Picha: Wasanii 41 wajiunga na chadema arusha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

PIC+2.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Mwigamba Samson
PIC+3.jpg



Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa
PIC+4.jpg


Mwnyekiti wa kikundi cha Serengeti akikabidhiwa katiba na kadi ya uanachama ya CHADEMA


PIC+5.jpg



PIC+6.jpg



PIC+7.jpg

Baadhi ya wasanii hao ambao wamevua gamba na kuvikwa gwanda

Na Idd Uwesu, Arusha Yetu


Sanaa kama moja wapo ya vyanzo vya ajira nchini haina budi kusimamiwa kikamilifu na serikali ili kuwezesha taifa kupunguza tatizo la ajira. Ni wakati muafaka hivi sasa kwa serikali kuhakikisha inaandaa utaratibu mzuri wa kukulinda maslahi ya wasanii kwa kusimamia uendeshwaji mzima wa biashara ya kazi hizo.


Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Arusha, Mwigamba Samson wakati akiwapokea wanachama zaidi ya 40 ambao ni wasanii wa kikundi cha Serengeti Art Group kama wanachama wapya wa chama hicho.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa inashangaza kuona wasanii wengi wa Tanzania wana hali mbaya kiuchumi licha ya kazi kubwa na nzuri wanazozifanya na kuongeza kuwa hali hiyo inasababibshwa na serikali iliyopo madarakani kutojali kazi hizo. Amesema kama chama na kupitia wabunge wa chadema wamefanya kazi kubwa ya kuishinikiza serikali kuliona hilo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa, amesema sera ya chama chake kuhusu sanaa ni kuona kuwa sanaa haibakii kutumbuiza peke yake bali ni kuhakikisha kuwa inakua ajira rasmi kwa wasanii na wadau wanaojihusisha nayo kwa namna moja ama nyingine.


Katibu huyo ameongeza kuwa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea hivi sasa lina lengo la kuzidi kukiimarisha chama na kwamba mkoani Arusha vuguvugu hilo litafanyika mnamo mwezi wa kumi na moja hivyo amewataka wanacham hao wapya kuanza kazi ya kuleta mabadiliko kama lengo la vuguvugu hilo linavyosema.

Blogzamikoa

blogszamikoa.blogspot.com
 
Jamani chadema hamna huruma! moro,mwanza,igunga,arusha sasa nape tuanzie wapi?
 
ongeleni, kumbe ni wasanii???

RAIS wetu amemuandalia red carpet MSANII DIAMOND na kuhakikisha anakwenda DMV kwenye Sherehe za UFUNGUZI wa Tawi USA

Sasa yeye pia ana wasanii... kwanini hautaki CHADEMA wawe na Wasanii? WIVU ni MBAYA; Questioning everything CHADEMA is DOING

CCM bila WASANII 2010 Mngepata Wananchi kwenye Mikutano?
 
Mtaishia kunawa, walaji ni wengine. subiri 2015, kura zitatosha tu. wembe ni ule ule.
 

RAIS wetu amemuandalia red carpet MSANII DIAMOND na kuhakikisha anakwenda DMV kwenye Sherehe za UFUNGUZI wa Tawi USA

Sasa yeye pia ana wasanii... kwanini hautaki CHADEMA wawe na Wasanii? WIVU ni MBAYA; Questioning everything CHADEMA is DOING

CCM bila WASANII 2010 Mngepata Wananchi kwenye Mikutano?

mkuu umenifungua akili nakumbuka nilimsikiliza yule katibu na mwenyekiti wa DMV kupitia you tube aliongea utumbo saana mwisho wa siku akamalizia akasema tutamleta msanii mkali tanzania siku ya ufunguzi wazalendo wamechanga pesa kumbe ni jk ndio anaratibu mambo hayo? nimeunganisha nimepata jibu,
 
Bora hata ungesema, wanaarusha 41 wamejiunga chadema kuli kutumia neno wasanii, siku hizi hata wacheza ngoma za kienyeji wamekua wasanii? Naona siku hizi topic zinakuja humuna na title kubwa,ukiingia ndani unakuta ni uharo tu.
 
Bora hata ungesema, wanaarusha 41 wamejiunga chadema kuli kutumia neno wasanii, siku hizi hata wacheza ngoma za kienyeji wamekua wasanii? Naona siku hizi topic zinakuja humuna na title kubwa,ukiingia ndani unakuta ni uharo tu.
Kwani uchezaji ngoma si sanaa?kumbe magamba akili zenu kiduchu mno.
 
hawa na wale wamasai wanao cheza ngoma ngorongoro kwaajili ya watalii wana tofauti gani. Neno msanii lina hadhi yake bana.
Kama wanachofanya hao wamasai ni sanaa,basi ni wasanii.usibandike tu just for the sake of it ama kishabikishabiki tu.Nina wasiwasi sana na uwezo wako wa kuelewa.
 
Back
Top Bottom