Picha nyingine zinajieleza

tatizo lenu nyie chadema udini unawasumbua, fitna majungu na kelele nyingi kwa zito sababu ni muislam

wewe ndo udini unakusumbua, nani kaongelea hayo hapa.... acha fikra za kibaguzi
mbona zito mwenyewe hajawahi sema na bado ni mwema kwa chama chake
acha kuleta udini kwenye vichwa vya watu
 
kwakua nyie chadema mna agenda ya udini nyuma ya pazia,bac muweke na alama ya msalaba kwenye bendera yenu ili muwe open zaidi.

walioipigia kura chadema ikashinda je ni wakristo tu????
mbona mlitangaza igunga watu wasiwapigie kura chadema na bado wakapata za kutosha kuliko hata chama cha CUF
AMBACHO WAISLAM walitaka kipewe kura....so mnataka nn nyie mlianza kuiunga mkono CUF imewashinda tuacheni na CHADEMA YETU jamani
 
Kwa taarifa yenu hakuna Chama chochote cha siasa nchi hii kinachohusudu udini, ukanda, umtandao, ukabila kama chama cha magamba. Hebu chunguza hata teuzi zinazofanywa sasa hivi ndo utajua. Ila tu nionye tu kwamba chama chochote kinachoendekeza mambo hayo, lazima ujue kwamba hakina dira, mwelekeo, maono wala itikadi madhubuti. Kwa hiyo hapa tusiishie kushambulia chama, ila tuambizane kama taifa kitu gani tunatakiwa kufanya. Kwanza watu wenye dini za asili hapa Tanzania ni wengi kuliko wakristo na waislam. Sasa mijadala kama hii tija yake nini hasa?????
 
udini upo wala msibishe na mkae mkijua hilo ndio litakuwa tatizo lenu kubwa uko mbele ya safari

si mnawakumhuka cuf walivyoonza na mambo yao ya kidini sasa kwishney nanyi msipoangalia

itakula kwenu-kwenye ukweli jaribuni kuwa wapole msiwe kama mpunga una rangi gani
Kilichoipeleka CUF chumba mahututi si udini uliokuwa ukipigiwa upatu na CCM bali kuji- identify kwao na genge la mafisadi hawa. Ndoa yao na CCM imewachanganya wananchi kiasi cha kuamini kwamba kumbe walipotea njia na kwamba CUF na CCM ni wamoja! CCM (Haswa wanapozidiwa) ni hodari sana wa kucheza karata za ukabila, ukanda na udini ili watekeleze malengo yao. Mwaka 1995 walihaha wakinadi NCCR ni ya wachagga na kwamba kuiweka madarakani ni kuwakabidhi nchi! Mwaka 2000 CUF walipokuwa na nguvu waliwageuzia kibao na kunadi wana sera za kidini ingawa cha kushangaza leo wamefunga ndoa na walewale watuhumiwa wa udini na hatuwasikii tena CCM wakimtuhumu mshirika wao huyo kwa udini bali CHADEMA. Mwenye akili timamu yeyote ataelewa udini na ukabila wa CHADEMA ni propaganda za CCM ambazo sasa wananchi wamezielewa vema na hawadanganyiki tena. Kuanzia mwanzo CHADEMA ilikuwa na mseto wa viongozi wa dini na kutoka maeneo mbalimbali. Hebu tujikumbushe waliopata kuwa viongozi wa CHADEMA; Mtei alikuwa Mkristo, Bob Makani Mwislamu, Dr. Aman Kabouru mwislam, Shaibu Akwilombe mwislamu, na sasa Makamu Mwenyekiti Mh. Arfi ni mwislamu n.k. Kisha chunguza hao wanatoka wapi? Mtei anatoka Kilimanjaro, Bob Makani Msukuma, Kabouru anatoka Kigoma, Shaibu Akwilombe (Aliyekuwa Makamu Katibu Mkuu hadi alipokimbilia CCM) ni wa kusini sasa ukabila na udini uko wapi hapo? Ukweli ni kwamba sera hizi za kijinga zinapuuzwa na wananchi, ndiyo maana CHADEMA imeendelea kujizolea umaarufu zaidi na kuchaguliwa na wananchi kuongoza majimbo mengi zaidi ya chama chochote cha upinzani kwa sasa katika nchi hii.

 
Kuna watu wengine wapo huku kwa bahati mbaya walitakiwa wawe kwenye magazeti ya udaku. Unapozungumza jambo ni vizuri ukawa na uhakika nalo. Kwamba mtu akiguswa hata kama ni kweli au watu wanatafuta ukweli mtu unakimbilia kwenye dini yake au kabila lake, hii inaonyesha jinsi uwezo wako wa kufikiri ulivyo mdogo. Na usifikiri ni lazima tu watu wakubaliane na yale unayofikiri au kuyapenda na tusipofikiri au kukubaliana na wewe ni kosa. Jipange tena mkuu acha porojo hili ni jamvi la watu wazima.
 
Nduguyangu tatizo la Zito si ndege si mnyama mafisadi wa magamba wanamtumia , wewe unaona ni sawa alivyotangaza kugombea uraisi wakati anajua chama kipo kwenye kampeni Arumeru?

Alafu wanaomtetea ni magamba wanaweka hoja zisizo na msingi
 
Kwani Zitto kwa uislamu wake hamuamini Mungu? Wewe ndo udini unakusumbua! Wenzako tunaona 'harmony' tu hapo.
tatizo lenu nyie chadema udini unawasumbua, fitna majungu na kelele nyingi kwa zito sababu ni muislam
 
NIKIFANYA KAZI NA MTU KAMA HUYU WA KULIA NITAKUWA SIMRUHUSU AiNGIE OFISINI KWANGU KAMA SIPO!!!!!!​

Huyo mwa mwisho kulia katika picha hii macho yake yamekaa kichawi chawi tu; hana kheri na chama hiki hata kidogo kitu asichojua ni kwamba nje ya Chadema yeye si lolote si chochote. These people do not learn ,amuangalie mgoma mwenzie Kaborou alivyochezewa na ccm na sasa anasaga rami baada ya kudanganywa na Makamba kwa ubunge wa E.A. wa term moja!!,
 
zitto ni mpumbavu sana, hawezi kumtukana mzee mtei kiasi hicho. siku zote amekuwa kikwazo cha chadema na watz. naomba kwa leo nijizuie nisiropoke iki nilichonacho juu yake kwasababu ataaibika mno. pusi.
 
Who is Zito? . Great thinkers; achen kujadili watu; jadilini masuala ( issues). Tunahitaji nn kama taifa in a short term, medium and in the long term. Then tu-analyse the candidates along our needs as the nation. Mmemsahau LUSINDE or you are now trapped by Lusinde? Tusijadili masuala ya Zito kama tunatafuta Shekhe, au mchungaji au Handsome. Tunahitaji kiongozi that is it. Nadhan kiongoz Bora ni yule anayeunganisha watu na rasilimali zao katika kusukuma gurudumu la maendeleo ( kwa busara na hekima). So along the creteria ndipo tuweza kusema Labda Zito au mwingine atatufaa. Ni mawazo yangu tu wakuu.
 
yewii nimecheka mie kwa kweli jinsi ulivyoieleza... nice one.

maana atawish picha isingepigwa duh
 
Back
Top Bottom