bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,667
Afcon ndio hiyo imeshika kasi pale nyumbani kwa Fundi Pacome Ivory coast mpaka sasa sio haba ila bado tunamiss lile soka haswa la kiafrika soka la mashuti mazito, soka la nguvu, soka la kutumia winga kwa timu kutoka upande wa Kaskazini mwa Afrika.
Tumeshuhudia mechi za awali timu zinazopigiwa chapuo nyingi zimeponea chupuchupu kupoteza mechi zao za awali na wakionyesha kiwango duni pamoja na wachezaji wao wengi kutoka vilabu vikubwa vya Ulaya na wengine ni mastaa kabisa kwenye timu zao.
Binafsi nahisi umefika wakati wa makocha wa timu za Taifa kuita wachezaji wengi wa ndani na angalau wachezaji wanne wa nje tena wale wengi uzalendo wa haswa ambao wapo tiyari kujitoa kwa maslahi ya nchi zao.
Nimeagalia gemu ya Nigeria jana pamoja na Cameroon leo pamoja na kuwa na wachezaji wengi karibia asilimia 99 ila bado hamna kitu wengi wanacheza kupata sifa binafsi na sio kwa maslahi ya timu.
Zamani tulikua na kauli ya kusema timu imejaa mafather au wanacheza kifather ndio nimelishuhudia hilo kwa hizi gemu za awali Nigeria wao wamebaki na style za nywele tu ubishoo mwingi, Cameroon leo mpaka Etoo alikua anatikisa kichwa kwa kiwango kibovu cha wachezaji wake.
Makocha Waite wachezaji wengi wa ndani ili tuone lile soka la kiafrika na hawa watacheza kwa bidii na nguvu ili wauzike Ulaya.