Picha nne ambazo ningependa Mh. Rais azione!

Picha nne ambazo ningependa Mh. Rais azione!

Kumekuwa na ubishani kuhusiana na hali ya njaa nchini na mengi yemeongelewa. Lakini ili kutatua ubishani huu na 'kumaliza' malumbano, ningeomba picha hizi zimfikie mheshimiwa Rais.

View attachment 458424 View attachment 458428 View attachment 458431 View attachment 458432

Assesment yangu ni hivi:

In general, sehemu kubwa kulingana na picha zilizopigwa na mtandao wa Google Earth zinaoesha kuwa zaidi ya asilimia sabini ya nchi iko katika hali ya ukijani.
Hiyo asilimia kama thelathini iliyobakia, acccording to Google Earth ni mikoa kama ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, na nusu ya Singida inaonekana kuwa na ukijani, ihali nusu ikionekana kuwa na hali ya jangwa.

Kwa kutumia picha hizi za google earth ninamuomba muheshimiwa kuwa watu wa mikoa hii ambayo inaonekana kuwa imeathiriwa na ukame, wapate msaada wa chakula cha dharula iwapo hali itabidi, pia wale walio na mifugo kwenye maeneo haya yalioathiriwa na ukame, waruhusiwe kuihamishiak wenye mikoa inayonekana kuwa na hali ya kijani kibichi kama inavyoonekana kwenye picha za Google Earth.

In general,
Naungana na mheshimiwa Raisi kukiri kuwa suala la ukame limekuzwa na wafanya biashara na wanasiasa wenye nia ya kuichafua serikali yake, kwani kutokana na assesment yangu ya picha za google earth, inaonekana sehemu kubwa ya nchi ikiwa katika hali ya ukijani....
Mwisho wa Mjadala...
mkuu naona tuanzie hapa, umewahi kulima?
 
Hali halisi ya bara la Afrika ikilinganishwa na Tanzania kwa ujumla kulingana na picha za Google Earth...
Pichani, nchi nyingi za barani Afrika zinaonekana kuwa zimeshambuliwa na ukame, na kulingana na picha hizi, Tanzania inaonekana kuwa ina nafuu kwa kiwango kikubwa. Hata kama kuna maeneo yameathirika na ukame, bado ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa kuna maeneo yana unafuu na kuwaonya wanasiasa uchwara waache upotoshaji wa hali ya nchi... Google earth ni mtandao wa kitaalam, hapa hamna siasa wala propaganda. Kama kuna mwana siasa anataka kubishana na picha za satelite na ajitokeze, sasa, la sivyo akae kimya milele...
View attachment 458453

Kodofan toa maelezo ya uhusiano wa Google Earth pictures na farming system ya Tanzania inayotegemea mvua kwazaidi ya 80% siyo maelezo ya Geographical interpretation ya picha. Sasa uliza marafiki wako walioko mikoa 5 (the big 5) ya uzalishaji wa mazao ya chakula, kiufupi Mimi nipo huku na nipo kwenye sector hiyo kwahiyo Google Earth haiwezi kutumika kubadilisha ukweli kwamba " unequal distribution of rainfall trends caused by climate change" na sasa mvua is unpredictable watu wana-abandon fields zao refer TMA watoe taarifa za uhakika wa mvua kwa msimu huu halafu watu wapime.
 
We ukiona ukijani unajua ni chakula,hiyo elimu yako umeipata wapi? Yani hizi elimu za kukalilishana hizi zina madhara makubwa sana.haya google na bei ya vyakula ulete hapa
Hahahahaaa.... Umenichekesha aisee.. Kwel agoogle na bei kabisa
 
Inasibiri hotuba ya rais ya kinaz ndio unajifanya umuunga mkono kwa kutuletea picha za kinafiki za Google njaa ipo cku zote akieshiba hamjui mwenye njaa yeye yupo ikulu kila kitu anapata bure tu hatoi hata sent tano yake unajifanya unamuunga mkono kwani swala LA kujua kama kuna njaa ai hakuna ww binafsi unaangalia nini ili kujiridhisha
Kwa kifupi tunaangalia mfumko WA bei katika mazao ya chakula kama njaa hakuna kwa nini beo ya vyakula inazidi kupanda kila siku
 
Duh. Kweli elimu elimu elimu.
Unashindwa connect the dots ukijani na mvua na chakula?? Huo ukijani pia ni misitu ambayo ni dense na inahitaji mvua ya kutosha ili iwe kijani, anzia hapo kuelewa uhusiano na ukijani na chakula, toka nje ya boks!!
Dah we jamaa umetoa majibu mazito sana kwa swali jepesi nauakika hatojibu tena text yako akijitaidi atakushambulia kwa kukutukana bas
 
Sehemu yenye kijani maana yake watu wangeweza kulima na kupata chakula; sasa kama watu ni wavivu mnataka Rais awalimie EBOO! Hata hivyo kama watu wa sehemu moja ya nchi wakipata ukame na wakawa na uhaba wa chakula je hiyo ndio maana yake nchi nzima ina njaa? Kama kuna mahindi ya ziada huko sumbawanga na Songea kwanini wafanya biashara waagize toka Brazil wakati kuna mahindi Katavi? Serikali itawajibika pale tu nchi nzima ikipatwa na baa la jaa na sio sehemu ya nchi ambapo wananchi wanaweza kuuza mifugo yao na kununua chakula badala ya kulimbikiza mifugo dhaifu huku wakitegemea serikali iwaletee chakula!!
1. Sehemu zenye kijani ni misitu minene ya asili na mapori na mashamba ya misitu yaliyohifadhiwa na serikali, mama yako anaruhusiwa kulima huko?
2. Hii nchi ni kubwa na jiografia yake ni tofauti kabisa. Unazungumzia Sumbawanga kuwa na mahindi ya ziada wakati wengine hawana. Hizo ni tofauti za kijiografia na hii nchi siyo Sumbawanga.
3. Hao wafanyabiashara wameagiza mahindi kutoka Brazil bila idhini ya serikali? Hilo ni suala la wananchi sasa?
4. Kwanini serikali isiratibu usambazaji wa hiyo ziada ya mahindi ya Sumbawanga yawafikie wanaoyahitaji?
5. Wapi wananchi wamesema wapelekewe chakula cha bure? Wanataka chakula cha msaada au cha bure? Sambazeni chakula watu watanunua.
 
  1. Kipindi cha uhaba wa sukari alisingizia, kuwa wafanyabiashara wameficha.
  2. Likaja suala la fedha kuadimika, nazo akasema kuwa mafisadi wameficha fedha.
  3. Issue ya DANGOTE akasema ni wajanja walitaka kujinufaisha na mradi huo.
Sasa kwenye suala la njaa, wanasingizwa waandishi wa habari...!
Mbona unatoka nje ya mada!

Mbona unasahau yaliyosemwa kuhusu avatar ya ID yako!

Mbona una mawazo mgando kwa masuala mazito ya kitaifa!

Picha za google zinatupa fursa ya kuchukua hatua sambamba na taarifa za hali ya hewa kwamba tuchukue hatua za kuweka hifadhi ya chakula majumbani mwetu, kwa mkulima na asiye mkulima,na siyo kutegemea chakula cha msaada!

Bei za vileo na sigara hupandishwa kila siku, lakini Watanzania hawaachi wala kupunguza kiasi wanachotumia, lakini wakati uleule wana njaa wakisubiri msaada wa serikali.

Wakulima wanauza chakula, na wengine wanatengeneza pombe, bila kujali kuweka akiba.

NAMBA TUTAISOMA
 
2. Hii nchi ni kubwa na jiografia yake ni tofauti kabisa. Unazungumzia Sumbawanga kuwa na mahindi ya ziada wakati wengine hawana. Hizo ni tofauti za kijiografia na hii nchi siyo Sumbawanga.

Sumbawanga ni sehemu ya Tanganyika hivyo kama Mbulu kuna njaa basi na wambulu wana uwezo wa kununua hicho chakula hakuna sababu ya kuomba serikali iwapelekee chakula kwani wafanyabiashara wataiona hiyo fursa na kupeleka mahitaji hayo huko!! Ninavyowaelewa hao wanaoomba chakula wanataka chakula cha dezo na sio kununua kutoka serikalini!! Na ndio maana wameambiwa safari hii "MWAFA"!!!!
 
Njaa kubwa itatokea Tanzania mwaka huu. Hapa tunaweka matumaini ktk mvua za msimu wa masika tu. Zije kwa wakati na zitosheleze.

Hata hivyo, mikoa ya kanda ya ziwa, haswa mwanza, simiyu na shinyanga, sina uhakika na mara, mvua za vuli ndo tegemeo lao kuu na hazikunyesha ipaswavyo, mimea inakauka huku.

Wasukuma wako wengi sana, (population) wanajua kufyatua watoto. Na wako vizuri ktk kula, wanakula chakula kingi nadhani kupita jamii nyingine zote, nadhani ni kwa utendaji wao wa kazi.

Sasa hapa linazaliwa tatizo, hizo mvua za masika hata zikinyesha zakutosha ktk hiyo mikoa, je wataweza kuzalisha kingi na cha ziada cha kuwalisha na hawa watani zangu huku?

Harakati zipo, kuhamasisha jamii kama mvua itatokea, wapande mazao yenye kukomaa haraka (viazi vitamu) na yale yenye kustahimili ukame.

Nadhani, kitaifa lifanyike jambo kwa haraka... kwanza uzalishaji wa chakula uongezwe kwa maeneo yote yenye uwakika na mvua za masika, mikoa ya Morogoro, mbeya, iringa, ruvuma na rukwa.... na kwingineko kote zitakaponyesha. Watu wazalishe maradufu, walime zaid kupita miaka yote.

Suluhisho la kudumu, umwagiliaji. Janga hili liwe fundisho kwa taifa. Njaa kubwa inaweza kutukia na kusimamisha ndoto zetu zote. Chakula ndo msingi wa maisha na ndo kipimo cha ustawi wa jamii yoyote ile duniani.

Usafirishaji, mawasiliano, elimu, afya, majengo na chochote si vya msingi penye njaa. Mi huwa nashangaa hivi kwanini hatuna mashamba makubwa kama ya mkonge, kahawa, na miwa yenye kuzalisha mahindi na mpunga Tanzania? Bado tunauishi ukoloni wa mjerumani hapa. Bajeti ijayo kipaumbele kiwe hicho. Njaa haifichiki wakuu, na hakuna raisi atakaye acha raia zake wafe kwa njaa.
Tutaliacha li boing na kuagiza mchele Thailand na vertinam huko. Tujisawazishe.
 
Sumbawanga ni sehemu ya Tanganyika hivyo kama Mbulu kuna njaa basi na wambulu wana uwezo wa kununua hicho chakula hakuna sababu ya kuomba serikali iwapelekee chakula kwani wafanyabiashara wataiona hiyo fursa na kupeleka mahitaji hayo huko!! Ninavyowaelewa hao wanaoomba chakula wanataka chakula cha dezo na sio kununua kutoka serikalini!! Na ndio maana wameambiwa safari hii "MWAFA"!!!!
Sasa hao wafanyabiashara wataiona lini hiyo fursa. Brazil walipewa kibali kuagiza mahindi ya kulisha kuku?
Lakini fact ni kwamba kuna sehemu wana njaa kali, na wamesema wenyewe. Sasa kama rais alifika huko kwao ulidhani wangemwambia nani badala yake? Juzi kati hapo niliona taarifa ya habari wananchi wanampokea mkuu wa mkoa na mabua ya mahindi au walikuwa ni wanafiki fulani tu?
 
Hali halisi ya bara la Afrika ikilinganishwa na Tanzania kwa ujumla kulingana na picha za Google Earth...
Pichani, nchi nyingi za barani Afrika zinaonekana kuwa zimeshambuliwa na ukame, na kulingana na picha hizi, Tanzania inaonekana kuwa ina nafuu kwa kiwango kikubwa. Hata kama kuna maeneo yameathirika na ukame, bado ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa kuna maeneo yana unafuu na kuwaonya wanasiasa uchwara waache upotoshaji wa hali ya nchi... Google earth ni mtandao wa kitaalam, hapa hamna siasa wala propaganda. Kama kuna mwana siasa anataka kubishana na picha za satelite na ajitokeze, sasa, la sivyo akae kimya milele...
View attachment 458453

Ndugu yangu maeneo ambayo ndiyo wazalishaji wakubwa wa Chakula zimekumbwa na ukame na hakuna mvua zilizonyesha.Hivyo ukijani unaouona si sababu ya hali nzuri za mvua,bali majani yanaweza yakawa kijani sababu ya unyevunyevu tu.

Maeneo yenye uzalishaji ndiyo yaliyokumbwa na UKAME kaka.Pole.kama hujawahi kuwa mkulima usije ukadanganyika na ukijani.Mwanza na Bukoba kuna ukijani lakini kuna njaa
 
Ukame kiasi ulioikumba nchi umesababisha upungufu wa chakula sio njaaa...hivi njaa ni ya kulazimisha kwenye mitandao? Njaa ikitamalaki hakuna wa kubisha sasa mnahangaika kulazimisha njaa? Nani amekufa kwa njaa?
 
Lakini fact ni kwamba kuna sehemu wana njaa kali, na wamesema wenyewe. Sasa kama rais alifika huko kwao ulidhani wangemwambia nani badala yake? Juzi kati hapo niliona taarifa ya habari wananchi wanampokea mkuu wa mkoa na mabua ya mahindi au walikuwa ni wanafiki fulani tu?

Sawa kweli wananchi walimuonesha mkuu wa mkoa mabua kuonesha kuwa mazao yao yamehalibika; sasa kuonesha kuwa mazao yao yamehalibika ndio maana yake kuna njaa?? Kawaida ya watu wa vijijini huweka akiba ya chakula mara mvua zinapokuwa hazitoshelezi na pia watu wa vijini hawategemei kilimo tu kwa chakula bali wanashuhulu nyingine ndogo ndogo zinazoweza kuwapatia chakula ukiwemo ufugaji. Serikali ya JPM inataka kuondoa dhana potofu iliyojengeka kuwa panapotokea upungufu wa chakula serikali itapeleka chakula cha bure/msaada sehemu husika ; hiyo dependecy syndrome ndiyo inayotakiwa kuwatoka wananchi!! Serikali isaidie pale tu ambapo kuna absolute need!!!
 
We ukiona ukijani unajua ni chakula,hiyo elimu yako umeipata wapi? Yani hizi elimu za kukalilishana hizi zina madhara makubwa sana.haya google na bei ya vyakula ulete hapa
Bei ya chakula kuwa juu haimaanishi kuna njaa kwenye njaa hata chakula cha kununua kwa bei yoyote huwa hakuna
 
Duh. Kweli elimu elimu elimu.
Unashindwa connect the dots ukijani na mvua na chakula?? Huo ukijani pia ni misitu ambayo ni dense na inahitaji mvua ya kutosha ili iwe kijani, anzia hapo kuelewa uhusiano na ukijani na chakula, toka nje ya boks!!
Tanzania hakuna njaa bali kuna upungufu wa chakula ambao unafanyiwa kazi hakuna atakufa kwa njaa whatch the space
 
Waihamishie kwenye mikoa ya kijan, halafu kilimo kifanyike jagwan au? We nawe hauko sawa in mind,,, ningekuelewa ungesema mikoa inayooonekana ya kijan isaidiwe pembejeo ili wazalishe chakula kingi kuja kulisha mikoa yenye ukame,
Sasa naona kwako mifugo ni bora kuliko chakula na hujui itasababisha ugomvi?
Umeshafanya utafiti ukaona maeneo ya wazi kwenye mikoa ya kijan au unakurupuka tu?
 
Kilimo cha kutegemea mvua ambao haitabiliki hakiwezi kuondoa tatizo la njaa maeneo yote ya nchi. ukijani hauondoi njaa na wala si kipino kizuri cha kuwepo chakula. Kuna wakulima walilima lakini kwa sababu ya mvua kutokuja kwa wakati mazao yao hayakuota/kukua. Dar es Salaam tumezungukwa na maji kila sehemu lakini tuna tatizo kubwa la maji majumbani mwetu! Yasije yakatukuta ya Ethiopia mpaka watu wa nje ndiyo wakaja kutangaza kuna njaa na kuomba usaidizi wakati wale wa ndani wakikana kuwepo na njaa!
 
Back
Top Bottom