke mapema ila mbeleko ikakatika, hawa si Comoro iliwatoa kamasi?

Cameroon wakubali kuwa kwa sasa hawana kikosi cha ushindani na waanze kuunda upya.

Tena ni aheri wasiende world cup, wanaweza kupoteza game zote.
 
Cameroon afcon alikuwa anabebwa bebwa na marefa tu.

World cup anaanzia wapi kufuzu huku bara zima la africa lina nchi 60 zinagombea nafasi 5 tu.

mwarabu kamfunga cameroon akiwa kwake mechi ya kwanza. Sasa cameroon anaanzia wapi kwenda kupindua meza uarabuni.. kule anaenda kula 5 kwa bila
 
Timu pekee afrika yenye ushindani WC ni Algeria Cameroon hawakuwa na bahati na ndio maana wakapangwa na wababe wa Afrika(Algeria).
Kwa mpira wa Cameroon hata Ivory Coast wangeshinda kwenda WC
 
Back
Top Bottom