Picha sio umati: Nape atamba kumuumbua Dk. Slaa kesho Singida

Mwambieni kijana nape Dakta wa ukweli si saizi yake. Aendelee kujivua magamba kwanza.
 
Ni warejeshe kidogo kwenye zile T-shirts walizovaa watanganyika hao hapo juu, sijui kama nakosea
mimi naona ni kama wafungwa wa kifungo cha nje, kwa hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, kama sio ufungwa basi ni fikira duni kwa watanganyika hao !
 
Ukisoma habari hiyo utagundua kwamba tayari secretariat mpya imeishaanza kukimbia hoja ya kuvua magamba ambayo iliwapa umaarufu mkubwa sana siku za mwanzo za Operation Vua Magamba.

Chiligati anataka kutuaminisha kwamba kujivua magamba ni kubadilisha uongozi. Tatizo siyo uongozi pekee bali ni sera ya chama ya kukumbatia ufisadi.

Mchemba anasema kwamba resources za chama hazitakuja kuliwa tena na wajanja wachache. Hivi ni lini watanzania walilalamika kwamba mali za CCM zinaliwa na wajanja wachache au kuna ufisadi ndani ya chama chao. CCM kila mara imekuwa ikiwachukulia hatua wale wote ambao wamekuwa wakitafuna mali za chama, lakini mafisadi wa mali za umma wakiachwa.

Nape amekosa hoja na sasa anaanza kumsakama Dr. Slaa. Kwanini hizo nyeti alizonazo hakuzitoa jana kwenye mkutano huo na kwanini asubiri mpaka kesho?

Nilisema hizi mbio za kufukuza mafisadi kwenye chama ni ngumu maana ni mbio za sakafuni, ukifika kwenye ukingo huwezi kuendelea kukimbia lazima usimame au urudi ulikotoka.

Yangu macho, CCM imefikia mwisho. Ama iwaache mafisadi chamani na kiendelee kuchukiwa au iwafukuze chamani halafu na wao wamwage hadharani nyongo yao. Mwisho wa siku ... wote watakosa, na hakuna ambaye yuko tayari kukosa.
 
Picha hizo zinajieleza kabisa kwamba Chama Cha Magamba kwishilia mbali. Ninafikiri hata picha ingepigwa kwenye kilabu ya pombe kutakuwa na watu wengi kuliko hao waliohudhuria huu mkutano. Na huyo babu aliyebeba jambia sijui ni ishara gani? Anaonekana ana njaa kweli kweli na pengine hajui anachokifanya:happy:
 
Huyu Nape sijui Nepi naye huwa namwona kama vuvuzela Hizza tambwe, mwache angilie biashara asoiweza itamkimbiza tu!
 
Zile nyimbo zake za RACHEL mafisadi nimewakere wenye chama,
naona sasa anatubadilishia chorus
mwaka huu kazi hipo, akamuulize mbunge wa kinondoni,
wenzake walikuwa wanatania kuhusu kujivua magamba hakusoma vizuri
wamemvua yeye.
huyu naye sio muda ataropoka matokeo yake chama kitaingia kwenye matatizo watamvua gamba.
 
Haha....!eti wameanzia kwa Tundu Lissu(Ikungi),mbona maendeleo hawaanzii huko?wameondoa walimu wote wazuri kwa Tundu ili pazidi kudorora wanaoumia ni watz sio Lissu.
 
Dogo Nape, sasa anataka kudandia gari kwa mbele. Hebu kwanza atuambie tambo zake za mafisadi na siku tisini zimeishia wapi?

Achana naye mtoto anataka kukulia kwenye migongo ya watu wakubwa! Naona ameshtukia kuwa kwa Lowasa kachemsha, itakuwa kwa Slaa Dr? Huyu kijana naona anasumbuliwa na cheo tu!
Wauza sura hao, kijana anajichubua huyo! Nafikiri anadhani tutachagua na na kushabikia tena sura kipindi hii! No!
 
Wahenga walisema kuchamba kwingi utashika mavi.Nape hana lolote.mda si mrefu atashika mavi kama baba janualy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom