Picha sio umati: Nape atamba kumuumbua Dk. Slaa kesho Singida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha sio umati: Nape atamba kumuumbua Dk. Slaa kesho Singida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 10, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  *Nikiangalia Picha za Mikutano ya Chadema, Naona Umati Mkubwa wa watu na sioni T-Shirt za Chadema, Khanga n.k kama picha chini zinavyoonyesha, Umati mdogo wa watu inaonyesha wamepewa asante...

  2011

  NAPE ATAMBA KUMUUMBUA DK. SLAA KESHO SINGIDA  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo atamwaga hadharani jinsi Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa anavyofanya ufisadi wa kutisha ndani ya chama hicho.

  Nape alisema ataeleza ufusadi huo, katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Stendi Kuu ya Mabasi mjini Singida mjini, ukiwa ni mkutano wa pili, katika ziara ya viongozi wa Sektretarieti ya Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM waliyoianza jana mkoani hapa.

  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya jengo la Ushirika Ikungi nje ya mji wa Singida, Nape alisema, anazo nyaraka zinazoonyesha Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wa Chadema wanavyojinufaaisha na fedha za chama hicho huku wanachama wenyewe wakiendelea kumpigia makofi.

  Katika ziara hiyo ya kujitambulisha msafara wa Sekretarieti hiyo ya CCM, unaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Kapteni Mstaafu, John Chiligati Nape amefuatana pia na Katibu wa Uchumi na Fedha, Mchumi Mwigulu Nchemba na Katibu wa Oganaizesheni Asha Juma Abdallah.

  Katika mikutano iliyofanyika jana, Ikungi na Ligwa, Nape alikanusha vikali kuwepo wa waraka wa siri wa Sekretarieti mpya ya CCM ambao Dk. Slaa anadai kuwa nao.

  Amesema, kwa kujitapa kwenye majukwaa juzi mjini Sumbawanga, kwamba anazo nyaraka za siri za Sekretarieti hiyo, kwanza inadhimhirisha kwamba hajui nini maana ya siri na dhahiri.

  Nape alisema, anachokiita Dk. Slaa kuwa siri ni udhanifu wa kupuuzwa kwa sababu yote yaliyoainishwa kwa ajili ya kutekelezwa na sekretarieti ya CCM baada ya kikao cha mjini Dodoma, hakuna hata moja ambalo ni siri hadi sasa.

  Alisema, baada tu ya sekretarieti kukabidhiwa mikoba, imefanya mikutano ya hadhara zaidi ya kumi katika mikoa mbalimbali na kuelezwa kwa kinaga ubaga nini hasa kilichotokea Dodoma hadi kupatikana kwa sekretarieti mpya.

  Nape alisema, pamoja na mambo kadhaa wamekuwa wakieleza wazi kwamba kilichofanyika ni CCM kujifanyia tathmini kuona kama kweli hali ilimo sasa na inatosha kuipigisha hatua ya kuongoza sasa na baadaye.

  Alisema, baada ya tathmini hiyo, kama chama komavu kiliyakubali mapungufu kiliyobaini na kuamua kwamba ili kuondokana na mapungufu yaliyobainika, lazima uongozi wa juu uliopo uwajibike, jambo ambalo hakuna chama kingine kinachoeweza kuthubu kikabaki salama.

  "Jamani tilichofanya Dodoma ni kuwasha Mwenge kwa ajili ya kuongeza matumaini pale yalipoanza kufifia, kuongeza imani kwa chama pale ilipoanza kudorora, jambo ambalo kwa chama chenye umri mkubwa kama CCM lilikuwa la lazima", alisema Nape.

  Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Chiligati alisema, anachodai kuwa nacho Dk. Slaa na kukiona kuwa ni waraka wa siri, kama kweli anacho ni gamba ililotupa CCM ambalo linamyima usingizi.

  Chiligati alisema, kwa kawaida kitu kinapokuwepo muda mrefu sana kisipojitazama upya kuendelea kuwepo kuwa kwa mashaka makubwa, na ndiyo maana CCM imeona umuhimu wa kujitathmini na kuamua bila kusita kujivua gamba.

  Alifafanua kwamba, gamba ililojivua CCM si ngozi ila ni yale matendo maovu ambayo baadhi ya viongozi walianza kuyakumbatia kama ufisadi, na kutokifanyaa chama kuwa cha wanachama badala yake kuonekana cha wenye fedha.

  Chiligati alisema, kimsingi ufisadi na hali hiyo ya kutokifanya chama kuwa cha wanachama ndilo gamba lililovuliwa toka CCM amabalo sasa Dk. Slaa anataka kutamaba nalo wakati CCM walishaachana nalo tangu mkutano ule mzito wa Dodoma.

  Kwa upande wake, Nchemba alisema, kwa kujivua gamba sasa CCM ni mpya, wale waliokuwa wamekimbia kutokana na kero za baadhi ya viongozi, sasa warejee kwa sababu yale hayawezi kujirudia tena.

  Alisema, sasa CCM ni itaendesha mambo yake kisasa na kisayansi zaidi kuliko ubabaishaji, amkbapo mali na miradi ya chama popote ilipo haitaweza kutafunwa na mbadhirifu yeyote bali rasilimali hizo zitakuwa kwa manufaa ya wanachama wote.

  Miongoni mwa viongozi wa Sekretarieti hiyo mpya ambao hawapo kwenye ziara hiyo mkoani Singida ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye ana majukumu mengine.

  Posted by: Bashir Nkoromo at Tuesday, May 10, 2011 0 Comments

  ZIARA YA NAPE, CHILIGATI NA NCHEMBA SINGIDA YAANZA  [​IMG]
  Nape akihutubia mkutano wa hadhara viwanja vya Ushirika Ikungi nje ya mji wa Singida LEO
  [​IMG]
  Nape akikumbatiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Joram Alute katika mapokezi ya , Ikunga.
  [​IMG]
  Chiligati alipungia mkono wananchi baada ya kuwasili na viongozi wa sekretarieti Ikunga, Singida. Kuhsoto ni Asha Juma abdallah, Mwenyekiti wa CCm mkoa wa Singida Joram Alute, Mwiguku Nchemba na Nape.
  [​IMG]
  kina Mama wa Ikungi wakisgangilia viongozi wa sekretarieti.
  [​IMG]
  Wana-CCM wakimsikiliza Nape, Ligwa Singida.
   
 2. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,186
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Watu wenyewe wachacheeeeeeeee hivi kweli hao ndio wapenzi wa chama huko singida?
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,715
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Dogo Nape, sasa anataka kudandia gari kwa mbele. Hebu kwanza atuambie tambo zake za mafisadi na siku tisini zimeishia wapi?
   
 4. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  Nape hana lolote,
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Duh!!!!!!!!!!! Inasikitisha kumbe hata hukom mikoani chama cha magamba kimekosa mvuto hivyo!!!!!!!!! Watu utafikiri wako kwenye mkutano wa serikali yaMtaa, na huyo Chiligati huko si ndio kwa majirani zake nae hapewi suport, kweli safari ya kujivua ngozi ni ndefu. mjivue ngozi sasa maana magamba hayatoshi
   
 6. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  picha hizi zingepigwa kwa mbali ili kuona ukingo wa watu walipoishia ingekuwa vizuri kuhukumu wingi au uchache wa watu na kuwa rahisi kuelewa uhalisia wa jambo na kuchambua kinaga ubaga. kawaida ukipiga picha kwa ukaribu ni vitu vichache huonekana tena kwa ukubwa wa hali ya juu, na hii ndio tabia ya aina ya picha ambayo kitaalamu huitwa horizontal au ground photograph, sifa yake kuu ni kwamba vitu huonekana kwa ukubwa kadiri vinavyokuwa karibu na kamera na jinsi unavyosogea mbali na ndivyo vitu vinapokuwa vidogo, na wala haiwezi kuonyesha sehemu kubwa kama zilivyo hizo picha hapo juu na kinyume chake ingependeza kama ingewekwa picha aina ya oblique ambayo ingekuwa imeonyesha sehemu kubwa mpaka horizon. ila kila la kheri katika mapambano dhaifu ya kulikomboa taifa hili masikini.:happy:
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,588
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  ****** ya kuku yana mafuta pia.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,293
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  hata hawaeleweki magamba ina maana ni sekretarieti au ni ufisadi?maana naona dereva ni yule yule mbovu mpaka gari likaenda mrama bado yupo!nina choona ni baadhi ya wazee ccm kuwapa madaraka watoto wao nnauye,makamba,mwinyi etc!pili hembu wazungumzie jinsi gani wanavyopambana tuondokane na haya maisha ya kinyama sio kuleta bla bla za kujilimbikizia wao!nape naomba utafakari mnatia kinyaa
   
 9. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaishiwa huyu naombeni wanajf mniachie huyu kijan nimkimbize kwenye miba kama atahimili
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,841
  Likes Received: 2,070
  Trophy Points: 280
  keshazibwa mdomo mpuuuzi huyo hana lolote uroho kwenye madaraka tu.................
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 6,842
  Likes Received: 1,024
  Trophy Points: 280
  Hawa wapuuzi wanafanya siasa wakati taifa linaangamia kwa uchumi teh teh. Wafanyakazi wanasota kupata mishahara lakini wanasiasa wanapata ruzuku za kuzunguka. Mbona sijasikia ruzuku kuchelewa? hivi serikali inasubiri nini kufuta hizi ruzuku?

  Yani wanafunzi hawapewi fedha bure lakini wanasiasa wanapata mabilioni bure bure tu na watu wanawashabikia. Amkeni.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kumbe singida ni mji wenye watu wachache sana! duh mbona idadi ya kura za Mbunge zilikuwa nyingi sana au ndio mambo ya kuiba kura vijijini na mikoa iliyoporini?

  Sasa Nape mbona kila siku atakuwa anaibuka na mambo hasiyo yaweza lile la mafisadi alipiga kelele sasa kanyamaza bila lolote, anataka tena kuja na Slaa? au hana elimu yoyote na kama kaenda shule hajaelimika, maana hana stragegy ni kulopoka bila kujua analoongea, watu wazima ndani ya CCM walijua siku nyingi kuwa Ufisadi ndio CCM hakuna wakufukuza maana Rais anaweza kuwa mchafu kuliko hata hao wanatajwa ila yeye kwavile hatumii vizuri akili alianza kupiga kelele bila kusoma na kuelewa vizuri swali! matokeo yake kaumbuka yeye na kelele zake.
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ninachoshangaa Nape ameshabadilisha lugha. hasemi tena kuhusu siku tisini wala barua. kwa jinsi wana ccm wanavyosubiri kwa hamu watu watimuliwe kisipofanyika kitu mtajimaliza kabisa jamani
   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,237
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mbona magamba bado yapo? Ni CCM ipi iliyovua gamba? Au ni mpaka siku 90 ziishe??
   
 15. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,186
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hapo huitaji zooming kijukwaa chenyewe kinajieleza. hamna kitu hapo. Ngoja siku pipozzz wakitua hapo utauona umati
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 32,124
  Likes Received: 7,086
  Trophy Points: 280
  Jamani hapa duniani kila kiumbe mungu kampa kipaji chake, kipaji cha Nape hiki hapa chini.

  13.JPG
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,025
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Masikini chama cha magamba bado mama zetu wanawapa moyo japo naona kwenye nyuso zao nao wamekubali hiki chama ni cha magamba wamedoro!
   
 18. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nape na Ridhiwani naomba Kaka Nanyaro uniwekee bili ya Maziwa na Pumpers bado ni watoto sana
   
 19. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwi kwi kwi, ooooh!
  Eti kwa kujivua gamba ccm imekuwa mpya na itaendesha mambo kisayansi.
  Tehe tehe teheee! Kwani hiyo sisiem kuukuu au chakavu iliyovuliwa kama gamba iko wapi? Au na yenyewe haionekani mpaka ku-mkonsalti yule mtu anayetoa ulinzi wa viumbe wasiyoonekana.
  Hakika nyani akitaka kufa miti yote huteleza!
   
 20. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,649
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Kama KIDUKU vileeee....hebu ukuzeni basi tuone vyedi.
   
Loading...