Njitapu: Nilicheza mpira kwa ajili ya maisha yangu, hata mlinzi wa getini hajawahi kula chakula changu

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,197
1,835
"Ndio, Sihitaji Watu wanisumbue tena, Mimi sio Msamaria Mwema Kama Samuel Eto'o, Kwani yule Ni Eto'o na Mimi Ni Njitap!

Sikuteseka kutafuta pesa kwa Miaka Mingi ili kuja kuiokoa Dunia Nzima. Hata Familia Yangu yenyewe tu Kuna Muda huwa inalalamika kuhusu Mimi lakini Mi Sijali, Ni Mungu Pekee atakayenihukumu na Sio Binadamu unayempa kitu, uliyempa kitu au ambaye hukumpa kitu.

Siku zote nimekuwa nikimwambia Eto'o Kwamba Kuna siku Watakucheka kwa Dhihaka, Na Biblia ilishatabiri Hayo yote, Mimi Jeremy Njitap nimebaki vile vile, Pesa Yangu Ni Yangu, Na Kama nisingecheza Mpira Nani angekuwa Tayari kunisaidia? Sinunui Huruma Mimi.

Huwezi kunisikia Nachangisha Michango kwa Mtu yeyote, Halafu Wengi Wanaamini pengine Mimi siishi Kabisa Cameroon Sababu Muda Karibu Wote napendelea kukaa Nyumbani na Geti langu Muda Wote likiwa limefungwa, Hata huyo Mlinzi wangu mwenyewe Hana sahani ya Chakula Nyumbani kwangu Maana Mshahara wake Unamtosha kula kwake". - Jeremy Njitap!

#Note: Njitap Ni Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Chelsea na Real Madrid.

1711301172476.jpg
 
Back
Top Bottom