ArD67
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 2,817
- 2,045
Mkuu kanda ya ziwa huku ni kweli mazao yanakauka, na vuli ndo msimu wao wanaoutegemea. Na wako wengi sana hawa jamaa, huku kuna famila yenye watoto 70 ni hakuna yenye chini ya watoto watatu.Sasa hao wafanyabiashara wataiona lini hiyo fursa. Brazil walipewa kibali kuagiza mahindi ya kulisha kuku?
Lakini fact ni kwamba kuna sehemu wana njaa kali, na wamesema wenyewe. Sasa kama rais alifika huko kwao ulidhani wangemwambia nani badala yake? Juzi kati hapo niliona taarifa ya habari wananchi wanampokea mkuu wa mkoa na mabua ya mahindi au walikuwa ni wanafiki fulani tu?
Hatua zichukuliwe tu, hata za kuwalazimisha wauze mifugo na waletewe mahindi wanunue kwa bei nafuu.
Wafanyabiashara si wakuwategemea sana, kwao kufa ni kufaana tu, kwa sasa debe (20kg) au hazifiki ni _sh. 15-20...na mifugo imeshuka bei... Wiki iliyopita mbuzi waliuzwa hadi 20 elfu. Kwahyo debe moja kwa mbuzi mmoja tu.