Picha/video wakati wa faragha

Akili Pesa

JF-Expert Member
Jun 18, 2014
616
854
Wadau wapenda mahusiano, mapenzi na urafiki habarini za usiku?

Nimeingia mda huu JF kiukwel ni kutokana na story ya Star mchanga kabisa "Nandy" kuibua mjadala mkubwa katka "social network" nyingi sana nchini na nchi za nje za majirani zetu, kiukwel kitendo alichokifanya cha kuachia post ya vdeo fupi "clip" akiwa yeye binafsi faragha na msanii mwenzie Billnas imeumiza watu wengi sana hasa tukiamini kwa Tanzania bado ni vitu vigeni kijamii ingawa kimmoja mmoja ni kawaida sana.

Nasema kuachia yeye nikiwa na maana kuwa yeye kama yeye kwenye video ndio anaonekana kurekod ile vdeo kwa bashasha kabisa lakini kwanini ije kurushwa na mtu mwingine mitandaoni?

Kwenye hili nafikiri naweza kuliangalia katika namna mbili tatu hivi;

1. Namna ya kwanza kwanza ni kwa Nandy kutaka kuwafanyia surprise waTz kuwa Billnass ni mpenzi wake na pengine hii inakuja kutoka na amesikia labda Billnenga kama anavyojiita kuwa anatoka na msichana mwingine ambaye kwa vyovyote ni msanii mwenzake hata yawezekana ni shosti yake kwahiyo imetumika trick ichukuliwe video fupi halafu Nandy atulie aje aitupie Billnas Insta nakuaminisha watu kuwa yeye hakufanya kwakuwa haikutokea kwake na pengine aliiogopa zaidi familia yake lakini akashndwa kufikiri mbinu nzuri ya kumthibitishia mbaya wake kuwa yeye yupo na Billnass kama wapenzi.

2.Namna nyingne ni pale ambapo nakumbuka ni juzijuzi tu wiki za karibuni Nandy alihojiwa juu ya mahusiano yake na Billnas na akakataa katakata juu ya mahusiano yao, sasa tuamini kuwa ni kweli hana mahusiano nae kwa sasa labda waliachana kwahiyo tuchukulie Billnas akaamua kuonesha video ile ili waTz wajue kuwa Nandy ni muongo na hakusema ukweli juu mahusiano yao.
Hivyo kwa video ile kuipost itamlazmu Nandy awe Punda kwa Billnas kwasababu pengine Nandy anajua kuna vituko vingi alishafanya na Billnas kipindi wapo katika mahusiano na anaamini vikirushwa kwa awamu itakuwa balaa kuanzia kwa familia yake, heshma yake na kazi yake kwa maana muziki wake. Kwahiyo hii ndio inamfanya awe yupo "stress" zaidi ya tukio lenyewe, ambapo itamlazmu kufuata matakwa ya Billnas pengine waendelea na mahusiano kama hayapo kwa sasa.

3.Namna ya tatu ni "masuala ya kibiashara" pengine kuna watu wameamua kufanyia kazi na kuratibu kila kitu juu hili jambo na hii ni baada ya kuona kuwa Nandy yupo juu pale kimuziki na asiweza kushuka Leo au kesho na muziki ni biashara ngumu kwa sasa na ghali Tz, hivyo wakaamua kuratibu hili na kulifanya liwe jambo kubwa la kumnyongonyeza Nandy katika kazi zake na kumtoa kwenye reli na hvyo kutoa nafasi kwa wadada wengine kupata airtime kwenye media za bongo hapa Tz, so kama ni hvyo basi lazma Billnas atahuska juu ya hili kama sehemu ya ushiriki wa kushusha heshima ya mtu tena kwa mambo ya faragha.

Nini kifanyike baada ya khasia hii:
a)Kwanza ni kuhakikisha Jamii inaachana na tabia hii ya kujirekodi wakati wa Ffaragha au kujipiga picha haina mantiki halisi yani wapenzi mkishakubaliana mpo faragha basi yapo mambo mengi ya kufanya lakini sio kitandani upande na camera au simu yani hata hao porn stars wakitaka kufanya movie zao wanakuwa wanajua ni uhalisia ndio maana inakuwa vile lakini siamini kupiga pcha na video ni sehemu ya kuamsha hisia na ukiona una mpenzi wa kupiga picha ndio aamshe ujue hapo una kanyaboya, sikatai kweli unaweza ukapiga picha na mpenzi faragha lakini basi iwe kipindi cha awali mmeingia tu bado hata kuanza chochote basi hapo ni sawa lakini sasa wewe mtu tayari kitandani mchupi huo kwa kamera haifai.

b) Ikiwa Nandy kweli anayojitetea ana hakika ni kweli kabisa basi nafikiri mimi sio mwanasheria lakini naamini akifuata protocal za kimahakama atapata nafasi nzuri ya kupata haki yake ya "kuheshimiwa" ambayo imepotezwa ndani ya sekunde chache sana na watu au mtu akishiriki kupost video ile kwa Mara ya kwanza mtandaoni hapa ndio ile sheria yetu chungu itafanya kazi kwa uhakika na wataadhibiwa wahuska wa kosa hilo.

c) Kuna kitu huwa tunakisahau sana jamani katika industry ya mziki nacho "manager wa msanii" hyu ni mtu muhimu sana ndiye dira ya msanii husika yani watu kama hawa inapotokea msanii ameharbu kama hivi mtu wa kwanza kumshambulia ni meneja wa msanii lakini sasa kwa bongo utagundua wasanii wengi wapo tu wakiamini game wanaweza kuisimamia wenyewe hapana tuwaelimisheni kuwa msanii lazima uwe "under management" ili kuleta mafanikio karibu na wewe. Niliwahi kuuliza baadhi ya wasanii kwanini huna meneja akanijibu kuwa " mameneja wanataka pesa ndefu wakati mi
im nalipwa laki nne au tano kwahiyo sitaweza mimi nitalisongesha hivohivo" nikajua tatizo lipo kwa watu wanaisimamia mziki kuwa hawakuwaanda mameneja wengi kwa hiyo wanazidiwa na wasanii.

Naomba tujikute tunakataa kufanya mambo bila kufikiri vyema athari zake hii inatupa funzo kuwa kabla ya kufanya jambo lolote hakikisha umetafakari vya kutosha kujua "uchanya na uhasi" wake ili uone wapi utasimamia baada ya matokeo. Tusiwe wepesi wa kulaumu na kujuta kwa mambo tuliyokwisha yafanya tena yakionesha maandalizi kabisa kama tulikaa tukafikiri na tukaamua kutenda.

Niwape pole wote hasa familia ya Nandy lakini pia mashabiki wake na mimi nikiwepo kiukweli wapo watu waliosema sitaki kuangalia wala kusikiliza tena nyimbo zake huyu binti lakini tatizo ni kwamba 85% ya mashabiki walimchukulia Nandy binti mdogo mchanga sana aliyefanikiwa haraka kutokana na kipaji chake lakini wakasahau yeye ni binadamu kama walivyo wengine.

Hivyo sifa ya ukamilifu wa binadamu ni ukosefu hivyo tukubali Nandy amekosea kama binti yeyote anavyoweza kukosea katika Jamii tumsapoti tukimuacha hapa kwa sasa kwa maana ya kumzira basi tutakuwa tunamzima kama mshumaa ulioweka ufukweni.

Usiku mwema.

Soma: Msanii Nandy aomba radhi baada ya video yake ya faragha akiwa na Billnass kusambaa mitandaoni
 
Atakua mwehu!
Simu ushike ujirekod mwenyewe halafu zikivuja uende mahakamani?

Akaushe tu yatapita ila baada ya muda maana Wabongo hawana dogo wanamuogesha kweli kweli kwa matusi ya maana huko insta..
 
Masikinii kivurugeee
Unajua siku zote ktk maisha. Ukishindwa kujiheshimu ww hakuna atakaye kuheshimu.
Hayo mambo kila mtu anafanya lkn kitendo cha kujirekodi ni cha kijinga sana.
Unatakiwa ujue ''mambo ya chumbani yabaki chumbani na haurusiwi kuchukua picha/video yyte ile yanayohusu mambo ya chumbani lbd km ni mcheza X).
 
Huyu binti amenisikitisha.mbaya zaidi baba yake na mama yake wapo hai na wanaonekana ni watu wanaojiheshimu.
Duh, hataree sana dada zetu sijui wanahisi wapo peke yao tu kwenye ukoo hawafirii kuhusu wadogo zao na ndgu wengine mpaka wanaamua kuruhusu kuona anal sex mchezo wa kawaida in short Yule binti anapigwa ndgo..duh.......
 
Back
Top Bottom